Friday, September 9, 2016

Wanne wajeruhiwa katika ajali wakiwa katika msafara wa makamu wa Rais Mtwara.


Mmoja wa majeruhi waliojeruhiwa katika ajali ya gari lililoanguka likiwa katika msafara wa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-Samia Suluhu Hassan ukielekea wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.



Mmoja wa Majeruhi akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuumia katika ajali


Juma Mohamed, Mtwara.

Wasaidizi wanne wa ofisi ya makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda kupata ajali likiwa katika msafara kuelekea wilayani Tandahimba, mkoani Mtwara.
 Akithibitisha kutokea kwa ajili hiyo iliyohusisha gari lenye namba za usajili ST. 244A, kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Thobias Sedoyeka, alisema ajali hiyo imetokea majira ya saa Nne na nusu asubuhi ambapo majeruhi wote wamekimbizwa katika ospitali ya rufaa ya Ligula kwa taratibu za kiuchunguzi.
“Katika kijiji cha Malanje majira ya saa Nne na Nusu katika msafara wa makamu wa Rais kuelekea wilayani Tandahimba kulitokea ajali, gari ST 244 A hata hivyo gari limeharibika na majeruhi tumewapeleka hospitali ya serikali kwa ajili ya taratibu nyingine za kiuchunguzi..” alisema kamanda.
Mganga mkuu wa mkoa wa Mtwara, Dkt. Wedson Sichawe, alisema katika majeruhi hao hakuna aliyeumia vibaya sana isipokuwa dereva wa gari hilo ambaye hakumtaja jina kuwa alikuwa akilalamika maumivu ya shingo.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, aliwaondoa hofu Watanzania na kusema kuwa waliopata ajali wote ni wazima huku msafara wa makamu wa Rais ukiendelea na ziara yake wilayani Tandahimba. 

Gari lililopata ajali katika msafara wa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-Samia Suluhu Hassan ukielekea wilayani Tandahimba mkoani Mtwara. Toyota Land Cruiser- ST 244 A



“Gari limepata madhara na ndugu zetu wameumia kidogo niwaondoe hofu ni wazima wote na tumewachukua tumewakimbiza hospitali yetu ya mkoa ya rufaa ya Ligula kwa ajili ya uwangaliazi zaidi..lakini ni jambo ambalo ni bahati mbaya kwakweli lakini msafara wote ukiacha hao waliopata ajali uko salama na tunaendelea na ziara kama
Mkamu wa Rais leo ametembelea kiwanda cha kubangua korosho cha AMAMA Farms Ltd katika mwendelezo wa ziara yake mkoani humo pamoja na kuzungumza na wakazi wa wilaya ya Tandahimba.

No comments: