Sunday, July 10, 2016

MITAZAMO YA MASHABIKI MTWARA FAINALI YA EURO LEO.

Juma Mohamed, Mtwara.

Kuelekea katika mchezo wa fainali wa michuano ya Uefa Euro 2016 unaowakutanisha wenyeji Ufaransa na Ureno, unaotarajiwa kupigwa muda mfupi ujao katika uwanja wa Stade de France, mashabiki wa soka mkoani Mtwara wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya matokeo yanayotarajiwa katika fainali hiyo.
Wakizungumza na Juma News, baadhi ya mashabiki hao wameonesha Imani kubwa kwa kikosi cha Ureno, ambacho mpaka kina tinga fainali kimeshinda mchezo mmoja tu ndani ya dakika 90, huku wengine wakiamini kuwa wenyeji Ufaransa wataibuka wababe hii leo.
 




Hii ni fainali nyingine ambayo inawakutanisha nyota wawili wanaokipiga katika vilabu vya ligi kuu ya nchini Spain, vinavyotoka katika jiji la Madrid, Antoine Griezman wa Atletico Madrid na Christiano Ronaldo wa Real Madrid ambao walikutana katika fainali ya UEFA iliyopigwa nchini Itali mwezi mei mwaka huu, na Ronaldo kuibuka mbabe  kwa kuipa taji Real Madrid…sasa Je, leo ni Ronaldo tena au Griezman atajibu mapigo? Bila shaka dk 90/120/penalt zitaamua.

No comments: