Monday, July 25, 2016

Habari Picha-Uhaba wa maji wawatesa wananchi wilayani Kilwa.


Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nahama, halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wakichota maji yaliyotuwama kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kila siku. Maji hayo pia hayana usalama kwasababu hata wanyama waporini na mifugo huyatumia kwa kuyanywa.


Shida ya maji



Wananchi wa kijiji cha Nahama, wakiwa katika jengo la Zahanati ambalo wameshirikiana kujenga lakini ujenzi umesimama kutokana na kukosa uwezo wa kulimalizia ikiwa ni pamoja na kukosa vifaa vinavyohitaji fedha katika upatikanaji wake.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nahama, halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, wakimsubiri mwandishi wa Juma News kwa ajili ya kumweleza kero zao.


No comments: