Tuesday, July 26, 2016

Wahamiaji haramu wakamatwa Mtwara wakijaribu kuvuka Boda.


Wahamiaji haramu waliokamatwa Mtwara wakijaribu kuvuka mpaka wa Tanzania na Msumbiji, katika kijiji cha Kilambo, halmashauri ya wilaya ya Mtwara.



Wanahudumiwa Chai na Mkate



Juma Mohamed, Mtwara.

Idara ya uhamiaji mkoa wa Mtwara imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu Kumi na wanane raia wa nchini Ethiopia wakiwa katika harakati za kuvuka katika mpaka wa Kilambo, halmashauri ya wilaya ya Mtwara kuelekea nchini Msumbiji.
Akizungumza mkoani hapa, naibu kamishina wa Uhamiaji, afisa uhamiaji mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama, alisema wahamiaji hao wamekamatwa huku ikiwa haijafahamika aliyehusika katika kuwasafirisha, na kwamba leo wanafikishwa mahakamani baada ya kujiridhisha kuwa wameingia nchini visivyo halali.
“Sisi kama Uhamiaji ambao ndio jukumu letu kuwashughulikia watu wa aina hii, tuko nao hapa na baada ya muda mfupi tutawafikisha mahakamani baada ya kujiridhisha kwamba wameingia nchini visivyo halali, wamekiuka sheria ya uhamiaji ya kuwapo nchini bila vibali..lakini kama haitoshi waliweza kupita njia zisizo rasmi..” alisema.

Naibu kamishina wa Uhamiaji, afisa uhamiaji mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama.



Aidha, alikiri kuwa mkoa huo unakabiliwa na changamoto ya kutumika kama njia kwa wahamiaji, kutokana na kupakana na nchi ya Msumbiji, nakuwataka wananchi kushirikiana na maafisa uhamiaji katika kutoa taarifa za raia hao, ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Wanarejeshewa Passport zao



Hatua imekuja ikiwa ni wiki mbili baada yawaziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Kassim Majaliwa, kutoa msisitizo kwa Idara hiyo kuhakikisha inaimarisha ulinzi katika mipaka yote inayopakana na nchi jirani ili kudhibiti raia hao.
Mkoa huo umefanikiwa kuwakamata jumla ya wahamiaji haramu 123 kuanzia mwezi Januari mpaka Juni mwaka huu, kutoka katika mataifa Kumi na Mbili na kati ya hao, raia Hamsini na sita ni kutoka nchini Ethiopia.





No comments: