Thursday, July 7, 2016

Waisilam Mtwara wachangia damu baada ya swala ya Eid.




Mmoja wa waumin wa Kiisilam akichangia damu baada ya swala ya Eid


Akina mama, watoto na wasichana waliojitokeza katika swala ya Eid jana katika viwanja vya shule ya Kiisilam ya Amana.



Waumin wakitekeleza ibada ya swala ya Eid


Swala ya Eid



Juma Mohamed, Mtwara.

Waumin wa dini ya kiislamu mkoani Mtwara wamehamasika na kushiriki katika kutoa sadaka ya sikukuu ya Eid El- Fitr kwa kuchangia damu kwa hiyari katika zoezi lililoendeshwa na mpango wa Taifa wa damu salama kanda ya kusini mara baada ya kuswali swala ya Eid katika viwanja vya shule ya sekondari ya Amana Islamic.
Wakizungumza na Juma News, walisema kuchangia damu ni sehemu ya ibada muhimu kwa waumin wa kiislam kwasababu mahitaji ya damu ni makubwa, na husaidia kuokoa maisha ya watu, na kuwataka wananchi wengine kuona umuhimu wa kufanya hivyo.
Walisema suala la kutoa sadaka ya Eid linaweza kufanyika kwa njia nyingi ambazo Mungu huzikubali kama hauna uwezo wa kutoa pesa au chakula basi ni kheri kujitolea damu ambayo itasaidia kuokoa maisha ya Watanzania wengine wenye mahitaji ya damu.

Uchangiaji wa damu salama.



“Nimeamua kutolea sadaka damu yangu mimi, kwamaana hiyo sikuwa na uwezo wa kutoa sadaka ya Fitir, sikuwa na uwezo wa kuchangia Majanvi nikachangia damu salama..na naomba wanawake wenzangu tujihamasishe kuchangia damu tuwachangie wagonjwa, kuna wengine wagonjwa hawajiwezi..” alisema Niya Ahmad.
Naye, Said Hassan, aliwataka wananchi wengine kuacha kuwa na woga katika kutekeleza zoezi hilo na kwamba kuchagia damu ni moja ya ibada muhimu kwa Waisilam ambayo inaokoa uhai wa wengine walio katika Hospitali mbalimbali.

Afisa uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama kanda ya kusini, Maary Meshy, akieleza namna wanavyoendsha zoezi la uchangiaji damu baada ya swala ya Eid.



Kwa upande wake, afisa uhamasishaji wa benki ya damu kanda ya kusini, Marry Meshy, alibainisha kuwa sasa katika benki ya damu kuna upungufu mkubwa wa kutokana na watu walikuwa katika mfungo wa Ramadhan hivyo kushindwa kuchangia.
“Benki ya damu kwa sasa tuna upungufu na uhitaji mkubwa kutokana na tumetoka katika kipindi cha mfungo..na watu tunatambua kipindi cha mfungo kuna baadhi ya taratibu au vigezo hawakidhi na wanahisi labda wataharibu funga yao kwahiyo kipindi hicho upatikanaji wa damu unakuwa ni mdogo..kwa sasa hivi tumekuja katika sikukuu ya Eid hii kwakuwa tunatambua mchango wa ndugu zetu Waisilam huwa hawatuangushi miaka yote hua wanachangia damu ya kutosha..” alisema Meshy.

Damu salama



Jumla ya wakazi 115 walifanikiwa kuchangia damu hapo jana kupitia zoezi hilo ambalo liliendeshwa katika vituo viwili vya Shule ya msingi Magomeni ambako walifanikiwa kukusanya Units 35 za damu pamoja na shule ya Kiisilam ya Amana na kupata Units 80.
Awali akitoa mawaidha kwa waumin baada ya swala ya Eid, Ustaadh Idrissa Bakari, aliwahusia waisilam kushikamana na kuwa wamoja pamoja na kuachana na kuingia katika makundi ambayo yatawaondoa katika kumcha Mwenyezimungu.
Ustadh huyo amewataka waisilam kuacha kujiita majina ya Kitaasisi ambayo yanaweza kuwafanya wamsahahu Mungu na kufanya maasi.

Ustaadh Idrssa Bakar, akitoa mawaidha baada ya swala ya Eid el Fitir.





No comments: