Tuesday, July 26, 2016

Ndanda FC wamrejesha Kapama wao kuitumikia tena.


Nassoro Kapama



Na Juma Mohamed, Mtwara.

Klabu ya soka ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara, inaendelea kuimarisha kikosi chake ikiwa ni kujiwinda na michuano ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya hii leo kumsainisha aliyekuwa mchezaji wao wa zamani Nassoro Kapama kuichezea timu hiyo kwa mwaka mmoja.
Taarifa ya afisa habari wa klabu hiyo, ilieleza kuwa Kapama ambaye msimu uliopita alikipiga katika klabu ya Coastal Union ya Tanga, amerejea Ndanda ambako alikipiga misimu miwili iliyopita kama kiungo mshambuliaji na kwamba ameahidi kushirikiana vyema na wachezaji wenzake huku akikiri kuwa kutakuwa na ushindani wa namba.
“Kikubwa alichokizungumza ni kwamba amefurahi kurudi nyumbani na kuungana na baadhi ya wachezaji wenzake ambao alicheza nao pamoja misimu miwili iliyopita..lakini amekiri kuwa kutakuwa na ushindani wa namba kutokana na ubora wa kikosi ulivyo msimu huu..” alisema Bandari.
Kapama anakuwa mchezaji wa Nne kusajiliwa na Ndanda msimu huu kama mchezaji mpya akiungana na Salum Telela aliyesaini jana, Ibrahim Mamba aliyekuwa Geita Gold Sports na Bakari Mtama kutoka Mgambo JKT ya Tanga.



No comments: