Wednesday, June 27, 2012

VIDIC APONA, KUANZA MAZOEZI WIKI HII

 


Vidic
BEKI Nemanja Vidic ataanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wiki hii, kabla ya wachezaji wenzake wa Manchester United kurejea kazini, wameandika Man Utd kwenye tovutui yao. Beki huyo wa kati wa kimataifa wa Serbia, hajagusa mpira tangu goti katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Basel, Desemba, mwaka jana.


MASIKINI BERKO, AUMIA TENA


Yaw 'Poster' Berko

KIPA namba moja wa mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati wa Young Africans Sports Club (YANGA), Yaw Berko amepewa mapunziko ya siku tano kufuatia kuchanika katika paji la uso wakati wa harakati za kuokoa mpira katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na www.youngafricans.co.tz ,Daktari wa timu Juma Sufian amesema mchezaji huyo ameshonwa jumla ya nyuzi tano katika paji lake la uso hivyo atakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha siku tano kuanzia kesho akiwa katika mapunziko.
Berko aliumia wakati akiwa katika harakati za kuokoa krosi iliyochongwa na golikipa mwenzake na kuweza kujigonga katika mlingoti wa goli na kusababisha kuchanika na kuweza kupata matibabu ya haraka uwanjani hapo.
Mchezaji mwingine aliyeumia katika mazoezi hayo siku ya leo ni Hamis Kiiza Diego ambaye aliumia katika eneo la kidevu baada ya kombora lililoachiwa na mshambuliaji mpya Said Bahanuzi kutua karibu na kidevu chake na kusababisha mchezaji huyo kugaagaa hadi alipopatiwa matibabu na kuendelea na mazoezi hayo.
Mchezaji majeruhi ambaye hakuweza kufanya mazoezi hayo ni Nurdine Bakari aliyeumia mwanzoni mwa wiki hii.

YANGA NA EXPRESS YA UGANDA JUMAMOSI TAIFA


Yanga mazoezini ufukweni

MABINGWA wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Young Africans Sports Club,siku ya jumamosi wanatarajia kujipima nguvu na Mabingwa wa Uganda timu ya Express pambano litakalopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na tovuti ya klabu www.youngafricans.co.tz Mratibu wa pambano hilo Frank Pangani amesema mipango ya mchezo huo tayari imekamilika ikiwemo Mabingwa hao wa Uganda Express inayotarajiwa kuwasili kesho jijini Dar es salaam wakitokea jijini mwanza ambapo mwisho wa wiki iliyopita ilicheza mchezo wa kirafiki mjini Shinyanga.
Pangani amesema timu hiyo ya Express kutoka Uganda ambayo hivi karibuni ilicheza na Simba katika uwanja wa Kirumba inatarajiwa kuwa na msafara wa wachezaji na Viongozi jumla 26
Timu hiyo ya Express kutoka nchini Uganda inarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam siku ya Alhamisi tayari kwa mchezo huo wa Jumamosi ikiwa chini ya kiongozi wa msafara Mohamed Katerega ambaye pia ni meneja wa timu hyo na msemaji wa timu ndugu Isack Mumena.
Kwa upande wake Kocha msaidizi Fred Felix Minziro amesema kikosi chake kinaendelea vizuri na mazoezi hivyo pambano hilo pia litasaidia kikosi chake kujiweka sawa kabla ya michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Julai 14 Mwaka huu.
Minziro amesema anafurahishwa na mazoezi yanayoendelea hivi sasa kutokana na bidii zinazofanywa na wachezaji wake ikilinganishwa na Mwaka jana anaamini kuwa michuano ya Kagame na ligi Kuu ya Vodacom itakapoanza timu yake itafanya vizuri katika michuano hiyo.
Kocha huyo amesema tayari ameona dalili za kila mchezaji kucheza kwa juhudi ili kuhakikisha kuwa kila mchezaji anapata namba za kudumu katika kikosi chake.

MANJI AWEKEWA PINGAMIZI TFF ASIGOMBEE YANGA


Manji kulia, akiwa amechuchumamaa kujmsalimu Bi Rukia, mwanachama maarufu wa Yanga

Na Princess Asia
WAKATI kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) inatarajiwa kuketi Julai 2 kwa ajili ya kupitia pingamizi zilizowasilishwa kwa wagombea uongozi wa klabu ya Yanga, wagombea wawili Yusuf Manji na Stanley Yono Kevela wamewekewa pingamizi.
Kwa mujinu wa dinasimail.blogspot.com Klabu ya Yanga inatarajiwa kufanya uchaguzi mdogo julai 15 jijini Dar es Salaam ili kuziba nafasi za baadhi ya viongozi waliojiuzulu akiwemo mwenyekiti Lloyd Nchunga.
Mjumbe wa kamati hiyo iliyo chini ya mwenyekiti wake Deogratius Lyatto, Salum Mbwezeleni alisema kwamba kamati yake itapitia pingamizi hizo kwa kusikiliza wapingaji na waliopingwa na kisha kutoa maamuzi.
Hata hivyo, Mbwezeleni hakuweza kutoa ufafanuzi wa pingamizi wa wagombea hao Manji (Uenyekiti) na Kevela (Makamu Mwenyekiti, Ujumbe) kwa madai kuwa bado hajapitia maelezo yaliyowasilishwa na waliopinga.
“Ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa kamati itakutana Julai 2 na kuwasikiliza wahusika wote na kisha tutatoa maamuzi ili majina yaweze kutangazwa na wagombea waanze kampeni zao,”alisema.
Kamati ya uchaguzi ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Jaji Mstaafu John Mkwawa wiki iliyopita ilitawataja waliopitishwa katika ujumbe ni pamoja na Jumanne Mwamenywa,Edgar Fongo, Beda Tindwa, Ramadhan Said,Omary A. Ndula, Shaban Katwila,Ramadhan Y. Kampira,Lameck Nyambaya na Peter H. Haule.
Wengine ni Justine S. Baruti,Abdalah A. Mbaraka, Kevela,Mosess K. Valentino,Aaron Nyanda,George M. Manyama.Abdalah Sharia Ameir,Jamal Kisongo na Gaudiusus Ishengoma.
Huku wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Ayoub Nyenze, Kevela na Clement A. Sanga, wakati Jonh Paul Jambele, Manji, Edgar W. Chibula na Sarah Ramadhan wameomba katika nafasi ya uenyekiti,”alisema.
Uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika Julai 15 mwaka huu, umelenga kuziba nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne wa kamati ya Utendaji ambao walijiunzulu.

GARETH BALE AJITIA KITANZI MIAKA MINNE WHITE HART LANE


EPL, Gareth Bale, Tottenham Hotspur v Swansea City
Gareth Bale
KLABU ya Tottenham imetangaza kwamba Gareth Bale amesaini mkataba mpya wa miaka minne, ambao utamuweka White Hart Lane hadi 2016, wameandika Goal.com. Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Wales, kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na habari za kuhama klabu hiyo kwenda Manchester United na Barcelona ambazo ziliripotiwa kumtaka nyota huyo mwenye umri wa miaka 22.



SASA INAKUJA GREAT KILIMANJARO RUN GKR


Na Princess Asia
BAADA ya mafanikio makubwa ya kumleta mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz kushiriki mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilizotimua vumbi tarehe 24 Juni 2012 sasa klabu ya Mout Kilimanjaro Marathon 1991 imeanzisha mbio za “Great Kilimanjaro Run – GKR”
GKR zitafanyika mjini Moshi kila mwaka kuanzia tarehe 22 - 28 October 2012 zikishirikisha klabu zote za riadha kutoka mkoa wa Kili manjaro. GKR itazishikisha mbio fupi (Track and Field events) na kumalizia na marathon siku ya jumapili tarehe 28 October.
Akizungunzia uamuzi wa kushirikisha mbio fupi katika GKR Rais wa klabu ya Mt. Kilimanbjaro Marathon 1991 Onesmo Ngowi alisema kuwa klabu yake inataka kuziendeleza pia mbio fupi na michezo mingine ya uwanjani badala ya kuweka juhudi zote kwenye marathon tu.“Watu wamekazania sana marathon na kusahau mbio fupi ambazo zilishawahi kuliletea taifa hili sfa kubwa sana” alisema Ngowi kwa msisitizo.
Kuanzishwa kwa GKR kutaufanya mji wa Moshi kuwa na mbio tatu za marathon kwa sasa na hii inaufanya mji huu kutoa nafasi kubwa kwa wanariadha kukuza na kuendeleza vipaji vyao.
Tutamleta Haile Gabreselasie aje kuzindua mbio hizi” alisema Ngowi ambaye mwaka jana alikuwa na mazungumzo marefu jijini Addis Ababa na gwiji hili la mbio ndefu duniani kutoka nchi ya Ethiopia. Ngoiwi aliweza pia kutiliana mkataba na shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopia Airlines) jijini Addis Ababa kufadhili mbio za Mount Kilimanjaro Marathon. Kwa sasa Ethiopia Airlines (ET) ndio wafadhali pekee wa Mount Kilimanjaro Marathon. ET wanatoa punguzo kwa wakimbiaji wanaoshirtiki kwenye mbio hizi kutoka sehemu mbalimbai duniani.
Aidha, ET wanalipia gharama za kutangaza mbio hizi wakati wa New York Marathon, L.A Marathon na Boston Marathon. Hii inaitangaza sana Tanzania kwani mbio hizi tatu zinawashirikisha wakimbiaji wengi sana kutoka katika nchi nyingi duniani. Kwenye mbio hizi za Marakani Mt. Kilimanjaro Marathon huweka banda la maonyesho linaloitangaza Tanzania na vivutio vyake.
Pia Mt. Kilimanjaro Marathom huchezesha nahati nasibu (raffle) kwenye mbio hizi tatu za Marekani ili kuwapata washiriki maarufu kama Deidre Lorenz kuja kukimbia na kuitangaza vyema Tanzania.
Aliendelea kusema kuwa nchi hii ni yetu sote hivyo tuna jukumu la kuitangaza na kuiendeleza wote alisisitiza Ngowi ambaye mwaka 2000 ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilimpa tuzo ya “Mwanateknolojia wa Karne ya 20” kwa juhudi zake za kuendeleza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Ngowi anawaalika watu binafsi, makampuni na taasisi kushirikiana naye kuendeleza Utalii wa michezo hapa Tanzania ili kuipeleka nchi hii hatua moja mbele kwenye utandawazi. Kwa wale wanaotaka kuwasiliana naye kuhusu ufadhili watumie anwani ya barua pepe yangowio@yahoo.com au wapige simu namba 0754-360828.

FLY540 WAFAFANUA NA KUOMBA RADHI WATEJA WAO

Meneja mkuu wa shirika la ndege la Fly540 bw. Brown Francis kushoto akizungumza katika mkutano navyombo vya Habari jijini Dar es Salaam leo katika wakati akiomba radhi kwa wateja wake kutokana na tatizo lilitokea wiki iliyopita na kupelekea abiria wake kuchelewa katika safari yao, baada ya ndege waliyokuwa wasafiri nayo kupata hitilafu. Kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Bi .Jean Uku.

No comments: