Wednesday, November 23, 2016

Hofu ya ajali yawafanya wanawake Tandahimba kuingia katika biashara ya Bodaboda.


Msafara wa madereva Bodaboda wilayani Tandahimba ukiongozwa na askari wa usalama Barabarani kuelekea katika kituo cha polisi kwa ajili ya sherehe ya wahitimu wa mafunzo ya usalama barabarani.



Katibu tawala wa wilaya ya Tandahimba, Azizi Fakhii akimkabidhi zawadi ya shuka kamanda wa polisi wilaya ya Tandahimba, Fraterine Tesha iliyotolewa na madereva Bodaboda



Juma Mohamed, Juma News

Baadhi ya wanawake wanaoendesha pikipiki za abiria maarufu Bodaboda wilayani Tandahimba mkoani Mtwara wamesema wameamua kuingia katika biashara hiyo kutokana na hofu ya kupata ajali pindi wanapopakizwa na madereva wanaume kutokana na kuendesha kwa mwendo kasi.

Msafara wa madereva Bodaboda wilayani Tandahimba ukiongozwa na askari wa usalama Barabarani kuelekea katika kituo cha polisi kwa ajili ya sherehe ya wahitimu wa mafunzo ya usalama barabarani.



Wakizungumza wilayani humo badaa ya kuhitimu mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yaliyoendeshwa na chuo cha Apec, wanawake hao walisema hatua hiyo ni njia mojawapo ya kujiingizia kipato hali ambayo inawafanya kuacha kuwa tegemezi kwa waume zao.

Katibu tawala wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, Azizi Fakhii akifurahia zawadi ya shuka aliyopewa na mmoja wa madereva Bodaboda wilayani humo.



Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Mtwara, Meloe Buzema, alisema pikipiki zinachangia asilimia 28 ya ajali zote za barabarani huku katibu tawala wa wilaya ya Tandahimba Azizi Fakhii akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Sebastian Waryuba akawataka washiriki wa mafunzo hayo kuanzisha vikundi kwa ajili ya kujiunga na SACOS.
Jumla ya madereva bodaboda 410 wamehitimu mafunzo hayo na kutunukiwa vyeti huku wakiahidiwa kuondolewa vikwazo katika kuwapatia leseni.


No comments: