Wednesday, October 19, 2016

Ndanda FC VS Mbeya City hakuna mbabe Nangwanda



Shija Nkina wa Ndanda FC akijaribu kumtoka mlinzi wa Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa Nangwanda Sijaona Mtwara. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1


Mshambuliaji wa Ndanda FC Shija Nkina akimiliki mpira mbele ya mlinzi wa Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa Nangwanda Sijaona Mtwara. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1

Wachezaji wa Ndanda wakitoka kushangilia goli lililofungwa na Riphati Kamis (15) kwa mkwaju wa penalty katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa Nangwanda Sijaona Mtwara. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1


Juma Mohamed, Juma News
 
Ndanda FC wameshindwa kutamba katika uwanja wao wa nyumbani Nangwanda Sijaona mbele ya wagonga nyundo Mbeya City baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo ulioamuliwa na mwamuzi Martin Saanya.
Ndanda walianza kuwafunga wapinzani wao katika dakika ya 43 kupitia kwa Riphat Hamisi kwa mkwaju wa Penalty baada ya Shija Nkina kuchezewamadhambi na kipa wa Mbeya City, kabla ya nahodha wa Mbeya City Ally Kenny kusawazisha bao katika dakika ya 89 kwa shuti kali.
 

Kikosi cha wachezaji wa Ndanda FC kilichoanza katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa Nangwanda Sijaona Mtwara. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1

Miongoni mwa wachezaji walioanza katika kikosi cha Mbeya City kilichocheza na Ndanda Fc Nangwanda Sijaona Mtwara katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa Nangwanda Sijaona Mtwara. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1

 

No comments: