Kocha wa Simba Mganda Jackson Mayanja ameanza vizuri kibarua chake baada ya kukiongoza kikosi cha ‘wekundu wa Msimbazi’ Simba kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mechi yake ya kwanza ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara akiwa kama kocha wa timu hiyo ambayo siku chache zilizopita imemfukuza aliyekuwa kocha wake mkuu Dylan Kerr.
Goli la Simba limefungwa na Amis Kiiza katika dakika ya tano kipindi cha kwanza bao ambalo limedumu hadi dakika ya 90 ya mchezo na kuishuhudia Simba ikiondoka uwanjani na pointi tatu mbele ya Mtibwa.
Baada ya kuondoka kwa Kerr Mayanja alipewa jukumu la kuinoa Simba akiwa kama kocha mkuu hadi hapo atakapopatikana kocha mkuu atakayechukua mikoba ya Kerr aliyetimuliwa baada kufungwa na Mtibwa Sugar kwenye michuano ya Mapinduzi Cup wiki iliyopita visiwani Zanzibar.
Mchezo huo ulikuwa ni kwanza kwa Mayanja na amefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya timu iliyowatoa kwenye Mapinduzi Cup wakati huo Mayanja alikuwa jukwaani akishuhudia mtanange huo. Ushindi wa leo wa kikosi cha Simba ni sawa na kulipa kisasi kwa wakatamiwa hao.
Mtibwa Sugar walicheza soka safi licha ya kupoteza mchezo huo lakinin watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi walizozipata kwenye mchezo huo.
Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa leo kwenye viwanja vingine ni kama ifuatavyo:
JKT Ruvu 1 – 5 Mgambo JKT
Toto Africans 0-1 Tanzania Prisons
Stand United 1-0 Kagera Sugar
Mbeya City 1-0 Mwadui FC
Coastal Union 1-1 Maji Maji FC
Azam 1-1 African Sports
SOURCE: shaffihdauda.co.tz
No comments:
Post a Comment