Na Juma
Mohamed, Mtwara.
Rais Mstaafu
wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa, amewataka wazazi wa mikoa ya
Kusini kutoa msukumo kwa watoto wao waweze kujali umuhimu wa elimu, ili wanufaike
na uwekezaji unaoendelea katika mikoa hiyo unaotokana na rasilimali za gesi na
mafuta.
Akizungumza mkoani hapa katika Mahafali ya Nne ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella
Maris, Mtwara, alisema kumekuwa na msukumo mdogo sana kwa wazazi katika kusisitiza
umuhimu wa elimu kwa vijana wa mikoa hiyo, jambo amabalo linapelekea kuwa na
uhaba wa vijana wanaopta elimu ya juu katika vyuo vilivyopo
Alisema,
chuo cha Stella Maris kina uwezo wa kupokea wanafunzi 3,000 lakini wanafunzi
wanaojiunga hawafikii idadi hiyo, na kwamba hiyo ni changamoto kwa wazazi.
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin W. Mkapa |
“Nafahamu
kuwa zilikuwepo changamoto nyingi kwenye mikoa yetu ya Kusini. Lakini nyingi ya
hizi changamoto zimebaki ni historia..ni vema sasa tukajiandaa vema kitaaluma
ili tuweze kunufaika na uchumi wa gesi ambao unatujia kwenye kanda hii, bila
elimu bora tutabaki kuwa waangaliaji tu huku wengine wakija kunufaika na
rasilimali hizi hapa nyumbani kwetu..” alisema.
Alisema,
anasikitishwa na takwimu za matokeo ya mitihani kwa shule za sekondari za miaka
ya karibuni kwa mikoa ya Kusini na pwani, kutokana na shule kutofanya vizuri
kwenye mitihani yao na kuhathiri hata udahili wa wanafunzi katika taasisi
mbalimbalii ikiwa ni pamoja na Stella Maris.
“Nikiwa
mzaliwa wa Kusini, nimekuwa nikisikitishwa sana na hali ya elimu kwenye eneo
hili hususani uchache wa shule na taasisi nyingine za elimu kama hizi..juhudi
kadhaa zimefanywa na serikali za awamu zote katika kujaribu kutatua tatizo
hili, lakini sekta binafsi na wadau mbalimbali wa elimu kama Kanisa Katoliki
wametoa mchango mkubwa sana kwenye kusaidia kutatua tatizo la mgawanyiko sawia
wa taasisi za elimu kwenye kanda mbalimbali.” Aliongeza.
Wahitimu |
Awali, mkuu
wa chuo hicho, Slaus Mwisomba, aliwasihi wahitimu hao ambao jumla yao ni 514,
kwenda kutumia vizuri taaluma zao walizopata katika kipindi chote walichokuwa
chuoni hapo ili jamii iweze kunufaika nao na kwamba waachane na hanasa
mbalimbali ambazo zinaweza kuwachafua na kuwashushia hadhi yao kama wasomi wa
elimu ya juu.
Aidha,
alieleza changamoto ambazo chuo inakabiliana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa
maabara kwa ajili ya masomo ya Sayansi ambayo ni Phizikia, Kemia na Baiolojia.
“Stemmuco
inalengo la kuanzisha Maabala ya Sayansi hali inayoweza kwa chuo kutoa fursa ya
kudahili wanafunzi wa masomo ya Sayansi...hii itaongeza nguvukazi, itaongeza
utaalamu na mambo mengine kwa kujua hapa tulipo kuna rasilimali gani amabzo
zinahitaji sayansi kwa ajili ya kuendelezwa..” alisema.
Kwa upande
wao, baadhi ya wahitimu, walieleza kufurahishwa na hotuba ya Mhe. Mkapa hasa
aliposisitiza juu ya wao kwenda kukabiliana na hali ya kimaisha huko waendako
na kuto kata tama pale wanapoona wanakosa fursa za ajira na kwamba wajaribu
kutumia elimu zao kwa kutafuta namna ya kujiajiri ili waweze kufanikiwa, na
kusema kuwa wameipokea hotuba hiyo kama chachu ya wao kwenda kufanikiwa
kimaisha.
Gladness
Paul, ambaye amepata elimu ya biashara, alisema atatumia elimu hiyo kwa kufanya
shughuli mbalimbali za ujasiliamli ambazo anaamini jamii kwa kiasi kikubwa
itanufaika na elimu yake kupitia shughuli hizo.
No comments:
Post a Comment