Sunday, June 29, 2014

PAUL G. NGALEMA..MASHINE MPYA YA NDANDA FC

Paul Ngalema katika moja ya mechi alizocheza akiwa na Simba Sc.

Ngalema, wakwanza kushoto

Ngalema, wapili kulia.

Moja ya mafanikio makubwa waliyoyapata Ndanda Fc katika usajili ni kumnasa mlinzi wa kushoto 'kisiki' Paul Ngalema, aliokuwa anakipiga Mtibwa Sugar ya Morogoro msimu uliopita.
Ngalema ambae kabla ya kujiunga na Mtibwa msimu uliopita akitokea Simba Sc ya Dar Es salaam, ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na ana uwezo wa kucheza katika nafasi zaidi ya moja uwanjani, pia ni mtu mwenye kasi na nguvu za miguu.

Amewahi kuvichezea vilabu vya Majimaji ya Songea na Ruvu Shooting Stars ya Pwani ambako alicheza kwa msimu mmoja na akaamua kujiunga na Wekundu wa Msimbazi.

Nimeanza kumfuatilia Ngalema tangia akiwa mwanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Lukuledi Wilayani Masasi, Mkoani Mtwara, wakati huo akicheza kama kiungo mkabaji katika timu ya Shule na hata timu ya kijiji pale ilipokua inamuhitaji wanapokuwa na mechi.

                                                      ........Itaendelea..................

No comments: