Manchester United wanategemea kumtangaza Jose Mourinho kuwa kocha wao
mkuu leo, tangazo rasmi la usajili wa kocha huyo linategemewa kutolewa
leo baada ya mchezo wa fainali ya FA Cup baina ya Manchester United vs
Crystal Palace.

Majadiliano
ya mkataba wa miaka 3 yalifanyika baina ya CEO wa United Ed Woodward na
wakala wa Mourinho, Jorge Mendes wiki kadhaa zilizopita; japokuwa
kumekuwepo na sintofahamu kubwa juu ya usajili wa Mourinho kwenye bodi
ya wakurugenzi wa Man United. Lakini baada ya majadiliano marefu maamuzi
yakafikiwa kwamba haijalishi na matokeo yatakayotokea leo pale Wembley,
utawala wa Van Gaal umefikia tamati.
Mourinho alisaini makubaliano ya kabla ya mkataba wa kazi rasmi,
ambao uliweka wazi kama kocha huyo hatopewa timu mwishoni mwa msimu basi
angelipwa mamilioni ya fedha na Man United.

Mourinho
huenda akawa analipwa kiasi cha cha €15 million kwa msimu mmoja akiwa
kocha Man Utd. Na pia Mourinho amepewa ahadi kupewa fungu la kubadili
kikosi. Huku akifahamu fika mpinzani wake Pep Guardiola ambaye anajiunga
na Man City nae amepewa fungu kubwa – na ikiwa hali itakuwa hivi basi
jiji la Manchester busy sana kwenye soko la usajili.
CHANZO: shaffihdauda.co.tz
No comments:
Post a Comment