Monday, July 25, 2016

Telela amwaga wino kukipiga Ndanda FC.


Kiungo Salum Telela akiweka dole gumba katika mkataba baina yake na klabu ya Ndanda FC ya Mtwara.



Na Juma Mohamed, Mtwara.

Katika harakati za kuimarisha kikosi chao kuelekea ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Klabu ya soka ya Ndanda Fc ya mkoani hapa, imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mkabaji Salum Telela kwa kuingia nae mkataba wa mwaka mmoja kuichezea timu hiyo.
Akizungumza na Juma News kwa njia ya simu kutoka jijini Dar es Salaam, afisa habari wa klabu hiyo, Idrissa Bandari, alisema makubaliano baina yao yamefikia baada ya kukamilika kwa mazungumzo ya takribani wiki mbili huku mchezaji huyo akizipiga chini ofa kutoka katika vilabu mbalimbali hapa nchini.
“Mwenye amesema kuwa watu watashtuka kuja katika klabu ya Ndanda lakini mwenyewe ana malengo yake na kuona kuwa ni moja ya klabu ambayo itampa mwelekeo mzuri..lakini amesema vipo vilabu vikubwa ambavyo vilimuhitaji lakini mwisho wa siku akaichagua Ndanda..” alisema.

Salum Telela

 
Telela ambaye msimu uliopita alikipiga na mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara klabu ya Yanga, lakini aliamua kuachana nao baada ya mkataba wake kumalizika.
Aidha, Bandari amesema timu hiyo tayari imeashaanza mazoezi katika kambi yake jijini Dar es Salaam huku ikiwa chini ya kocha wa timu ya vijana ya U-20, Shaweji Nawanda kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Simba utakaopigwa uwanja wa Taifa kabla ya kwenda kuwavaa Mtibwa Sugar huko Manungu mkoani Morogoro.
  

No comments: