KITAIFA



Wazee Newala ‘wamlilia’ DC kusuluhisha mgogoro wa vijiji Vitatu kuhusu uhaba wa maji.
 

Mkuu wa wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo akisalimiana na wazee wa vijiji vya Mnali na Mapinduzi wilayani Newala waliomuomba kufanya kikao cha pamoja baina ya wananchi wa vijiji hivyo na kijiji cha Nanda ili kusuluhisha mgogoro uliopo kati yao.

Juma Mohamed, Mtwara

Kero ya maji iliyodumu kwa miaka 12 katika vijiji vya Mnali na Mapinduzi wilayani Newala mkoani Mtwara, imezua mgogoro baina ya wananchi wa vijiji hivyo na kijiji cha Nanda, na kupelekea wananchi hao kuanza kupeana vitisho hali ambayo imezua hofu kwa wazee wa vijiji hivyo.
Juma News ilifika katika vijiji hivyo na kufanikiwa kuzungumza na wazee hao ambao wanadai kuwa hali ya usalama inaelekea kuwa mbaya kutokana na vitisho vinavyotolewa na vijana wa vijiji hivyo, na kuamua kumuomba mkuu wa wilaya ya Newala Aziza Mangosongo kukaa na wazee wa vijiji vyote ili kusuluhisha mgogoro huo.

Afisa tarafa ya Kitangali, Victoria Fredy, alitoa ushuhuda wa kijana mmoja ambaye hakumtaja jina aliyeamua kuchukua Upupu wa kuwasha na kummwagia meneja wa Maji wakiwa katika shughuli ya kurekebisha miundombinu ya maji.

Mkuu wa wilaya ya Newala Aziza Mangosongo, ambaye amefanikiwa kumaliza tatizo hilo la maji baada ya kuweka kambi ya siku Tatu akiwa na timu yake, alikiri kuwapo kwa hujuma zilizokusudia kukwamisha upatikanaji wa maji katika vijiji vya Mnali na Mapinduzi na kuahidi kukaa na wazee ili kumaliza tofauti zilizopo.

Wananchi wa Mnali na Mapinduzi wameamua kumpa zawadi mbalimbali mkuu wa wilaya kutokana na kufanikisha upatikanaji wa maji katika vijiji hivyo.

No comments: