Na Juma
Mohamed, Mtwara.
MWAKILISHI
mkaazi wa kampuni ya Dangote nchini Tanzania, Esther Baruti, ameomba radhi
kwaniaba ya kampuni hiyo kufuatia taarifa zilizoandikwa kwenye vyombo vya
habari wiki moja iliyopita juu ya kubainika kwa raia wakigeni kiwandani hapo
wanaofanya kazi bila kuwa na vibali.
Akizngumza
na waandishi wa habari mkoani hapa mbele ya mkurugenzi wa sekta binafsi nchini
(TPSF), Godfrey Simbeye, alisema majukumu aliyonayo ni kuhakikisha kampuni hiyo
inatekeleza wajibu wake na kufuata taratibu zote za nchi ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha wafanyakazi wake wanakuwa na vibali.
![]() |
Rais Kikwete akitembezwa na Alhaj Dangote kujionea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha saruji cha Dangote Cement Obajan Plant (PICHA-MTANDAO) |
Alisema,
amekuwa kiungo wa kuunganisha kampuni hiyo na serikali ili kuhakikisha sheria
zinafuatwa na kwamba amekuwa akishirikiana vyema na waandishi wa habari wa
mkoani hapa kwa kipindi kirefu toka kilipoanza kiwanda hicho mpka kipindi hiki
kinapoelekea katika shughuli za uzalishaji ingawa kuna baadhi ya watu ambao wanachangia
kuibuka kwa changamoto kadhaa.
“Mimi toka
tumeanza kiwanda nimepata ushirikiano mkubwa na waandishi wa Mtwara, hapa
katikati tu kuna wengine wanakuja wanavuruga lakini bado mimi niko na
Wana-Mtwara..kwasababu sasa hivi tunatoka kwenye ‘project’ tunakwenda kwenye
‘operations’ ndio maana kunakuwa na watu mbalimbali wanaoingilia taratibu
wanafanya hivii, unajua kuna mtu mwingine anaweza akaja akakuambia usifanye
hivyo mimi namjua Fulani..sasa inafika mahali wewe mwenye jukumu la kushauri hiki
kiwe hivi unakuwa husikilizwi..” alisema.
Alisema,
vibali wameshaomba katika idara husika na hata huko nyuma walikuwa wanaomba
vibali kwa utaratibu ambao unafahamika baina yao na Idara ya Uhamiaji isipokuwa
hili ambalo lilitokea ni kutokana na meneja mkuu wa kiwanda hicho Vidya Sagar
Dixit kutotoa ushirikiano kwa maafisa wa Idara hiyo.
“Na mimi
kwaniaba ya Dangote na Watanzania wenzangu tunaomba msamaha kwa yote
yaliyotokea turuhusu wafanyakazi na serikali nayo ifanye kazi yake ili kiwanda
kiendelee tuendelee kupata mipango yote na serikali ambayo imejipanga ili
kumsaidia Dangote kwasababu wote, serikali na sekta binafsi tunashirikiana..”
aliongeza.
Alitoa wito
kwa serikali na watu binafsi kufanya kazi kulingana na mipaka yao na kutokuwa
na tabia ya kuingilia majukumu ya mtu mwingine, na kwamba kama sehemu kuna
tatizo basi mtu aelekezwe vizuri namna ya kutatua.
Godfrey Simbeye |
Kwa upande
wake, mkurugenzi wa sekta binafsi nchini, Godfrey Simbeye, alisema alipata
nafasi ya kukutana na meneja huyo na alieleza masikitiko yake juu ya kushikiliwa
na Idara hiyo huku akiamini kuwa serikali inalishughulikia suala hilo ili
shughuli za kiwandani hapo ziendelee kama kawaida.
Alisema,
kuhusu wafanyakazi raia wakigeni waliosimamishwa kuendelea na kazi kiwandani
hapo kutokana na kukosa vibali, bado wapo nchini na kwamba serikali
inalishughulikia suala lao ili kuhakikisha wale wanaokidhi vigezo vya kuendelea
kufanya kazi warudi kazini.
“Serikali
sasa hivi inachofanya inatathimini ili kuona kwamba wale ambao wanakidhi haja
ya kuwa na ‘permit’ ya kuishi Tanzania wanapewa ‘special pass’ ambayo
mwakilishi wa Dangote tayari ameshaambiwa alipie ada yake ili vitolewe vibali
kwa watu wote ambao wapo Dangote waendelee na kazi huku serikali ikijipanga
kutoa vibali vya muda mrefu..” alisema.
![]() |
Rais Kikwete akikata utepe katika sherehe za uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza Saruji cha Dangote eneo la Msijute mkoani Mtwara (PICHA-MTANDAO) |
No comments:
Post a Comment