Friday, July 8, 2016

MASHABIKI WA SOKA MTWARA WATOA MAONI TOFAUTI KUTOLEWA KWA UJERUMANI EURO 2016 UFARANSA.

 

Juma Mohamed, Mtwara.


Kufuatia timu ya soka ya Ujerumani kuondoshwa katika michuano ya Euro 2016 inayoendelea nchini Ufaransa katika hatua ya nusu fainali kwa kukubali kipigo cha magoli 2-0 kutoka kwa wenyeji Ufaransa, mashabiki wa soka mkoani Mtwara wamekuwa na maoni tofauti juu ya matokeo hayo.
Wakizungumza na Juma News, baadhi yao wamesema Ujerumani walistahili kupata kipigo hicho kutokana na ubora wa kikosi cha Ufaransa ulivyo huku wengine wakishangazwa na kuona kama ni matokeo ambayo hayakutarajiwa na wengi ukizingatia Mabingwa hao wa Dunia walifanikiwa kuiondoa timu ngumu ya Italia katika hatua ya robo fainali.
Angalia video hapo chini...





Fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kupigwa Julai 10 mwaka huu kwa kuwakutanisha wenyeji Ufaransa na Ureno ambao wamefanikiwa kuiondosha Wales katika hatua ya nusu fainali kwa ushindi sawa na Ufaransa wa mabao 2-0.

No comments: