BIASHARA

Vodacom watoa barakazao kwa Yanga na Simba kesho Taifa.
 

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa VODACOM,Nandi Mwiyombella, akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Yanga na Simba Oktoba 1 mwaka huu.

Na mwandishi wetu, Juma News.

Wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, kampuni ya mawasiliano ya VODACOM Tanzania imetoa Baraka zake kwa timu za Yanga na Simba katika mzunguko wa kwanza kwa timu hizi kubwa hapa nyumbani  zitakazomenyana siku ya jumamosi ya tarehe 1 mwezi Oktoba katika uwanja wa Taifa jijini Da res Salaam.
“Tunaamini mchezo huu utakuwa mzuri na wakuburudisha washabiki wote wa timu hizi watakaofika uwanjani kuushuhudia kwani ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana tangia msimu huu kuanza,Pia napenda kuwatoa wasiwasi wapenzi wa mchezo huu ambao hawatapata na nafasi ya kufika uwanjani kwani Vodacom Tanzania haitawaacha mbali na matokeo yatakayokuwa yakiendelea uwanjani hapo”LIVE” ili kupata matokeo ya mchezo huo ni rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kujiunga na kifurushi cha ‘Soka bando’ na utakuwa unapata frusa ya kupata matokeo kiurahisi kabisa popote pale ulipo ya timu yako uipendayo kati ya Simba na Yanga.” Anasema Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Nandi Mwiyombella, nakuongeza;

“Kifurushi hiki ni chenye gharama nafuu ya shilingi 500/-ni mahususi kwa ajili ya mashabiki wa mchezo wa mpira wa miguu unaopendwa duniani kote kinawapatia mashabiki wa soka muda wa maongezi wa dakika 14 Vodacom kwenda Vodacom na pia dakika 2 vodacom kwenda mitandao mingine, na pia utapata sms 20 kwa masaa 24.”
Ili kununua kifurushi hiki anachotakiwa kufanya mteja ni kupiga  namba *149 * 01#, Ofa mpya alafu chagua ‘Soka Bando’. Baada ya  hapo mteja atapata ujumbe unaomtaka ajisajili kwa timu ya soka anayoishabikia kwa kutuma jina la timu mfano “Yanga”  “Simba” au “Azam” nk. kwenda namba 15460.Pia mteja anaweza kupata taarifa za soka kupitia tovuti ya  Mspoti.vodacom.co.tz. 

No comments: