Tuesday, May 29, 2012


SHAABAN NDITI ATUA COASTAL UNION, TIMU YAENDA ZIARANI UTURUKI


MABINGWA wa Ligi Kuu ya Bara mwaka 1988, Coastal Union ya Tanga wanatarajiwa kufanya ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Uturuki, Julai mwaka huu, huku habari zaidi zikisema wamemsajili kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Shaaban Mussa Nditi (pichani kushoto) aliyewahi kuwika Simba SC.
Msemaji wa Coastal Union, maarufu kama Wagosi wa Kaya, Edward ‘Edo’ Kumwembe ameiambia BIN ZUBEIRY jioni ya leo kwamba wapo kwenye mchakato wa ziara hiyo na utakapokamilika watatoa ratiba kamili.
Ingawa Edo, ambaye pia ni Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa soka katika gazeti la Mwanaspoti, hakusema ziara hiyo imefadhiliwa na nani, lakini habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Barabara ya 13, Tanga zimesema ni mchezaji wao wa zamani, Kassa Mussa.
Kiungo huyo hodari wa zamani wa Mkoa wa Tanga, aliyekuwemo kwenye kikosi kilichochukua ubingwa wa Bara 1988, kwa sasa anaishi Uturuki ambako inaelezwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kimaisha.
Tayari Coastal imekwishaanza mchakato wa kuunda kikosi ‘baab kubwa’ cha msimu ujao na habari zaidi zinasema wako mbioni kumsajili kiungo wa zamani wa Simba, Mkenya Jerry Santo wakati wachezaji wengine ambao viwango vyao vimeshuka kama Ben Mwalala, Mkenya pia na Ramadhan Wasso, Mrundi, wamekwishaonyeshwa mlango wa kutokea.
Coastal inatarajiwa kutengeneza ‘bonge la mshituko’ kwa wapenzi wa soka nchini katika usajili wao, kutokana na harakati zao za chini chini za usajili wanazofanya, ikiwemo kumsajili kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Mussa Nditi.
Wengine ambao tayari wamenasa kwenye rada za Coastal ni mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Nsa Job Mahenya ambaye msimu huu alichezea Villa Squad iliyoshuka daraja.

UKRAINE, CROATIA WATAJA VIKOSI VYA UBINGWA


Kocha wa Croatia, Slaven Bilić.

KIKOSI KAMILI CHA CROATIA:
MAKIPA: Stipe Pletikosa (FC Rostov), Ivan Kelava (GNK Dinamo Zagreb), Danijel Subašić (AS Monaco FC).
MABEKI: Jurica Buljat (Maccabi Haifa FC), Vedran Ćorluka (Tottenham Hotspur FC), Danijel Pranjić (FC Bayern München), Gordon Schildenfeld (Eintracht Frankfurt), Josip Šimunić (GNK Dinamo Zagreb), Darijo Srna (FC Shakhtar Donetsk), Ivan Strinić (FC Dnipro Dnipropetrovsk), Domagoj Vida (GNK Dinamo Zagreb).
VIUNGO: Milan Badelj (GNK Dinamo Zagreb), Tomislav Dujmović (FC Dinamo Moskva), Ivo Iličević (Hamburger SV), Niko Kranjčar (Tottenham Hotspur FC), Luka Modrić (Tottenham Hotspur FC), Ivan Perišić (Borussia Dortmund), Ivan Rakitić (Sevilla FC), Ognjen Vukojević (FC Dynamo Kyiv).
WASHAMBULIAJI: Eduardo (FC Shakhtar Donetsk), Nikica Jelavić (Everton FC), Mario Mandžukić (VfL Wolfsburg), Ivica Olić (VfL Wolfsburg).


Kocha wa Ukraine, Oleg Blokhin

KIKOSI KAMILI UKRAINE
MAKIPA: Oleksandr Goryainov (FC Metalist Kharkiv), Maxym Koval (FC Dynamo Kyiv), Andriy Pyatov (FC Shakhtar Donetsk).
MABEKI: Bohdan Butko (FC Illychivets Mariupil), Olexandr Kucher (FC Shakhtar Donetsk), Taras Mikhalik (FC Dynamo Kyiv), Yaroslav Rakitskiy (FC Shakhtar Donetsk), Yevhen Selin (FC Vorskla Poltava), Yevhen Khacheridi (FC Dynamo Kyiv), Vyacheslav Shevchuk (FC Shakhtar Donetsk).
VIUNGO: Olexandr Aliyev (FC Dynamo Kyiv), Denys Garmash (FC Dynamo Kyiv), Oleh Gusev (FC Dynamo Kyiv), Yevhen Konoplyanka (FC Dnipro Dnipropetrovsk), Serhiy Nazarenko (SC Tavriya Simferopol), Ruslan Rotan (FC Dnipro Dnipropetrovsk), Anatoliy Tymoshchuk (FC Bayern München), Andriy Yarmolenko (FC Dynamo Kyiv).
WASHAMBULIAJI: Andriy Voronin (FC Dinamo Moskva), Marko Dević (FC Metalist Kharkiv), Artem Milevskiy (FC Dynamo Kyiv), Yevhen Seleznyov (FC Shakhtar Donetsk), Andriy Shevchenko (FC Dynamo Kyiv)

MAAJABU YA MICHEZO, MESSI ALILIMWA KADI NYEKUNDU YA MOJA KWA MOJA 2005


Messi amewahi kupewa kadi nyekundu mwaka 2005

WAIJUA ASILI YA MCHEZO WA DARTS?
Inaelezwa kuwa mchezo huu ulianza katika nchi za Jumuiya ya Madola barani ulaya ambapo wanajeshi walikuwa na utaratibu wa kulenga miti kwa kutumia vishale kama sehemu ya mafunzo ya kulenga shabaha.
Kufuatia mazoezi hayo ndipo watu wengine wakaanza kuiga na kuanzisha mchezo wa Darts.
XX
HII NDIYO PENATI YA KWANZA KABISA
Penati ya kwanza kabisa kupigwa katika historia ya mchezo wa soka ilikuwa kwenye mechi kati ya Wolverhampton Wanderers dhidi ya Accrington.
Mechi hiyo ilichezwa kwenye uwanja wa Molineux siku ya Septemba 14 mwaka 1891.
Kwa mujibu wa historia hiyo mchezaji wa Wolves Billy Heath ndiye aliyeweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga penati mara baada ya kupewa mpira ili aweze kupiga.
XXX

MPIRA WA MEZA WAWEKA REKODI YA AJABU
Septemba 26 mwaka 2010 pale mjini Guangzhou katika uwanja wa Guangzhou mchezo wa mpira wa meza uliweka rekodi ya aina yake baada ya kuingiza watazamaji wengi zaidi kuliko kawaida.
Mara zote tumekuwa tukishuhudia mchezo wa soka, ngumi,tenis, kikapu ama netiboli ikiingiza mashabiki wengi zaidi uwanjani ikilingamnishwa na michezo midogo kama darts,skwashi, mpira wa meza pamoja na mingineyo.
Lakini hii ilikuwa ajabu kwenye mchezo wa mpira wa meza ambapo kwenye uwanja wa Guangzhou nchini China jumla ya watazamaji 1,197 waliingia kutazama mchezo huo.
Rekodi hiyo bado inaendelea kutamba na imefanya mechi hiyo kuwa kubwa kuliko zote duniani katika michezo yote iliyochezwa ya mpira wa meza.
XXX
MAAJABU YA MESSI KUONYESHWA KADI NYEKUNDU
MESSI kama tunavyofahamu ni kwamba mara nyingi amekuwa si mkorofi ndani ya dimba ikiwemo kupigana na wachezaji wenzake ama kucheza rafu za hatari.
Hii imefanya wapenzi wengi wa soka kuzua mjadala mkali wa mabishano ambapo wapo wanaosema kwamba MESSI amewahi kupata kadi nyekundu huku wengine wakisema kuwa hana kadi nyekundu tangu aanze soka lake.
Ukweli ni kwamba mchezaji LIONEL MESSI amewahi kuonyeshwa kadi nyekundu tena ya moja kwa moja.
Kadi hiyo nyekundu aliipata mwaka 2005 wakati akiwa anaichezea timu ya taifa ya Argentina ya vijana wenye umri chini ya miaka 20.
Akiwa anaichezea timu hiyo dhidi ya Hungary katika mechi ya kimataifa ya kirafiki, MESSI ambaye wakati huo alikuwa na miaka 18, alionyeshwa kadi nyekundu.
MESSI alionyeshwa kadi hiyo katika kipindi cha pili cha mchezo wakati akijaribu kumzuia kwa mkono beki wa Hungary aliyemvuta jezi kwa nyuma wakati akielekea katika lango la Hungary.
Katika tukio hilo MESSI ambaye alikuwa kwenye kasi ya kuelekea langoni mwa timu pinzani ghafla alijikuta akivutwa jezi na beki VILMOS VANEZAK na mara tu alipojaribu kupeleka mkono wake kwa nyuma kwa bahati mbaya ukampiga shingoni mwa beki huyo na kumuumiza, kitu ambacho kilipelekea mwamuzi kumpa kadi nyekundu.
Mechi hiyo ilimalizika kwa timu ya vijana ya Argentina kupigwa bao 2-1.
XXXX
WAMJUA ALIYECHEZA MECHI NYINGI ZAIDI ENGLAND?
Mchezaji huyo si mwingine bali ni golikipa mstaafu wa kimataifa wa Uingereza PETER SHILTON ambaye amecheza jumla ya mechi 1005 za ligi kuu ya Uingereza na kuweka rekodi ya kipekee.
Mbali na rekodi hiyo PETER SHILTON bado anaendelea kushikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee kuichezea timu ya taifa ya Unigereza mechi nyingi zaidi kushinda mwingine yoyote.
Ni kwamba hadi sasa SHILTON anatamba na rekodi ya kuichezea Uingereza jumla ya mechi 125 na kwa ujumla alistaafu soka mnamo mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 47.
Full name Peter Leslie Shilton
Date of birth(1949-09-18) 18 September 1949 (age 62)
Place of birth Leicester, England
Playing position Goalkeeper
XXXXX
By ARONE MPANDUKA(Radio Tumaini) kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya mtandao wa Intaneti.

MCHAKATO MISS WORLD WAANZA RASMI TANZANIA


Salha Israel, Miss Tanzania 2011
KAMPUNI ya Lino International Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, imewataka warembo wanaotaka kushindana katika shindano dogo la kumsaka mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Dunia (Miss World 2012) wameombwa kuendelea kuchukua fomu za kushindana katika kinyang’anyiro hicho na kuzirudisha kabla ya Juni 4.
Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba sema kuwa wanatarajia kufanya mchujo wa washiriki Juni 5 kwa ajili ya kubakiza warembo 10 kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika Agosti 18 kwenye ukumbi wa Dongsheng Fitness Center Stadium, mjini Ordos, Inner Mongolia, China.
Lundenga alisema kuwa zoezi hilo lilisimamishwa kutokana na zuio la Serikali na wakati huo, jumla ya warembo 12 walikuwa wamekwisha chukua fomu za kushiriki. Alisema kuwa muda wa kufanya mashindano hayo umekaribia na wanatarajia kuitangaza tarehe mpya hivi karibuni.
Alisema kuwa amefurahishwa na kasi ya kuchukua na kurejesha fomu, hata hivyo wanahitaji warembo wengi zaidi ili kuweza kupata wigo mpana kwa ajili ya kumsaka mrembo atakayewania taji la Dunia ambalo kwa sasa lina mikononi mwa mrembo kutoka Venezuela, Ivian Sarcos.
“Tunakaribia kufanya mashindano madogo hivi karibuni, hivyo ni wajibu wetu kuwakumbusha warembo wanaotaka kuwania taji hilo kufanya hivyo kabla ya Juni 4 ili kuweza kuingia katika zoezi la mchujo,” alisema Lundenga.
Alisema kuwa mpaka sasa jumla ya nchi 84 zimekwisha pata wawakilishi wao kwa ajili ya mashindano hayo. Nchi 32 pamoja na Tanzania bado hazija chagua wawakilishi wao katika mashindano hayo.
Fomu za kuomba kushiriki zinapatikana katika ofisi za Miss Tanzania za jijini na mawakala wote wa mashindano hayo katika mikoa ya Tanzania Bara.

ENGLAND YATAJA KIKOSI CHA MWISHO

Rooney kulia na Wellbeck kushoto

JINA KLABU
MAKIPA:
1. Joe Hart Manchester City
13. Robert Green West Ham
23. Jack Butland Birmingham City
MABEKI:
2. Glen Johnson Liverpool
3. Ashley Cole Chelsea
5. Gary Cahill Chelsea
6. John Terry Chelsea
12. Leighton Baines Everton
14. Phil Jones Manchester United
15. Joleon Lescott Manchester City
18. Phil Jagielka
Everton
VIUNGO:
4. Steven Gerrard Liverpool
7. Theo Walcott Arsenal
8. Frank Lampard
Chelsea
11. Ashley Young Manchester United
16. James Milner Manchester City
17. Scott Parker Tottenham
19. Stewart Downing Liverpool
20. Alex Oxlade-Chamberlain Arsenal
WASHAMBULIAJI:
9. Andy Carroll Liverpool
10. Wayne Rooney Manchester United
21. Jermain Defoe Tottenham
22. Danny Welbeck Manchester United

No comments: