Monday, May 16, 2016

Yanga Sc wamfuta machozi Minelly Taifa.>>> www.jumanews.blogspot.com



Wachezaji wa Ndanda Fc wakimfariji mwenzao Salum Minelly, ambaye alikuwa analia baada ya kukosa mabao mengi ya wazi katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya African Sports ya Tanga katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.


Salum Minelly, akimiliki mpira mbele ya Juma Jabu wa Kagera Sugar.



Na Juma Mohamed, Mtwara.


MCHEZO wa kukabidhiwa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mabingwa wapya Yanga Sc waliopambana na Ndanda Fc, umekuwa ni wa kumfuta machozi kiungo kinda wa Ndanda, Salum Minelly, ambaye aliifungia timu yake bao la kusawazisha katika dakika za majeruhi.
Minelly mwenye umri wa miaka 17 ambaye huu ni msimu wake wa pili kuichezea timu ya Ndanda katika ligi kuu, aliwahi kutoa machozi uwanjani Nangwanda Sijaona Mtwara katika mchezo wao dhidi ya African Sports baada ya kupoteza nafasi takribani sita za wazi.
“Nilikuwa nasononeka sana, nilishawahi hadi kulia ‘game’ na Kagera (African Sports) nilikosa magoli zaidi ya sita ile ‘one against one’ nakosa napoteza lakini sijakata tama nimshukuru Mungu leo nimefunga na tena nimeifunga timu kubwa..” alisema.
Mchezaji huyo ambaye ni kipenzi cha mashabiki wa Ndanda kutokana na namna anavyojituma uwanjani na kutokuwa na moyo wa kukata tama licha ya kuanzishwa kama mchezaji wa akiba mara kadhaa, msimu huu amekuwa na bahati ya kuanzishwa na pengine kumaliza dakika zote 90 chini ya mwalimu Malale Hamsini.

Kikosi cha Ndanda Fc.

Alisema, ukame wa mabao ambao alikuwa akikabiliana nao haukumkatisha tamaa bali ilikuwa ni chachu ya kuzidi kuongeza juhudi huku akiamini ipo siku atafunga goli, pamoja na kuwashukuru wachezaji wenzake na mwalimu wao kuweza kumpa moyo pale inapotokea anakosa nafasi nyingi za kufunga.
“Walikuwa wananiambia tu ongeza juhudi utafunga ipo siku utafunga, nashukuru Mungu nimefunga leo wamenipongeza wote wameniambia tulichokuwa tunakuambia leo kimetokea, nawashukuru wachezaji wengu wote kwa kunipa ‘support’ yao nashukuru..tuzidi tu kumwomba Mungu inshaallah kila kitu kitawezekana.” Aliongeza.
Alisema kitendo cha kufunga katika mechi dhidi ya Yanga ni kitendo cha kufurahisha na kinampa moyo wa kuzidi kufanya vizuri ikiwa ni goli lake la kwanza la msimu ingawa ligi imebakiza mchezo mmoja iweze kumalizika, na kudai kuwa anajipanga kwa msimu ujao.


2 comments:

Unknown said...

kila kitu ni mipango....viva ndanda

Juma Mohamed said...

Yah ni kweli bab..ila dogo anapambana kiukweli, pamoja na ufupi wake lakini anawatoa jasho wapinzani.