Thursday, July 28, 2016

SERIKALI YAIAGIZA NEMC KUFANYA UKAGUZI KIWANDA CHA SBS MTWARA.



Naibu waziri wa Mazingira, Mhe. Luhanga Mpina (katikati) akiwa katika ziara ya kikazi katika kiwanda cha SBS Mtwara.


Naibu waziri wa Mazingira, Mhe. Luhanga Mpina, akisikiliza maelekezo kutoka kwa meneja uzalishaji wa kiwanda cha SBS Mtwara, Joseph Wandiba.


JUMA MOHAMED, MTWARA.

Serikali imeliagiza Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuhakikisha ndani ya mwezi wanafanya ukaguzi wa viwango vya moshi na maji katika kiwanda cha kuchakata taka zinazotokana na shughuli za uzalishaji wa mafuta na gesi cha Supply Base Solution (SBS) mkoani Mtwara, na kujiridhisha kuwa havina madhara kwa jamii.
Agizo hilo limetolewa mkoani Mtwara na naibu waziri wa Mazingira, Mhe. Luhanga Mpina, baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho na kuona namna ambavyo shughuli zinavyoendeshwa.
“NEMC wajiridhishe na vipimo vya moshi, wajiridhishe na vipimo vya maji wayapime na wajiridhishe kwamba yako salama katika viwango vinavyoruhusiwa..kwasababu maji yale ya kwenye tenki kama tuvyoyaona huwezi sana kuyazuia kutoroka..unaweza kupunguza lakini huwezi kuyazuia kabisa..” alisema.
Hatua hiyo ilitokana na katibu tawala wa mkoa wa M

Mmoja wa wafanya kazi wa kiwanda cha SBS Mtwara, akiendelea na majukumu yake.

twara, Alfred Luanda kudai kuwa kiwanda hicho kilishaamriwa kuhamishwa kutokana na kuwa katika eneo linalozungukwa na makazi ya watu, hali ambayo inaweza kusababisha athari za kimazingira.
Luanda alisema maelekzo ya kuwataka kuhama yalishatolewa mapema na aliyekuwa naibu waziri wa Mazingira katika serikali ya awamu ya Nne, Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kiwanda hicho pamoja na kusikiliza maoni ya wananchi.
“Kulikuwa na maelekezo kwamba hawa watu watafute eneo, wahamishe kiwanda..kiwanda ambacho tunakihitaji kwasababu shughuli za mafuta ndio zinaendelea mkoani Mtwara..” alisema Luanda.
Kwa upande wake, meneja uzalishaji wa kiwanda hicho, Joseph Wandiba alisema kuwa hajawahi kupokea agizo lolote la kuwataka kuondoka eneo hilo, na kudai kuwa atalifikisha kwa viongozi wa ngazi za juu kwasababu ndio amelisikia kwa mara ya kwanza.
Naibu waziri huyo anaendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani humo ambapo miongoni mwa maeneo atakayotembelea ni pamoja na kiwanda cha Saruji cha Dangote Industries Limited na kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba.




No comments: