Saturday, July 9, 2016

NDANDA FC WAKANUSHA UVUMI DHIDI YA KOCHA WAO KUTIMKIA RUVU.

Juma Mohamed, Mtwara.
 

Klabu ya soka ya Ndanda Fc ya mkoani Mtwara, imekanusha uvumi unaoenea juu ya kocha wao Malale Hamsini kuwa na mpango wa kujiunga na timu ya JKT Ruvu ya Pwani ambayo imemsajili aliyekuwa kinara wa mabao wa Ndanda msimu uliopita, Atupele Green.
Akizungumza na Juma News TV, afisa habari wa klabu hiyo Idrissa Bandari, amesema kocha huyo bado wana mkataba naye na kwamba kwa sasa yupo mapumzikoni nyumbani kwao Zanzibar, huku akitarajiwa katika siku za karibuni kuungana na kamati ya usajili iliyopo jijini Dar es Salaam kuendelea na usajili.
 

 


Kwa upande wake, Malale Hamsini akizungumza kwa simu kutoka Zanzibar, amesema taarifa hizo sio za kweli, na kwamba hao JKT Ruvu hawajawahi kumfuata na kumweleza chochote.
Aiidha, Bandari amesema suala la usajili linaendelea vizuri na tayari wameshawaongezea mikataba baadhi ya wachezaji wao wa zamani, ikiwa ni pamoja na mshambuliaji Omary Mponda na kiungo Salum Minelly, na kwamba wanatarajia kuanza kambi mapema wiki ijayo baada ya kukamilisha usajili.

No comments: