Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya

HULK ACHAGUA CHELSEA

MSHAMBULIAJIn wa Porto, Hulk, mwenye umri wa miaka 25, ameiambia Paris St-Germain angependa zaidi kujiunga na Chelsea, kwa dau la pauni Milioni 38 lililoripotiwa.
KLABU ya Liverpool ina nia ya kumsajili mshambuliaji Fabio Borini, mwenye umri wa miaka 21, ambaye amefunga mabao 10 katika mechi 26 alizoichezea Roma ya Italia, hiivyo kuingia kikosi cha Italia cha Euro 2012. Kocha wa Wekundu hao, Brendan Rodgers alipiga kazi na mpachika mabao huyo akiwa Chelsea na alimsajili kwa mkopo The Blues baada ya kutua Swansea.
Luka Modric
Luka Modric is a £30m target for Real Madrid
KLABU ya Real Madrid inajiandaa kuilipa Tottenham pauni Milioni 30 kwa ajili ya kumnasa Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, baada ya kocha Jose Mourinho kuitaka klabu yake iongeze dau.
KLABU ya Porto inaweza kujikuta inapoteza mchezaji mwingine, baada ya wakala wa mchezaji wao anayetakiwa na Manchester United kumlenga James Rodriguez, mwenye umri wa miaka 20, kusema mteja wake yupo katika mazingira magumu Porto.

OTHER GOSSIP

KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini anaamini Italia wanatakiwa kumtumia Mario Balotelli kama wanataka nafasi ya kuifunga England Jumapili.
KOCHA wa Everton, David Moyes ameunga mkono wa kuchanga fedha kwa ajili ya ujenzi mpya ambao watautumia kwa pamoja na wapinzani wao, Liverpool.
Joey Barton
Joey Barton set to learn his fate
MUSTAKABALI wa Joey Barton katika klabu ya Queens Park Rangers utaeleweka katika siku chache zijazo, baada ya klabu hiyo kukamilisha uchunguzi wake wa ndani juu ya kadi nyekundu aliyopewa katika mechi dhidi ya Manchester City ya kufunga msimuj uliopita wa Ligi Kuu