Na Princess
Asia
MJINI Magharibi imetinga hatua
ya 16 bora ya michuano ya Copa Coca-Cola baada ya leo (Julai 4 mwaka huu)
kuilaza Tanga bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Dar es Salaam.
Bao
la washindi katika mechi hiyo ya kundi B lilifungwa dakika ya 68 na Juma Ally.
Kwa matokeo hayo Mjini Magharibi ambayo imemaliza mechi zake imefikisha pointi
13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine katika kundi
hilo.
Mbeya imejipatia ushindi wa
pili mfululizo katika kundi lake la C baada ya leo kuifunga Mara bao 1-0 katika
mechi iliyochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam.
Mshambuliaji John Jerome alifunga bao hilo pekee dakika ya
43.
Licha ya ushindi huo Mbeya
wameshindwa kukata tiketi ya 16 bora kwani wamemaliza mechi zao wakiwa na pointi
sita tu. Timu za Dodoma yenye pointi 12 na Kinondoni ambayo imefikisha pointi 10
na mechi moja mkononi ndizo zilizofuzu kucheza 16 bora kutoka kundi
hilo.
Pwani imepata ushindi wake wa
kwanza katika kundi lake la D baada ya leo kuichapa Kagera mabao 3-1 katika
mchezo uliofanyika Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani. Mabao ya washindi yalifungwa
na Cotiveno Ngaga dakika ya 19, Abdallah Juma dakika ya 30 na Salum Ame dakika
ya 68.
Kagera ambayo imebakiza mechi
moja dhidi ya Shinyanga ikiwa na pointi sita ilipata bao dakika ya 42 kupitia
kwa Athuman Kassim. Nazo Ruvuma na Arusha zimetoka suluhu katika mechi ya kundi
A iliyochezwa Uwanja wa Tamco.
‘LULU’ YA SIMBA ‘TAKATAKA TU’ COASTAL UNION
Shiboli |
Na
Princess Asia
MSHAMBULIAJI aliyewahi kugombewa na klabu za Simba na
Yanga, kabla ya hajaangukia kwa Wekundu wa Msimbazi, mwaka juzi- Ahmad Ally
‘Shiboli’ ni miongoni mwa wachezaji 11 waliomaliza mikataba yao ya kuichezea
timu ya Coastal Union ya Tanga inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, na sasa
wako huru kujiunga na klabu yoyote.
Kwa mujibu
wa Coastal Union, wachezaji wengine ni Ben Mwalala, Samwel Temu, Francis
Busungu, Lawrence Mugia, Daudi Chengula, Godfrey Mmasa, Mwinyi Abdulrahman,
Sabri Ramadhan China, Soud Abdallah na Ramadhan Wasso.
Uhamisho wa
wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika Julai 30 mwaka
huu wakati kipindi cha kuanza wachezaji (kwa wasio wa Ligi Kuu) ni kati ya Juni
15 na 30 mwaka huu.
Kwa klabu za
Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni kuanzia Juni 15-30
mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10
mwaka huu.
STARS YAKWEA MATAWI YA JUU FIFA
PONGEZI KWAKO; Kocha mpya Taifa Stars, Kim Poulsen kazi ya mwezi uliopita imezaa matunda |
Na Prince
Akbar
TANZANIA imependa kwa nafasi
12 kwenye orodha ya viwango vya ubora ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA)
iliyotolewa leo (Julai 4 mwaka huu) na shirikisho hilo.
Kwa
viwango vya Juni mwaka huu, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ilikuwa namba 139 hivi sasa
imefika nafasi ya 127 ikiwa na pointi 253 kulinganisha na 214 za Juni mwaka
huu.
Ivory Coast inayoshika nafasi
ya 16 duniani bado inaongoza kwa upande wa Afrika ikiwa na pointi 939. Timu hiyo
ilikuwa katika nafasi hiyo hiyo kwa viwango vilivyotolewa Juni 6 mwaka huu.
Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya na Dunia ndiyo wanaoendelea kuongoza kwa
kukamata nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 1,691.
BREAKING NEWS: YANGA WAFUKUZWA ZANZIBAR
Na Prince
Akbar
CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA)
kimewafukuza Yanga katika mashindano ya Urafiki, kwa kitendo cha kupeleka kikosi
cha vijana (Yanga B) badala ya kikosi cha wakubwa kwenye michuano hiyo kama
walivyokubaliana.
Chanzo cha habari kutoka ndani
ya ZFA, kimeiambia BIN ZUBEIRY jioni hii, kwamba ZFA na Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar kwa ujumla wamekerwa na kitendo kilichofanywa na uongozi
wa Yanga na wamekichukulia kama ni dharau, kupeleka timu B badala ya timu
A.
“Mashindano haya kuendesha ni
gharama, jana Yanga wamecheza, watu wamekuja wanaona timu B, wametukana sana,
wamesema ni utapeli, dhahiri mechi ijayo watu hawatakuja uwanjani. Sasa
tutawahudhumia Yanga kwa gharama kubwa, wakati watu hawaendi uwanjani kuwaona
watoto wao wa B.
Kwa
sababu hiyo, ZFA baada ya kushauriana pia na baadhi ya viongozi wa serikali (ya
Mapinduzi), tumeamua kuwarudisha watoto wa Yanga Dar es Salaam, wameondoka na
boti ya saa 10:00 na watafika Dar es Salaam saa 12, kawapokeeni,”kilisema chanzo
chetu kutoka ZFA.
Chanzo hicho kilisema
mashindano hayo, yalikuwa yana lengo zuri tu la kuzipa matayarisho timu zote
zinazocheza michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama
Kombe la Kagame, inayoanza Julai 14, Dar es Salaam- ambazo ni Mafunzo kwa upande
wa Zanzibar na Simba, Azam na Yanga kwa upande wa Bara.
“Lakini ajabu Simba na Azam
wameleta timu zao za kwanza, ila wao Yanga wanaleta watoto, sasa hii ni dharau
kwetu kama ZFA na kinyume cha makubaliano yetu na wao. Ni dharau kwa falimia
yote ya wapenda soka wa Zanzibar, ni dharau kwa wapenzi wa Yanga wa
huku,”kilisema hicho.
Yanga pamoja na kupeleka timu
B, lakini jana kilicheza soka ya uhakika dhidi ya mabingwa wa zamani wa
Tanzania, Jamhuri ya Pemba na kufungwa kwa taabu mabao 3-2.
TBL YAKABIDHI 'MPUNGA' WA UCHAGUZI YANGA
Angetile akielezea jambo, kulia kwake ni Kaswahili |
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu katikati akiwa na 'vimwana' Dina Ismail kulia na Elizabeth Mayemba kushoto |
Mwesigwa akiondoka TBL na begi lake dogo likiwa na 'mahela', kulia ni Clara Alphonce wa Mwananchi |
Mkurugenzi wa Executive Solutions, Aggrey Marealle aliyekuwa mwongoza shughuli hiyo |
Oscar Shelukindo katikati akimuwakilisha George Kavishe. Kulia ni Kilindo na kushoto Mwesigwa |
Jaji Mkwawa akitafakri jambo |
Mwesigwa akizungumza |
Sehemu ya Waandishi walioalikwa |
Michael Momburi wa Mwanaspoti kulia, akiwa Dina Ismail wa Tanzania Daima |
Unaweza kuwaona magwiji hapo, Clara, Eliza, Grace Hoka na |Somoe Ng'itu na kwa mbele kulia ni jembe la Channel 10, Said Makalla |
Ofisa wa Executive Solutions, Ibrahim Kyaruzi kulia akiwa Ofisa wa TBL kwenye hafla hiyo |
No comments:
Post a Comment