Friday, May 20, 2016

Wanafunzi sekondari ya Sabodo Mtwara wajisaidia maporini.



Mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mustafa Sabodo, Eva Sipryan, akielezea changamoto zinazowakabili shuleni hapo.




Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiongea na walimu katika shule ya sekondari ya Mustafa Sabodo.


Na Juma Mohamed, Mtwara.

WANAFUNZI wa shule ya sekondari ya Mustafa Sabodo iliyopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara, wako hatarini kupata magonjwa ya milipuko pamoja na kung’atwa na wadudu kutokana na kujisaidia maporini.
Wakizungumza shuleni hapo, wanafunzi hao walisema tatizo hilo ni la muda mrefu na kwamba linatokana na kukosekana kwa vyoo karibu na mabweni ambapo wanalazimika kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kwenda kujisaidia huku baadhi yao wakiamua kujisaidia katika mapori yaliyopo nyuma ya mabweni yao.
“Athari yakwanza kwamfano shuleni kwetu hapa kuna ugonjwa wa kuharisha, muda wa usiku tunapata shida kwasababu vyoo vipo mbali alafu kuharisha kule kunahitaji kujisaidia kwa haraka kwahiyo kutoka hapa mpaka kule inakuwa tunapata shida..” alisema Shadia Mohamed, mwanafunzi wa kidato cha Nne.
Naye, Eva Sipryan, mwanafunzi wa kidato cha Nne, alisema hali hiyo inawapa tabu sana na kupeleka baadhi yao kuoga nje ya mabweni yao nyakati za usiku kwa woga kutokana na umbali uliopo baina ya vyoo na mabweni.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiongea na walimu wa shule ya sekondari ya Mustafa Sabodo.



“Muda mwingine inatulazimu kwenda kuoga nje kule nyuma ya mabweni, kwahiyo kule vyooni ni mbali sana na mtu mwingine vyoo vipo mbali alafu unamkuta ugonjwa wa kuharisha kwahiyo muda ule tunajisaidia nyuma ya mabweni kwahiyo inatuathiri sana na inapelekea kuwaambukiza wengine..” alisema.
Aidha, alisema shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa maji jambo ambalo linapelekea wananfunzi kukosa kuoga mpaka muda wa siku Tatu hata mabweni kuwa katika hari ya uchafu.
Alisema, maji wanapatiwa kwa wiki mara moja ambapo hata hivyo hupatiwa ndoo Moja ambalo wanatakiwa watumie kwa shughuli zao zote ikiwamo usafi binafsi, kusafisha mabweni pamoja na usafi wa vyoo.
“Tunagaiwa ndoo moja tu kwahiyo kufua, kuoga ndoo hiyo hiyo kwahiyo mabweni yanakuwa machafu na tunatumia wiki nzima..Ndoo hiyo hiyo unafulia na hiyo hiyo inakusaidia katika kuoga, maana utakuta kama siku mbili tu ndio unaoga alafu siku nyingine zote unaingia darasani bila kuoga..” aliongeza Eva.
Mwalimu Mkomo Katani, ambaye husimamia masuala ya afya za wanafunzi shuleni hapo, aliiomba serikali kuushinikiza uongozi wa shule kuona umuhimu wa kujenga vyoo karibu na mabweni ili kuhepusha athari za kiusalama kwa wanafunzi pamoja na kupatwa na magonjwa ya milipuko.
“Lakini siku ambayo Yule motto akiumwa na Nyoka tutakuja kuambiwa walimu mulikuwa wapi, hali ya kuwa serikali au uongozi wa shule umeshindwa kutengeneza miundombinu mizuri wale watoto wakapa vyoo ambavyo itakuwa ni rahisi kwenda kujisaidia..bweni liko kule lakini vyoo vipo mita 100, sasa motto amebanwa usiku na mkojo au haja kubwa atashindwaje kwenda kichakani ambako ni karibu kuliko aende choo ambacho kiko mbali..” alihoji.

Mkuu wa mka wa Mtwara, Halima Dendego, akiwa katika ziara ya kikazi katika shule ya sekondari ya Mustafa Sabado halmashauri ya wilaya ya Mtwara, kwa ajili ya kukagua miradi ya elimu na kusikiliza maoni na changamoto za walimu. Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally.



Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, ambae alifika shuleni hapo kusikiliza kero mbalimbali pamoja na kupokea maoni ya walimu ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea sehemu mbalimbali mkoani hapa, aliutaka uongozi wa shule kushirikiana na jamii inayowazunguka kutatua changamoto hizo ambazo zipo ndani ya uwezo wao.
Alisema, sio kila jambo linatakiwa kuilalamikia serikali, mambo mengine yanatakiwa kumalizwa na wananchi wenyewe kwa manufaa yao huku yale makubwa ndio yanapaswa kufikishwa katika ngazi za juu kwa ajili ya msaada zaidi.
“Mtachekesha sana leo shule kubwa kama hii kuvuna maji tu mpaka mkuu wa mkoa aingilie kati..mimi nimekaa nina mwaka sasa, lini nimepata hodi ya mkuu wa shule kwamba mkuu mimi nina mradi huu nina ‘proposal’ naomba tutafutie fedha, mpaka leo nimekuja kama nisingekuja?..wewe mwenye tatizo umejipanga vipi kulimaliza?..maana katika mambo yote mliyosema ndugu zangu hakuna jambo kubwa hapa..” alisema Dendego.
Mkuu wa mkoa anafanya ziara ya kikazi katika halmashauri za Mtwara Mikindani, halmashauri ya Wilaya ya Mtwara pamoja na halmashauri ya mji wa Nanyamba kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi ambapo anatarajia kuhitimisha Mei 24 mwaka huu katika halmashauri ya Nanyamba.
………………………………………………mwisho……………………………………………….


No comments: