Friday, July 8, 2016

WANANCHI KITERE WALALAMIKIA MRADI WA UMWAGILIAJI KWA KUSUSUA NA KUTOKAMILIKA KWA WAKATI.

Juma Mohamed, Mtwara.

Wananchi wa kata ya Kitere halmashauri ya wilaya ya Mtwara, wameelezea kukerwa na kusuasua na kutokamilika kwa mradi wa bwawa la umwagiliaji unaotekelezwa na mkandarasi, Malcon Investment Company Limited ambayo ndio amepewa tenda ya ujenzi huo.
Hatua hiyo imekuja baada ya timu ya wataalamu kutoka katika halmashauri hiyo kwenda katani humo kwa ajili ya kusikiliza maoni ya wananchi ambao wamelalamikia zaidi kutoshirikishwa na kutoridhishwa na ujenzi wa mradi huo.
Tazama video hapo chini…


 

Mradi huo ambao thamani yake ni sh. Bilioni 1.1 ulikuwa ukabidhiwe kutoka kwa mkandarasi mwezi Novemba mwaka jana, lakini ikashidikana kutokana na kuwa na dosari, ambapo mpaka kufikia Julai 15 mwaka huu mkandarasi anatakiwa kuanza ujenzi

No comments: