Saturday, October 22, 2016

Ndanda FC washindwa kutamba Mtwara mbele ya Mwadui.


Riphati Hamis na Ally Mohamed wa Ndanda wakishangilia bao la kuongoza baada ya kuwafunga Mwadui katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda Fc. Mwadui walishinda 2-1.




Kipa wa Mwadui Shaban Kado akitoka kuokoa mpira uliokuwa ukielekea langoni mwake katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda Fc. Mwadui walishinda 2-1.


Heka heka langoni kwa Mwadui, mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC  Nangwanda Sijaona Mtwara. Mwadui walishinda 2-1


Mshambuliaji Shija Nkina wa Ndanda FC akijaribu kumtoka mlinzi wa Mwadui FC, katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara. Mwadui walishinda 2-1


Wachezaji wa Mwadui FC wakishangilia bao la pili pamoja na benchi la ufundi lililofungwa na Abdallah Mfuko, katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara. Mwadui walishinda 2-1

Juma Mohamed, Juma Newa

Kwa mara nyingine wakiwa katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara, wenyeji Ndanda FC wanashindwa kuondoka na pointi Tatu baada ya leo hii kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mwadui FC kutoka Shinyanga, ikiwa ni siku chache baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City.

Riphati Hamis wa Ndanda akishangilia bao la kuongoza baada ya kuwafunga Mwadui katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ndanda Fc. Mwadui walishinda 2-1.

 
Ndanda walianza kufunga mapema dakika ya 16 baada ya mshambuliaji Riphat Khamis kuunganisha krosi ya Helbert Lukindo na kuifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Mwadui walicharuka kipindi cha pili kwa kuliandama lango la Ndanda ambapo dakika ya 61 Abdallah Mfuko alisawazisha bao kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu ndogo kabla ya dakika ya 68 kufunga bao la ushindi kwa kichwa tena.

Kikosi cha Ndanda kilichoanza dhidi ya Mwadui. Mwadui walishinda 2-1

 

Kikosi cha Mwadui kilichoanza dhidi ya Ndanda. Mwadui walishinda 2-1

No comments: