Monday, May 21, 2012

NADAL AMGARAGAZA DJOKOVICK


Rafael Nadal
Nadal sasa anashikilia nafasi ya pili kwa ubora wa mchezo miongoni mwa wachezaji wa kiume duniani
MCHEZA tenisi wa Hispania, Rafael Nadal, amemshinda mchezaji bora zaidi duniani wa kiume, Novak Djokovic katika mashindano ya Italia Open, na kupata ubingwa wake wa sita katika mashindano hayo ya Italia.
Nadal alipata ushindi wa 7-5 6-3 katika fainali hiyo ambayo ilichezwa Jumatatu baada ya kuahirishwa siku ya Jumapili kutokana na mvua kunyesha mno mjini Roma.
Ushindi huo umemweka Nadal katika nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji bora zaidi katika mashindano ya wanaume duniani.
Kabla ya mashindano ya Jumatatu, Djokovic, raia wa Serbia, amekuwa akimshinda Nadal mfululizo katika mashindano saba yaliyopita, kabla ya kuanza kuibuka tena kama mshindi katika fainali ya Monte Carlo Masters mwezi uliopita.
Sasa Nadal amemshinda katika fainali mbili za mwisho walizokutana.
Nadal alisema: "Mawazo ya ushindi yalinijia wakati muwafaka, kwani kumshinda Novak, unahitaji kuwa katika hali yako bora zaidi ya uchezaji, kwani yeye hukusukuma hadi mjwisho katika pambano lote.
"Nadhani kiakili nilikuwa katika hali thabiti kila wakati muhimu nilipohitajika kuwa hivyo."

RASHID YEKINI ALIYEKUFA NA DONGE NA MOYONI



MEI 4, mwaka huu wapenzi wa soka Nigeria na Afrika kwa ujumla walipokea habari za kusikitisha, kuhusu kifo cha mshambuliaji mahiri zamani barani, Rashidi Yekini.
Rashidi Yekini alikuwa mshambuliaji hatari kabisa kuwahi kutokea nchini Nigeria tangu kugunduliwa kwa mchezo wa soka. Alipewa jina la utani la ‘Ye-King’ kutokana na ufumaniaji wake wa nyavu.
Alikulia mjini Kaduna ambaklo alikuwa ni gumzo kwa mashabiki wa soka kabla ya kujulikana nchi nzima.
Mwaka 1994, Yekini aliiongoza Super Eagles kutwaa taji la Mataifa ya Afrika huko Tunisia na kuwa mfungaji bora. Alikuwa tishio kwa mabeki na makipa wa upinzani waliokuwa wakishindwa kumdhibiti, kutokana na umbo lake kubwa na mashuti makali.
Baada ya mashindano ya Tunisia mwaka 1994, dunia nzima ilikuwa na furaha ya kikaribisha timu bora ya Afrika kwenye fainali zake za mara ya kwanza za Kombe la Dunia zilizofanyika Marekani. Mechi ya kwanza ya Nigeria ilikuwa dhidi ya Bulgaria kwenye Uwanja wa Cotton Bowl huko Dallas.
Mbele ya mashabiki zaidi ya 40,000, Super Eagles ilifunga bao la kwanza dakika ya 21 kutokana na shambulizi kali lililotengenezwa na Yekini ambaye wakati huo alikuwa akichezea Victoria Setubal ya Ureno.
Lilikuwa bao zuri lililotokana na uchezaji wa uhakika kutoka winga ya kulia alikokuwapo winga wa Ajax Amsterdam ya Uholanzi - Finidi George.
Nyota huyo, Finidi, aliichanganya beki ya Bulgaria na kupiga krosi bomba iliyomkuta Yekini akiwa kwenye kasi ndani ya mita sita kutoka langonmi mwa Bulgaria. Hakufanya makosa na kuandika bao la kwanza la Nigeria kwenye historia ya Kombe la Dunia.
Uwanja mzima ulilipuka kwa shangwe na nusura Yekini azichane nyavu za Bulgaria kwa furaha kubwa iliyoonekana wazi mwili mzima.
Aina yake ya ushangiliaji iliingia kwenye vitabu vya kumbukumbu. Mechi hiyo ilimalizika kwa Nigeria kushinda 3-0 na kuizamisha kabisa timu iliyokuwa ikiongozwa na Hristo Stoichkov. Ni mechi iliyoshuhudia ubora wa soka la Afrika duniani.
Baada ya kustaafu soka la kimataifa, Yekini alishangaza watu aliporejea kwenye Ligi Kuu ya Nigeria, na kung’ara akiwa na Julius Berger ya Lagos msimju wa 2005-2006. Alifunga mabao kadhaa kabla hajatangazaa kustaafu kikweli kweli na kumuachia umaarufu mkubwa.
Akiwa na Super Eagles alifunga mabao 37 na alijinyakulia heshima duniani alipopewa tuzo ya uanasoka bora wa mwaka wa Afrika na CAF mwaka 1993.
Wakali wengine wa enzi zake kama Daniel Amokachi, Samson Siasia, Augustine Eguavoen, Mike Emenalo, Sunday Oliseh na Ben Iroha ama wameifundisha timu ya taifa au kuajiriwa na Nigeria Football Federation ( NFF) au klabu za Ulaya, ni tofauti kabisa kwa Rashidi Yekini alikuwa ‘kimya’ alijiweka mbali na umaarufu baada ya soka, akibaki kuwa mchamungu tu
Hakuna aliyekuwa akifahamu nyendo zake, ingawa ni wazi walijua alikuwa anaishi Ibadan. Aligoma kuzungumza na waandishi wa habari wanaomwinda mara kwa mara kwa ajili ya mahojiano. Mwandishi aliyejaribu kupanga mahojiano kwa msaada wa mchezaji mwenzake na Yekini nyumbani kwake, alishangaa pale mpachika mabao huyo alipogoma kufungua mlango!
Pia Yekini alimuonya rafiki yake aache mara moja kuwapeleka waandishi wa habari nyumbani kwake. Ni kwa nini Yekini, aliyefunga bao la kwanza la Nigeria kwenye Kombe la Dunia aliamua kujitenga na jamii?
Aligomea ombi la NFF la kuipeleka pasi yake ya kusafiria ili atengenezewe visa ya kwenda Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka juzi. Mabosi hao wa soka walikuwa wamemteua Yekini kuwa Balozi kwenye Kombe la Dunia 2010 pamoja na kocha wa zamani wa timu ya taifa, Christian Chukwu, wachezaji wa zamani wa Eagles, Garba Lawal, Amodu Shuaibu na Tijani Yusuf.
Tangu atundike buti mwaka 2005 baada ya kuzichezea Julius Berger FC na Gateway FC ya Abeokuta, alikuwa anajali shughuli zake tu. Sababu kadhaa zilikuwa zikitolewa kuhusu chuki ya Yekini kwa jamii.
Kuna uvumi kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Eagles ana matatizo na wachezaji wenzake wa timu ya taifa. Kulikuwapo na taarifa zisizo rasmi kuwa kulikuwa na njama za kutompasia mipira nyota huyo wakati wa fainali za Marekani mwaka 1994.
Inasemekana kuna kundi la wachezaji walichukizwa na jinsi alivyoshangilia kwa nguvu baada ya kuifunga Bulgaria. Yekini hakufunga bao lingine kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994. Na kikundi hicho kiliendelea kumwangusha hata kwenye fainali za 1998 huko Ufaransa.
Huenda pia Yekini hakupenda kukutana na wabaya wake, ambao baadhi yao walikwenda Afrika Kusini.
Halafu kuna suala la Jenerali Sani Abacha. Baada ya kombe la mataifa kule Tunisia mwaka 1994, Yekini alikuwa ameweka kimiani mabao 13 na alikuwa na lengo la kuvunja rekodi ya mabao 14 ya Laurent Pokou wa Ivory Coast.
Ndoto hizo za kutimiza azma hiyo kwenye fainali za Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini mwaka 1996 zilichanwa na uamuzi wa Abacha kuizuia Eagles kushiriki mashindano hayo baada ya kuhitilafiana na Nelson Mandela. Nigeria ilifungiwa kushiriki fainali za Burkina Faso mwaka 1998.
Mwaka 2000, wakati Nigeria na Ghana zilipoandaa mashindano hayo, enzi za Yekini zilikuwa zimepita. Samuel Eto Fils wa Cameroun akaivunja rekodi aliyokuwa akiitamani Yekini.
Insemekana kuwa hadi anafikwa na umauti, Yekini alikuwa akiumizwa sana na jambo hilo na alikamua kuuguza majeraha hayo kwa kuwa peke yake. Wachambuzi wengine wa soka wanasema uduni wa elimu aliokuwa nayo Yekini ulimzuia kujichanganya na wenzake wenye elimu zaidi yake.
Kabla ya kifo chake, alikuwa anaendesha hoteli iitwayo Liberty Motel, Barabara ya Ring, Ibadan, jimbo la Oyo, japo hakupenda kujichanganya na watu. Inasemekana hata marafiki zake ni wachache sana kwenye jiji hilo la zamani.
Naam, huyo ndiye Rashid Yekini, nguli wa soka aliyeiaga dunia kipweke licha ya umaarufu mkubwa na heshima aliyojijengea- zaidi kutokana na chuki aliyokuwa nayo dhidi ya wabaya wake, ambayo inadaiwa ilichangia kifo chake. Mungu aiweke pema poponi roho ya marehemu. Amin.

WASIFU WAKE:
JINA: Rashidi Yekini
KUZALIWA: Oktoba 23, 1963 (Miaka 47)
KUFARIKI DUNIA: Mei 4, 2012
ALIPOFIA: Ibadan
KLABU ALIZOCHEZEA:
Mwaka Klabu
1981–1982 UNTL Kaduna
1982–1984 Shooting Stars
1984–1987 Abiola Babes
1987–1990 Africa Sports
1990–1994 Vitória Setúbal
1994–1995 Olympiacos
1995–1996 Sporting Gijón
1997 Vitória Setúbal
1997–1998 FC Zürich
1998–1999 Bizerte
1999 Al-Shabab
1999–2002 Africa Sports
2002–2003 Julius Berger
2005 Gateway
(Tangu 1986 hadi 1998, aliichezea Nigeria mechi 70, akaifungia mabao 37)

ABIDAL ATOKA HOSPITALI


Eric Abidal - Barcelona
Eric Abidal - Barcelona
BEKI wa Barcelona, Eric Abidal ameruhusiwa kutoka hospitali na ataendelea kujisikilizia hali yake nyumbani baada ya kufanyiwa upasuaji mapema mwaka huu.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 32, alifanyiwa upasuaji wa ini katika hospitali ya Barcaclinic, Aprili 10 ikiwa ni kiasi cha mwaka mmoja kuondolewa uvimbe.
Abidal sasa amepwa ruhusa kurejea nyumbani, ambako ataendelea kupata ahueni akiwa karibu na familia yake.
Hizi ni habari njema kwa The Blaugrana wakielekea kwenye Fainali ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey dhidi ya Athletic Bilbao, Mei 25, mwaka huu ambayo itakuwa ni mechi ya mwisho kwa kocha Pep Guardiola kufanya kazi katika klabu hiyo.
Abidal, aliyejiunga na Barca akitokea Olympique Lyonnais mwaka 2007, ameichezea timu hiyo mechi 38 kwenye mashindano yote msimu huu wa 2011-2012, kabla ya kufanyiwa upasuaji huo

SIMBA YAMUONGEZA MKATABA PROFESA MILOVAN


Mwenyekiti wa Simba, ALhaj Ismail Aden Rage kulia akitiliana saini Mkataba na Profesa Milovan Novemba mwaka jana aliporejea Simba. Milo ameongeza mkataba wa miaka miwili, ambao utamuweka Msimbazi hadi 2014.

KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imemuongezea mkataba wa miaka miwili kocha wake Mserbia, Profesa Milovan Cirkovic baada ya kuridhishwa na kazi yake kwa kipindi cha nusu msimu alichokuwa na timu hiyo tangu arithi mikoba ya Mganda, Moses Basena.
Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia BIN ZUBEIRY jioni kwamba Milovan atakuwa kocha wa Simba kwa miaka miwili zaidi tangu sasa baada ya kuongezewa mkataba.
“Kipimo cha mafanikio ya kocha ni mataji na soka safi, kitu ambacho sisi kama viongozi tumekishuhudia Simba chini ya Profesa Milovan, sasa hatuoni kwa nini tusimuongeze mkataba,”alisema Kaburu.
Pamoja na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara kwa kishindo, Milovan aliiwezesha Simba kufika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako ilitolewa kwa penalti 9-8 na Al Ahly Shandy ya Sudan, baada ya sare ya jumla ya 3-3.

TFF YAWAKANA AL SHAABAB, WASEMA WAO NI NCHUNGA TU



 

NAWAKUMBUSHA TU AL SHABAAB 700, NCHUNGA ALISHINDA KWA KURA 1,437


ETI wanachama 700 wa Yanga walikutana Jumapili makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kufikia uamuzi wa kumng’oa madarakani Mwenyekiti, Wakili Lloyd Bahargu Nchunga.
Mapinduzi haya yaliongozwa na Mzee Ibrahim Akilimali, ambaye kihistoria nilishasema siku nyingi ni mzee kinara wa migogoro na mvuruga amani klabuni.
Kweli, Nchunga ameshindwa kuongoza Yanga na sababu kubwa ni uelewa wake mdogo katika masuala ya michezo na kukosa ushirikiano kutoka kwa Wajumbe wenzake wa Kamati ya Utendaji na wadau wengine wa klabu, wakiwemo hao wanaojiita wazee.
Lakini ukirejea uchaguzi uliomuweka madarakani Nchunga Jumapili ya Mei 18, mwaka 2010, alishinda Uenyekiti baada ya kupata kura 1,437, akiwaangusha wapinzani wake wanne, Francis Kifukwe aliyepata kura 370, Mbaraka Igangula aliyepata kura 305, Abeid Falcon aliyepata kura 301 na Edgar Chibura aliyeambulia kura 65 katika kura 2,220 zilizopigwa, wakati kura 23 kati ya hizo ziliharibika.
Kura 370 za Kifukwe na 305 za Igangula kwa pamoja wakichanganya, bado hawawezi kufikia kura za Nchunga- ina maana alishinda kwa kishindo. Inakuwa rahisi kuhisi watu hawa 700 waliokutana Jumapili ni wale wale 700 waliomnyima kura Nchunga PTA Mei 18, 2010.
Sitaki kuzama ndani sana- kwa sababu nimeshapitisha sera ya kutoandika habari za migogoro- lakini kwa pamoja na wasomaji wangu napenda tujadili, kiongozi aliyeshinda kwa kura 1,437 anaweza kung’olewa madarakani na watu 700?
Tena watu ambao hakuna aliyewahakiki kama kweli ni 700 na hakuna aliyehakikisha kama kweli ni wanachama wa Yanga? Tujadili.
LLOYD NCHUNGA


MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI YA YANGA, RIDHIWAN KIKWETE AKITANGAZA MATOKEO MEI 19, 2010, KULIA NI MFADHILI WA KLABU HIYO, YUSUF MANJI


MAKAMU MWENYEKITI, DAVIS MOSHA AKITOA SHUKURANI KWA WANACHAMA


SARAH RAMADHAN ALIYESHINDA UJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI


ALLY MAYAI TEMBELE ALIYESHINDA UJUMBE


CHARLES MUGONDO ALIYESHINDA UJUMBE


THEOFRID RUTASHOBORWA (SASA MAREHEMU) ALIYESHINDA UJUMBE


SALIM RUPIA ALIYESHINDA UJUMBE


MZEE YUSSUF ALIYESHINDA UJUMBE


MOHAMMED BHINDA ALIYESHINDA UJUMBE

HASHEEM THABEET AKIONYESHA MITINDO YA MAVAZI DAR JANA


Mchezaji wa mpira wa Kikapu, Hasheem Thabeet, akipita jukwaani na vazi la asili kwa mikogo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diambond Jubilee, jana Mei 20, 2012
MBunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, akipita jukwaani na vazi la Harusi kwa mikogo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diambond Jubilee, jana Mei 20, 2012


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi ya ua mmoja wa wanachama wa Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation’, Joha Simba, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi hiyo, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diambond Jubilee, jana Me i 20, 2012
Mke wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mama Margareth Samue Sitta, akipita jukwaani na vazi la asili kwa mikogo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya kusherehekea kutimiza miaka miwili ya Taasisi ya Tushikamane Pamoja Foundation, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diambond Jubilee, jana Mei 20, 2012.(picha zote na Amour Nassor)



SOURCE: DINA ISMAIL (http/mamapipiro.blogspot.com)
 

ROBIN GIBB WA BEE GEES AFARIKI DUNIA





Robin Gibb has died aged 62
Robin Gibb amefariki akiwa ana miaka 62
MWIMBAJI wa kundi la Bee Gees, Robin Gibb, amefariki dunia jana akiwa ana umri wa miaka 62.
Mwimbaji huyo ambaye ameuza nakala zaidi ya Milioni 200 na kutoa nyimbo kibao zilizotikisa akiwa na ndugu zake Maurice na Barry, alifanyiwa upasuaji na akakutwa na maradhi ya saratani.
Familia ya Robin Gibb wa kundi lililokuwa likiundwa na ndugu, Bee Gees imetangaza kwa machungu makubwa kifo cha Robin leo.
Robin Hugh Gibb alizaliwa Desemba 22, mwaka 1949 kabla ya kifo chake jana Mei 20, 2012 na alikuwa mweanamuziki maarufu Uingereza na mtunzi pia. Umaarufu wake ulitokana na kundi la Bee Gees, alilokuwa akipiga kazi na ndugu zake, pacha wake Maurice na kaka yake Barry. Mdogo wake mwingine, Andy Gibb, pia ni mwanamuziki maarufu wa kujitegemea.
Mara ya mwisho, Gibb alionekana jukwaani akitumbuiza Februari mwaka huu katika shoo ua hisanihuko London Palladium.
Hitmakers: Robin was part of one of the biggest groups of all time the Bee Gees with his brother Maurice, who passed away in 2003 and Barry who is now the only surviving member of the band
Robin na kundi lake Bee Gees na kaka zake Maurice, aliyefariki dunia mwaka 2003 na Barry ambaye sasa ni pekee aliyebaki.
Bee Gee Robin Gibb is seen arriving at a medical centre which specialises in cancer care on London's exclusive Harley Street
Gone but not forgotten: Robin leaves behind his wife Dwina
Comeback: Robin Gibb on stage with brothers Maurice (left) and Barry (right) at a Bee Gees concert in Sydney in 1999
Robin Gibb jukwani na ndugu zake Maurice (kushoto) na Barry (kulia) katika tamasha la Bee Gees mjini Sydney mwaka 1999
Honoured: In 2004 Robin was presented with a CBE with his brother Barry
Mwaka 2004 Robin na kaka yake, Barry
Back in the day: Robin as a young musician in 1970
1970
Robin Gibb in 1969
Robin Gibb of the Bee Gees at a party, March 23, 1978
Robin Gibb 1978
Robin Gibb in 1981
Robin 1991
Robin Gibb 1991
Robin 1981
1983: Robin Gibb with Dwina and their son Robin-John, known as RJ, with whom he went on to write the Titanic Requiem
1983: Robin Gibb na mkewe Dwina na mtoto wao wa kiume, Robin-John, anayefahamika kama RJ




TORRES AWATOLEA UVIVU CHELSEA


Fernando Torres

Anachotaka ni kujua moja tu, mustakabali wake inakuwaje?

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Fernando Torres atakuwa na mazungumzo na klabu hiyo baada ya kukosoa jinsi anavyofanyiwa katika klabu hiyo.
Mspanyola huyo alisema ni moja ya mambo makubwa yaliyomsononesha kuanzishiwa becnhi katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.
Torres alimuambia Mwandishi wa Kispanyola, Guillem Balague: "Nimekuwa na wakati mbaya sana katika msimu wangu huu.
"Nafikiri walikuwa wananichukulia katika namba ambayo sikuitarajia."
Mshambuliaji huyo wa Hispania, alisaini akitokea Liverpool kwa dau la pauni Milioni 50 Januari mwaka jana na amefunga mabao sita kwenye ligi katika ya 11 aliyofunga kwenye mashindano yote.
"Sijsikii vizuri. Ushindi kama huu dhidi ya Munich si kitu, lakini nataka waniambie itakuwaje katika mustakabali wangu.
"Sasa nafikiria kama soka ni mbaya, lakini nimepitia kipindi kigumu. Wananiharibia maisha. na sitaki kupitia huko tena."
Chelsea imepanga kuzungumza na mwakilishi wa Didier Drogba baadaye wiki hii kuangalia nafasi ya mchezaji huyo kubaki.
Klabu hiyo imekataa kumpa mkataba wa miaka miwili Drogba aliokuwa anautaka na iko tayari kumuongeza mwaka mmoja.

CHELSEA WAMTUPIA VIRAGO DROGBA, ABRAMOVICH ATAKA NDOO NNE ZAIDI ZA ULAYA


21 May 2012Last updated at 06:38 GMT

Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya

DROGBA ATEMWA CHELSEA, ANAKWENDA CHINA...

MKONGWE Didier Drogba mwenye umri wa miaka 34, ni kama tayari amekwishapiga mpira wake wa mwisho Chelsea, na klabu hiyo inatarajia atathibitisha uhamisho wa bure kwenda Shanghai Shenhua ya China.
KIUNGO wa Tottenham, Luka Modric mwenye umri wa miaka 26, anatarajia kuomba uhamisho baada ya klabu hiyo kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Didier Drogba
Didier Drogba
KOCHA wa West Ham, Sam Allardyce anataka kumrejesha kiungo wa zamani wa Hammer, Joe Cole mwenye umri wa miaka, 30, arejeshe cheche zake Upton Park baada ya klabu hiyo kurejea Ligi Kuu. Msimu uliopita Cole alikuwa akicheza kwa mkopo Lille ya Ufaransa, akitokea Liverpool.
NYOTA wa Blackpool, Matt Phillips mwenye umri wa miaka 21, bado anaweza kucheza Ligi Kuu msimu ujao, licha ya timu yake kushindwa kupanda, baada ya kunaswa na jicho la kocha wa Reading,Brian McDermott.

MANCINI MIAKA MITATU ZAIDI MAN CITY

KLABU ya Manchester City inatarajiwa kumzawadia mkataba wa miaka mitatu kocha wao Roberto Mancini utakaokuwa na thamani ya pauni Milioni 15.
WACHEZAJI wawili wa Tottenham, Louis Saha na Steven Pienaar wamekandiwa na mashabiki wa timu yao kwa kitendo chao cha kuwapongeza Chelsea kwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
KOCHA wa Ajax, Frank de Boer ndiye ni mtu namba moja kwa sasa katika orodha ya makocha wanaowaniwa Liverpool kuziba nafasi ya Kenny Dalglish aliyefukuzwa.
MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich anataka mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na a metoa hotuba kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya ushindi wa mikwaju ya penalti dhidi ya Bayern Munich.
Roberto Mancini set to be offered a new deal
Mancini
KOCHA wa Muda wa Chelsea, Roberto Di Matteo ghafla amegeuka lulu na klabu ya Aston Villa inamtaka baada ya kuwapa Chelsea taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
WACHEZAJI wamemtaka mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kumfanya Roberto Di Matteo awe kocha wao kamili, baada ya kuwaongoza vema kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
NYOTA wa Ivory Coast, Salomon Kalou anaamini Chelsea isingeweza kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kama Andre Villas-Boas angebaki kuwa kocha wa Stamford Bridge.
OBI MIKEL ALIMTILIA GUNDU ROBBEN
KIUNGO wa Chelsea, John Mikel Obi amesema alimuambia Arjen Robben atakosa penalti, wakati mchezaji huyo wa Bayern Munich akijiandaa kupiga mkwaju huo katika dakika za nyongeza.


TAIFA STARS MAZOEZINI LEO KARUME

Pondamali na makipa
Aggrey Morris
Meneja Leopold Mukebezi 'Taso''

Kocha wa makipa Juma Pondamali akiwanoa makipa wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars asubuhi ya leo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kocha Msaidizi, Sylvester Marsh akiwanoa wachezaji wa timu ya taifa, taifa Stars asubuhi ya leo, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Wachezaji wa Stars mazoezini




Sunday, May 20, 2012

MAELFU WAIPOKEA CHELSEA LONDON, HAKUNA PA KUKANYAGA


20 Mei, 2012 - Saa 16:07 GMT













MAELFU kwa maelfu ya mashabiki wanaimba na kushangilia kikosi cha Chelsea kilichoshinda Ligi ya mabingwa baada ya kurejea kutoka Munich kupitia mitaa ya London ya magharibi.
Timu ya Chelsea ikisafiri juu ya mabasi mawili yaliyo wazi, ilianza msafara wake kutoka uwanja wa Stamford Bridge majira ya adhuhuri hapa London.
Chelsea au maarufu kama The Blues' ilifanikiwa kushinda kombe la Ligi ya mabingwa kwa kuibwaga klabu iliyo shinda kombe le mshindi mara nne, Bayern Munich huko Ujerumani.
Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya London kushinda kombe la Ulaya.
Basi ambalo Timu ya Chelsea ilisafiria, limepambwa kwa rangi za klabu, na limekua likisimama kwenye kila hatua ambapo wachezaji wakiliinua Kombe kuwaonyesha mashabiki waengi ambao wamekua wakijitokeza kwa masaa mengi.
Mashabiki wamekua wakiwarushia wachezaji mawele kama ishara ya kuwaenzi -desturi iliyoanza mwishoni mwa miaka ya 1980, mashabiki walipoanzisha tabia ya kurusha figili angani, na kufuatiwa na nyimbo.
Baadaye klabu ya Chelsea ikapiga marufuku figili kutumiwa ndani ya uwanja wa Stamford Bridge.
Mwandishi wa BBC aliyeshuhudia sherehe hizo Ed Davey, amesema kua mashabiki walirusha vijiti vya figili wakati wakisubiri msafara, lakini walikua wachangamfu waliojaa nidhamu.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameronamesema si jambo la kawaida kuiona timu kutoka Uingereza ikishindana kupiga mashuti ya matuta dhidi ya klabu kutoka Ujerumani na Waingereza kushinda.
Nilishuhudia yote hayo nikiwa pamoja na Chancellor wa Ujerumani, ulikuwa wakati mgumu kusubiri kuona mshindi, lakini baadaye tulipongezana,alisema Waziri Mkuu

No comments: