Friday, September 16, 2016

Waandishi wa habari Mtwara kuungana na wadau wao kufanya usafi Hospitali ya Ligula.



Mwandishi wa habari ya Juma News, Juma Mohamed, akiwa na wadau wa maendeleo wilayani Masasi katika shughuli za usafi wa mazingira.




Juma Mohamed, Mtwara

Waandishi wa habari mkoani Mtwara wanatarajiwa kuungana na wadau wao pamoja na viongozi wa mkoa kesho septemba 17 kuendesha zoezi la kufanya usafi katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo, Ligula.
Katibu mtendaji wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mtwara MTPC, Bryson Mshana, alisema lengo la zoezi hilo ambalo limepangwa kutekelezwa mwezi septemba ya kila mwaka ni kukutana na wanajamii ambao ni wadau wakubwa katika tasnia ya habari.
“lengo letu hasa ni kukutana na wanajamii ambao tunafanya nao kazi na kufanya nao shughuli mbalimbali na siku ya kesho tumeamua kufanya usafi katika hospitali yetu ya Ligula..kwa maana ya kufanya usafi, kutazama wagonjwa lakini pia kupanda miti..” alisema Mshana.
Frank Fue, nimiongoni mwa wanahabari watakaofanya usafi huo utakaoambatana na zoezi la upandaji miti kuanzia saa 2 mpaka saa 4 asubuhi, alieleza umuhimu wake na kutoa rai kwa jamii.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiwa katika moja ya shughuli za usafi katika wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Zoezi hilo litaongozwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego, atakaeambatana na mkuu wa wilaya hiyo Dokta Khatibu Kazungu, ambaye aliwataka wakazi wa mkoa wake kujitokeza kwa wingi katika kuwaunga mkono wanahabari.
“jambo hili hufanywa kila mwaka na ndugu zetu hawa wadau wa maendeleo,kwahiyo niwaombe wanamtwara wote kwa utamaduni wetu tuliouzoea tujitokeze, kwasababu wanalolifanya ni kwa ajili ya jamii yetu, najua tukiunga mkono kazi hii kubwa wanayoenda kuifanya kesho basi matokeo yake yatatugusa sisi sote.” Alisema Dendego
Zoezi la usafi kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Mtwara linafanyika kila ifikapo Jumamosi ya kwanza ya mwezi Septemba ya kila mwaka.



No comments: