Wednesday, July 13, 2016

SERIKALI MTWARA YAWATAKA WAWEKEZAJI KURUDISHA HUDUMA KWA JAMII ILI ZIWANUFAISHE.

JUMA MOHAMED, MTWARA.

Serikali mkoani Mtwara imezitaka kampuni mbalimbali za uwekezaji nchini kujenga utaratibu wa kurudisha huduma kwa jamii kwa lengo la kuwanufaisha wananchi ikiwa ni pamoja na kuboresha elimu na kutatua kero za upatikanaji wa maji.
Akizungumza mkoani humo katika sherehe ya kuadhimisha miaka 25 ya kuwapo kwa kampuni ya Chemicotex ambao ndio wazalishaji wa dawa ya meno ya Whitedent, katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Mtwara, Renatus Mongogwela, amesema kampuni hiyo iwe mfano wa kuigwa kutokana na kutoa zawadi ya magari kwa wananchi ambayo yanashindaniwa kwa kujaza fomu.
 
Naye, afisa mauzo wa kampuni hiyo kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam, Riyaz Dewj, amesema wameandaa shindano hilo kwa ajili ya kutoa shukrani kwa wananchi ambao hawatozwi gharama yoyote katika kushindania, huku baadhi ya wananchi hao wakihamasihana kushiriki kwa wingi ili mshindi apatikane kutoka Mtwara.

Tazama Video >>>

  
 
Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika katika mikoa yote nchini yamehitimishwa katika mkoa wa Mtwara.
 


No comments: