Friday, June 17, 2016

Watumishi Wanne halmashauri ya Tandahimba kufikishwa mahakamani kwa ubadhirifu wa fedha





Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.

Wajumbe wa kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Tandahimba, wakiwa katika kikao cha baraza maalum la kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kwa mwaka wa fedha 2014/2015



Juma Mohamed, Mtwara.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego ameamrisha kukamatwa na kufikishwa mahakamani watumishi wanne wa idara ya manunuzi ya halmashauri ya wilaya ya Tandahimba kutokana na kukabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha wakati wa mchakato wa tenda ya kutafuta mkandarasi wa ujenzi wa barabara za halmashauri na kuisababishia halmashaurii hasara ya sh. Milioni 27.
Hatua hiyo imetokana na hoja ya kutaka kuchukuliwa hatua watumishi hao iliyowasilishwa na mweka hazina wa halmashauri hiyo Ally Machela, katika kikao maalum cha baraza la madiwani cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2014/2015, na kuungwa mkono na wajumbe wote.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, akiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Tandahimba. Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Tandahimba, Emmanuel Luhahula.



“Waheshimiwa madiwani naomba tusifanye kazi kwa woga, nyinyi ndio wenye halmashauri na nyinyi ndio mliopewa dhamana kwa niaba ya wananchi, mnapoongea na watendaji ni rafiki zenu pale wanapoenda vizuri, lakini pale wanapoipeleka halmashauri kinyume na taratibu naomba tusiweke pazia tuchukue hatua..hakuna hata mtendaji mmoja kati ya hao wakuu wa idara ambaye hajaenda shule..” alisema Dendego.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Namkulya Salum alisema watumishi hao ni pamoja na afisa manunuzi wa halmashauri Michal Ngajua, afisa mifugo Robert Mwanawima, “lakini pia kuna mtu mmoja anitwa Musa yuko TANROAD pale (Wakala wa Barabara) na mtu mmoja ambaye anaitwa Bakari, kwahiyo hao kwa ujumla wake ndio ambao wametakiwa wakamatwe na hatua za kisheria kama ambavyo mkaguzi ametutaka ziweze kuchukuliwa..” alisema 

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego



Aidha alisema miongoni mwa udanganyifu ambao umefanywa na watumishi hao ni kubadilisha mapendekezo yaliyotolewa na mkandarasi husika kampuni ya Accuracy Constructions Ltd ya kutaka alipwe sh. Milioni 110 ambaye ilibadilishwa na kuwekwa sh. Milioni 117.
“Tumepata hasara nyingine, kulikuwa na watu waliomba kwa bei ndogo ya Milioni 110 lakini tukawapa watu ambao waliomba kwa bei kubwa ya Milioni 127, maana yake halmashauri imepata hasara y a sh. Milioni 27 kwasababu mtu wa Milioni 110 tungempa angefanya kazi ile nah ii ni katika suala zima la barabara..” alisema.
Kwamujibu wa taarifa za mkuu wa wilaya hiyo, Emmanuel Luhahula ni kwamba tayari watuhumiwa watatu kati yao wameshakamatwa.

No comments: