Tuesday, June 12, 2012

WAREMBO 12 wanaotarajia kuwania taji la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu


Na Mwandishi Wetu
WAREMBO 12 wanaotarajia kuwania taji la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' leo Jumatano wanatarajiwa kufanyiwa usaili kwa ajili ya kuanza safari ya kumpata mshindi wa shindano hilo litakalofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Navy Beach jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shindano hilo, kutoka kampuni ya K&L Media Solutions, Somoe Ng'itu, alisema jana kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na wanachosubiri ni siku ya shindano ifike.
Alisema kuwa kitongoji hicho kina warembo wenye sifa na wanaojiamini ambao wamepania kurudisha taji la Miss Tanzania kwenye Kanda ya Temeke.
Aliongeza kuwa ili kuboresha shindano hilo bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma na msanii na mchekeshaji mahiri hapa nchini, Mpoki watatumbuiza kwenye kinyang'anyiro hicho.
"Tunawaomba wadau wa sanaa ya urembo kufika kushuhudia mrembo wa Kigamboni atakavyopatikana, ni Kitongoji kilichoko sehemu pekee hapa nchini na kulikosa kushuhudia itakuwa ni kujinyima burudani wewe mwenyewe," alisema mratibu huyo.
Aliwataja warembo watakaochuana kuwa ni pamoja na Susanne Jeremiah, Agness Goodluck, Elizabeth Boniface, Dorothea Kessy, Esther Albert, Edda Silyvester, Sophia Martin, Doreen Kweka, Khadija Kombo, Linnah David, Rosemary Peter na Winnie Karaya.
Aliwashukuru wadhamini ambao wamejitokeza kusaidia shindano hilo ambao ni Redd's, Dodoma Wine, hoteli ya Hope Country, Screen Masters, Global Publishers, Nobro Collections, Times FM na Clouds FM.
Aliongeza kuwa warembo watakaoshika nafasi tatu za juu kutoka katika shindano hilo wataungana na wenzao kutoka vitongoji vya Kurasini na Chang'ombe ili kuwania taji la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.

Monday, June 11, 2012

CHEMSHA BONGO! TAJA WALAU MAJINA MATATU YA KIKOSI HIKI.

SHEVCHENKO AMFUNIKA IBRAHIMOVIC - UKRAINE WAKIIFUNGA SWEDEN NA KUONGOZA KUNDI D


Ukraine vs Sweden 2:1 FULL MATCH HIGHLIGHTS by Preoperumzn

MAN CITY WAAMUA MATOKEO YA MECHI KATI ENGLAND NA UFARANSA


France vs England 1:1 MATCH HIGHLIGHTS by Preoperumzn

EXCLUSIVE: SIMBA KWENYE MIKAKATI MIZITO YA KUMNYAKUA SHEDRACK NSAJIGWA

Siku chache baada ya mchezaji Shedrack Nsajigwa kumaliza mkataba wa kuichezea klabu ya Yanga huku akiripotiwa kuwepo nchini Kenya akifanya mazungumzo na klabu ya Gor Mahia, leo taarifa za uhakika kutoka kwenye kamati ya usajili ya Simba, zinasema viongozi wa mabingwa wa Tanzania wapo tayari kumsaini nahodha huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars.

Simba ambao leo hii wamepata pigo baada ya beki wao wa upande wa kulia Said Nassoro Chollo kuripotiwa kupata majeraha makubwa kama yale yaliyompata Uhuru Seleman, wanamuona Nsajigwa kama mbadala halisi atakayefaa kuziba mapengo kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Mtoa taarifa anasema, "Nsajigwa bado ni mchezaji mzuri sana, na uwezo mkubwa na kikubwa zaidi ni uzoefu alionao ambao ni hazina kubwa kwa klabu kama yetu ambayo sasa tunajaribu kuingiza vijana wadogo kama akina Singano, na ndio maana tumeamua kuanza harakati za kumsajili na kwa hakika tutafanikiwa."

MZALENDO -'' YANGA SASA TUNAMTAKA SHOMARI KAPOMBE ''

VIDEO: MAGOLI YOTE TANZANIA 2:1 GAMBIA

EURO 2012 UKRAINE VS SWEDEN: VITA YA ZLATAN IBRAHIMOVIC NA SHEVCHENKO: NANI KUIBUKA MSHINDI?


VIKOSI VINAVOTARAJIWA KUANZA
Ukraine: Pyatov, Selin, Rakitskly, Kucher, Gusev, Tymoschchu, Konoplyanka, Voronin, Yarmolenko, Milevskly, Shevchenko.

Sweden: Isaksson, Olsson, Mellberg, Granqvist, Lustig, Kallstrom, Elm, Larsson, , Rosenborg, Ibrahimovic


MAMBO MUHIMU KUHUSU TIMU ZOTE MBILI
  • Ukraine inabidi wachague kati ya Artem Milvskiy, Andrey Voronin, Marko Devic na veteran Andrey Shevchenko kuanza kwenye safu ya ushambuliaji, huku tishio lao kubwa likiwa linatokea kwenye winga.
  • Makinda Konoplyanka na Yarmolenko watakuwa na mzigo mkubwa wa kuleta ubunifu kwenye kiungo cha timu hiyo mbele ya mashabiki wao wa nyumbani, kwa hakika watakuwa kwenye presha kubwa ya kufanya vizuri huku wakiwa na umri wa miaka 22 tu.
  • Anatoliy Tymoshchuk ndio atakuwa kiungo mkabaji wa kuulinda ukuta wa timu yake, huku beki wa kulia akiongoza mashambulizi kutokea pembeni.


  • Ishara za mapema zinaonyesha kwamba Markus Rosenborg ataanza mbele ya dhidi ya Johan Elmander, huku tegemeo lao Zlatan Ibrahimovic akiongoza safu hiyo ya ushambuliaji.
  • Toivonen atarudi kwenye nafasi yake aliyoizoea ya bekiwa kushoto, huku Rasmus Elm akitegemewa kushirikiana na Kallstrom mbele ya veteran Anders Svensson.
  • Sweden wanaweza kukichezesha kikosi kile kile kilichoshinda kwenye mechi ya karibuni dhidi ya Serbia, huku Jonas Olsson akiwa nje na Granqvist akianza.

TAKWIMU
Kumekuwepo na wastani wa zaidi 2.5 wa magoli kwenye mechi 9 za Sweden kwenye Euro.


Sweden wameshinda mechi zao 6 kati ya 7 za mwisho za Euro.


Sweden wamefunga angalau mabao 2 katika kila mechi zao 6 kati ya 7za Euro.



EURO 2012: ENGLAND BILA WAYNE ROONEY KUACHA UTEJA KWA UFARANSA LEO?

VIKOSI VITAKAVYOANZA
France: Lloris, Debuchy, Rami, Mexes, Evra, Diarra, Cabaye, Ribery, Malouda, Nasri, Benzema


England: Joe Hart, Johnson, Terry, Lescot, Ashley Cole, Milner, Parker, Steven Gerrard, Oxlade-Chamberlain, Ashley Young, Welbeck


MAMBO MUHIMU KUHUSU TIMI ZOTE MBILI
  • France wanaingia kwenye mchezo wao huku wakiwa na crisis kwenye safu ya kiungo huku Yohan Cabaye ndio pekee aliye fiti kwa asilimia mia, huku M'Vila, Matuidi na Diarra wakiwa na shaka juu ya ufiti wao.
  • Patrice Evra amekuwa akishutumiwa kwa kucheza chini ya kiwango lakini anaonekana ataanza mbele ya Gael Clichy, huku vita kubwa ya namba ya kiungo mshambuliaji ikiwa kati ya Menez, Malouda na Valbuena.
  • Karim Benzema atapata nafasi ya kuanza, huku Olivier Giroud akiwa anasubiri kwenye benchi.
  • Akifunga goli lake la kwanza la mechi ya kimataifa katika mchezo wa hivi karibuni dhidi ya Ubelgiji, kumemfanya Welbeck apate nafasi kubwa ya kuanza leo mbele ya Andy Carroll, ambaye nae kama Giroud, ni hatari sana kwa mipira ya juu.
  • Ashley Young anategemewa kupewa free role nyuma ya mshambuliaji, huku James Milner na Alex Oxlade Chamberlain wakipewa nafasi ya kuanza mbelel ya Downing na Theo Walcott kwenye winga.
  • Safu nyingine yenye upinzani mkubwa ni ulinzi wa kati, mtu wa kucheza sambamba na Terry, Hodgson kichwa kinamuuma ampe nafasi nani kati ya Lescott au Phil Jagielka.
  • Wayne Rooney ndio anaanza adhabu yake ya kusimamishwa michezo miwili baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kufuzu dhidi Montenegro.
TAKWIMU
England wamefunga atleast magoli 2 katika mechi zao 12 kati ya 15 za Euro Cup.


Kumekuwepo na wastani wa 2.5 wa mabao yaliyofungwa kwenye mechi 9 za mwisho za Euro za Ufaransa.


Ufaransa hawajafungwa kwenye mechi zao 9 za Euro Cup.


Ufaransa wameifunga England katika mechi zao 3 za mwisho kwenye mashindano yote.


England hawajafungwa kwenye mechi zao 8 za mwisho za Euro Cup.



Sunday, June 10, 2012

GOLI LA PILI LA STARS LILIANZIA HAPA!

Azam FC yaanza rasmi mazoezi Leo

Kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall anatarajiwa kuwasili nchini leo asubuhi kwa ajili ya kuanza program ya maandalizi kwa mashindano ya kombe la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Stewart alikuwa nchini Uingereza kwa mapumziko baada ya kumaliza msimu uliopita kwa mafanikio ya kutwaa medali ya fedha kwa kuwa washindi wa pili wa VPL.
Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa jana ameiambia tovuti ya http://www.azamfc.co.tz/ kuwa wataanza mazoezi jioni kutokana na kocha huyo kurudi asubuhi ya siku hiyo.
Akizungumzia wachezaji wengine alisema, wachezaji wote wa kimataifa wameshawasili tayari kwa kuanza mazoezi hayo wakiwa pamoja na wachezaji wengine. Mazoezi hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Azam Chamazi jijini Dar es Salaam.
Idrissa aliongeza kuwa wachezaji waliopo timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ watajiunga mara baada ya kumaliza michezo yao, na wale wa Zanzibar Heroes watarejea nchini baada ya kumaliza michezo ya Kombe la Dunia kwa nchini ambazo sio wanachama wa FIFA.
Aliwataja wachezaji waliowasili kuwa ni George Odhiambo na Ibrahim Shikanda kutoka nchini Kenya ambao wote waliingia Alhamis, Tchetche Kipre na Michael Kipre kutoka nchini Ivory na Joseph Owino wa Uganda.
Idrissa alisema wachezaji wa Tanzania nao wameshaandaa mazingira kwa ajili ya kuanza mazoezi hayo wakiwemo vijana kutoka Azam Academy ambao wamepanda kuicheza timu kubwa, Aishi Salum, Juckson Wandwi, Dizana Issa, Ibrahim Rajab ‘Jeba’ na Joseph Kimwaga.
Aidha Idrissa alisema Azam Academy wameshaanza mazoezi siku ya Ijumaa isipokuwa wacheza watatu ambao bado hawajawasili kujiunga na timu hiyo.

SOURCE: azamfc.co.tz

MAKOCHA BONIFACE MKWASA NA KAIJAGE WAISIFIA STARS - WAMWAMBIA KIM ASHUGHULIKIE UMALIZIAJI





EXCLUSIVE INTERVIEW: MBWANA SAMATTA - TIMU YETU BADO CHANGA NA INAHITAJI UZOEFU NA SAPOTI YENU MASHABIKI



EXCLUSIVE INTERVIEW: FRANK DOMAYO KINDA LA STARS LILONG'ARA DHIDI YA GAMBIA

EXCLUSIVE: KIM POULSEN - TIMU YANGU BADO CHANGA INAHITAJI UZOEFU ZAIDI







EXCLUSIVE INTERVIEW: SURE BOY NA MRISHO NGASSA WASHUKURU SAPOTI YA MASHABIKI

WAHESHIMIWA ZITTO KABWE NA IDD AZZAN WALIWAPA SAPOTI TAIFA STARS

ANGALIA ERASTO NYONI ALIVYOPIGA PENATI YA USHINDI WA STARS

TAIFA STARS YANG'ARA TAIFA - WATANDIKA GAMBIA 2-1

Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza leo.
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gambia jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, katika mechi ya pili ya Kundi C, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Stars ilitoka nyuma kwa 1-0 kipindi cha kwanza na kuibuka na ushindi huo- kwa mabao ya kipindi cha pili ya Shomari Kapombe dakika ya 60 na Erasto Nyoni dakika ya 87 kwa penalti, baada ya beki mmoja wa Gambia kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Stars ambayo mechi ya kwanza ilifungwa 2-0 na wenyeji Ivory Coast mjini Abidjan Jumamosi iliyopita, kipindi cha kwanza ilicheza ovyo kidogo, lakini kuingia kwa Haruna Moshi ‘Boban’ aliyechukua nafasi John Bocco ‘Adebayor’ kipindi cha pili, kuliifanya Tanzania icheze kwa uhai na kulitia misukosuko lango la Gambia hatimaye kupata mabao hayo mawili.
Gambia walitangulia kupata bao lililofungwa na Mamadou Ceesay dakika ya nne.

Stars sasa imejinasua mkiani mwa kundi C na kupanda nafasi ya pili badaaye Morocco kutoa sare ya 2-2 jana na Ivory Coast inayoongoza kwa pointi zake nne.

Kwa Stars huu ni ushindi wa kwanza nyumbani tangu waifunge Jamhuri ya Afrika ya Kati Machi 26, mwaka jana.
Haruna Moshi Boban na Nurdin Bakary wakiwa kwenye benchi wakiwaangalia wadogo zao wakasakata soka safi dhidi ya Gambia.

Nahodha wa Stars Juma Kaseja na mshambuliaji Mrisho Ngassa wakipozi baada ya kuwatungua Gambia.


EURO 2012: JAMHURI YA IRELAND DHIDI MAFUNDI WACROATIA NANI KUIBUKA MBABE.

VIKOSI VITAKAVYOANZA LEO

Ireland: Shay Given, John O'Shea, Ledger, Richard Dunne, Ward, Damian Duff, Whelan, Andrews, McGeady, Keane, Doyle.


Croatia: Pletikosa, Srna, Corluka, Simunic, Strinic, Kranjcar, Luka Modric, Dujmovic, Rakitic, Eduardo, Mandzukic


  • Giovanni Trapattoni ametoa ishara kwamba anaweza kuuacha mfumo wake wa 4-4-2 uliokuwa ukimpa nafasi ya kuwa na viungo wengi, lakini pia akasema anahisi Robbie Keane anaweza kucheza kama mshambuliaji pekee hivyo mabadiliko kwenye kikosi yanaweza kujitokeza.
  • Kevin Doyle anapewa nafasi kubwa ya kuanza mbelel ya Long na Walters pamoja na kutokuwa na msimu mzuri na Wolves.
  • Mashabiki wengi wa Ireland wamekuwa wakitaka kumuona James McClean ajaribiwe kwenye mechi kubwa lakini wanaweza kumuona kinda hili likipata nafasi ya kucheza kama sub, huku Andrews na Whelan wanaweza kumtoa Gibson.
  • Utawala wa Slaven Bilic kama kocha wa Croatia utaisha baada ya michuano hii na kwa hakika ana maamuzi ya kugumu kwenye kikosi chake hasa katika safu ya ulinzi, huku bekiwa kati Dejan Lovren na Ivica Olic wakiondolewa kwenye mashindano kwa majeruhi.
  • Kwenye safu ya ushambuliaji kichwa kinampasuka juu ya uteuzi wa kuanza na Jelavic au Eduardo, huku Mario Mandzukic akicheza kama mshambuliaji wa pili.
  • Dujmovic na Vukojevic wanapigania nafasi ya kuanza kwenye kiungo mkabaji, wakati Kranjcar na Rakitic wakipewa nafasi kubwa ya kucheza kwenye wings.
TAKWIMU

Croatia hawajafungwa katika mechi 25 kati ya 28 za mwisho za EURO Cup.

Croatia wamekuwa na ukuta mgumu usioruhusu bao kwenye mechi 3 za mwisho za EURO.

Ireland hawajafungwa katika mechi zao 9 za mwisho za EURO.

EURO 2012: SPAIN DHIDI YA ITALIA - VITA YA WAPIGA PASI BORA XAVI NA ANDREA PIRLO

VIKOSI VINAVYOATARAJIWA KUANZA LEO


Spain: Iker Casillas, Arbeloa, Sergio Ramos, Jordi Alba, Segio Busquets, Xavi, Alonso, Iniesta, Torres, Silva.


Italia: Buffon, Bonucci, Chiellini, Rossi, Baizaretti, Marchisio, Pirlo, Nocerino, Maggio, Balotelli, Cassano.

MAMBO MUHIMU KUHUSU MECHI HII


  • Tangu kuumia kwa Carles Puyol na David Villa wote waondolewe kwenye Euro 2012 kwa majeruhi, Spain hawajapata habari nyingine mbaya ya majeruhi.
  • Wamecheza mechi kadhaa za kirafiki hivi karibuni huku Del Bosque akikbadilisha kikosi mara kwa mara bila tatizo lolote, na katika michezo yote walipata matokeo.
  • Kiuhalisia wachezaji wote wenye majina makubwa wataanza kwenye hii mechi, baada ya mambo kubadilika kwenye mechi za kirafiki. Andres Iniesta alitokea benchi na kucheza vizuri kusababisha ushindi dhidi ya China, leo atarudi kwenye line up katika mchezo ambao unatajwa kama mgumu zaidi kwa Spain kwenye hatua ya makundi.
  • Andrea Barzagli ameripotiwa kuwa na mashaka juu ya kucheza kutokana na majeruhi ambayo yatafanya asiweze kucheza mbili za kwanza au zaidi. Cesare Prandelli amemuita Davide Astori kwenye stand by list na atafanya maamuzi Ijumaa kama amrudishe Barzagil nyumbani au kuendelea nae mbele akiwa na matumaini ya atapona.
  • Waitaliano leo wanaweza kutumia mfumo wa 3-5-2 huku Daniele de Rossi akicheza nyuma na Marchisio na Balzaretti wakicheza kwenye mashavu ya kushoto na kulia.
TAKWIMU
Spain wameshinda mechi 10 zilizopita kwenye Euro Cup

Italy hawajaruhusu wavu wao kuguswa katika mechi 8 kati ya 9 kwenye Euro Cup.

Spain wamefunga atleast goli 2 katika mechi zao 8 za Euro Cup

Italy hawajafungwa katika mechi zao 13 kwenye Euro Cup.

Spain hawajaruhusu wavu kuguswa katika mechi zao 3 za mwisho dhidi ya Italia kwenye mashindano yote.

Saturday, June 9, 2012

MESSI AWAFUNDISHA SOKA WABRAZIL: APIGA HAT TRICK ARGENTINA WAKIUA BRAZIL 4-3

SUPER MARIO GOMEZ AIPA UJERUMANI USHINDI MGUMU DHIDI YA URENO


Germany 1-0 Portugal (Euro 2012 - Group B) by fasthighlights-2012

VAN PERSIE NA WENZIE WAGONGWA KIDUDE KIMOJA NA DENMARK


Netherlands 0-1 Denmark | utakmice.net by sportsbett

JE MNAIFAHAMU COASTAL UNION?PATA HISTORIA KAMILI HAPA


Tanga City is the home of Coastal Union Sports Club. Coastal Union has been founded in 1948 after a group of school boys
from different schools along the coastal area especially Tanga Municipality by then, who came from various street
soccer clubs, united and formed one soccer club and named it Coastal Union. Through member’s contribution the club
rented ...a house at street no 11 Ngamiani ward in the then Tanga Municipality and it became the club house. The club was
legally registered in the same year and was officially named Coastal Union Sports Club with its official logo bearing a shield
and fox. As the club progressed it attracted many fans all over Tanga and the first achievement the club got was buying its
own club house situated at the same street no. 11 where it remains the official club house to-date.

Honours: Lifted the NARGIS CUP in 1950 after beating Arab Boys in the final, another Tanga soccer club. Arab
Boys later united with Coastal Union Football Club.

In Tanga there are several soccer clubs but rival to Coastal Union is African Sports Club once a very powerful club but now trades its .
soccer in the lower division. Apart from African Sports, Coastal Union has been challenging major clubs in the country such
as Simba Sports Club, Dar Es Salaam Young Africans Sports Club and Cosmopolitan Football Club.

Coastal Union Sports Club was among one of the top clubs in Tanzania to participate in the first major league in the country in 1961 after the country’s independence. Other top clubs that took part in this first major league are:
1. Dar Es Salam Young Africa (Yanga) of Dar es salaam
2. Sunderland (now Simba Sports Club) of Dar es salaam
3. Cosmopolitan Football Club of Dar es salaam
4. African Sports Football Club of Tanga.

In 1982 Coastal Union Sports Club were runner’s up in the Tanzania Major League but we could not participate in the then Africa Cup Winners Cup due to financial problems on the part of the Football Association of Tanzania.

In 1988 Coastal Union Sports Club was crowned Tanzania Champions and hence got a ticket to participate in two major championships,
1. East and Central Club Championship in Kenya.
Results: We beat Nchanga Rangers of Zambia in the quarter final and went on to beat the Kenya champions, Abaluhya FC in the semifinal 6-5 on penalties but we got beaten by Kenya Breweries in the final.
2. African Club Championship.
Results: We were eliminated in the first round by Costa de Sol of Mozambique.

In 2002 Coastal Union was relegated from the Super League to the lower league. After spending almost 5 seasons in the lower league, Coastal Union Sports Club was promoted to the now Premier League in 2007/08 season. Again it was relegated in the same season. During the 2010/2011 season Coastal Union Sports Club gained promotion again to the premier league where it got a ticket to participate in the 2011/2012 season and managed to finish in fifth position.

The year 1961 saw Coastal Union loosing most of its prominent players to the newly formed soccer team from sugar planting company known Tanzania Planting Company (TPC) of Moshi, Northern Tanzania. This team had a mixture of players from all over East African Region and again US players were the backbone of TPC club and these were:-
1. Mbwana Abushiri (a.k.a Director)
2. Marshed Seif
3. Shariff Salim
4. John Lyimo
5. Khatibu Mtoto
6. Suwed Abdallah
7. Hemed Seif
8. Sembwana Behewa

Despite of losing its top players all being 1st eleven players, Coastal Union was never shaken by this because it still had a cream of players in the likes of:-
1. Habibu Rhemtulah
2. Mohamed Shossi (a.k.a Springet)
3. Mohamed Muslii
4. Awadhi Bafadhil
5. Hassan Mzaramo
who went on to bring more honors to the club by successfully participating in other national competitions and winning the following trophies:-

1. HEALTHO CUP (1957)
2. MWAFRIKA CUP (1958)
3. OFUMA CUP (1976)

We were finalist in the
1 1971 BIMA CUP (a competition organized by The National Insurance Corporation), losing 1-0 to Simba Sports Club.
2 1987 Finalist AICC Cup Arusha (an international competition organized by Arusha International Conference Centre). We lost to Nchanga Rangers of Zambia.

International friendly games.

1979 in Tanga Coastal Union vs Water Corporation FC of Nigeria Results 1-0 (played in Tanga)

Coastal Union was then invited to Nigeria by the Water Corporation Football Club and played 3 friendly games
1. Bendel Insurance vs. Coastal Union Results 4-1 (Bendel were 1979 runner’s up in the Africa Club Championship)
2. Housing Corporation vs Coastal Union 0-1 won
3. Water Corporation 0-0 drew
4. Odo state club 2-1 lost

On our way back we stopped in Ethiopia and played a friendly game against Ethiopia National Team and lost by 2-1.

Invited to Burundi and played one friendly game against
Vitalo FC of Burundi 0-0

For the past 5 decades CUSC has been the core club in providing players to the regional and national team where in competition such as Sunlight Cup (Inter Regional Competition later known as Taifa Cup) Gossage Cup (a competition involving East African countries, later renamed East African Challenge Cup) CUSC players were involved.

Players that were frequently selected to the national team for Sunlight and Gossage cups were:
1. Marshed Seif (Deceased)
2. John Lyhimo ( now team Manager under 20 national team)
3. Sharrif Salim (Deceased)
4. Mbwana Abushiri
5. Sembawana Behewa
6. Hemed Seif

The trend of CUSC providing players to the national team continued with such players
1 Kinanda Zakaria (Deceased)
2 Rashidi Moyo (Deceased)
3 Salim Amiri
4 Zaharan Makame
5 Mbwana Mtoto (Deceased)
6 Jalala Mursal
7 Mohamed Salim
8 Mohamed Makunda (Deceased)
9 Godfrey Nguruko
10 Mohamed Muslii
11 Salim Omar
12 Muhaj Alli
13 Saidi George
14 Ali Maumba
15 Hussein Mwakuluzo
16 Douglas Muhani
17 Mohamed Mwameja
18 Yasini Abuu Napili
19 Razaq Yusuph (a.k.a Careca)
20 Rifatih Saidi (Deceased)
21 Yanga Bwanga
22 Jumbe Makata
23 Mohamed Kampira
24 Juma Mgunda (Current assistant coach of CUSC)
25 Abdallah Saleh (Sabebe)
Other Facts:

1. Founded in 1948
2. Home colours Red and White
3. Nick name: WAGOSI WA KAYA (meaning Home boys)
4. Current club residence: Street no. 11 Ngamiani ward, Tanga City
5. Team’s current coach Juma Mgunda
6. Current captain Said Sued
7. Current Chairman: Hemed Hilal a.k.a Aurora
8. Current league standing 5th position

Passed Chairmen
1 Mzee Mbwana Malau (deseased)
2 Peter Feer (deseased)
3 Hans Leopard (deseased)
4 Mzee Abuu Bakary (deseased)
5 Mzee Mjahidi (deseased)
6 Mzee Abubakar Athuman Chande (deseased)

EURO 2012: UHOLANZI VS DENMARK - SAFU BORA YA USHAMBULIAJI DHIDI YA TIMU ISIYOTABIRIKA.

Netherlands-Denmark

VIKOSI VINAVYOWEZA KUANZA
Uholanzi: 1: Stekelenburg 2: Wiel 3: Bouma 4: Heitinga 5: Vlaar 6: De Jong 7: Robben 8: Van Bommel 9: Van Persie 10: Sneijder 11: Afellay

Denmark: 1: Lindergaard 2: Wass 3: Poulsen 4: Kjear 5: Agger 6: Poulsen 7: Rhommedal 8: Kvist 9: Bendtner 10: Erikssen 11: Kron-Dehli

MAMBO MUHIMU KUHUSU MECHI
  • Kumekuwepo na tetesi kwa wiki kadhaa kuelekea Euro 2012 kuhusu kama meneja wa Uholanzi Bert van Marwijk atawachezesha washambuliaji wake wawili Klaas-Jan Huntelaar na Robin van Persie, pamoja kupenda kutumia mfumo wa 4-2-3-1 katika kufuzu, van Persie alikuwa akichezeshwa upande wa kulia lakini amekuwa akicheza pekee yake mbele katika mechi za kirafiki za hivi karibuni ikiwemo mechi waliowafunga Ireland mabao 6-0.
  • Ibrahim Afellay pia alicheza vizuri kwenye mechi hiyo, akifunga bao zuri na akiongeza lingine kwa penati. Anaweza kuanza kwenye mchezo wa leo kama kocha ataamua kutumia mfumo wa kushambulia zaidi, akimuacha Van Marwijk akiwa na machaguo mengi kwenye benchi, huku Huntelaar, van der Vaart na Kuyt pia wakiwa na nafasi ya kuanza.
  • Joris Mathijsen pia ana wasiwasi wa kucheza kwenye mchezo wa ufunguzi kwa majeruhi aliyoyapata wiki iliyopita.
  • Wilfred Bouma anahangaika kuweza kuimudu nafasi ya beki wa kushoto huku vijana Jetro Willems na Stijn Schaars wakiwa wameonyesha viwango vizuri.
  • Denmark
  • Denmark hawana majeruhi mpya kwenye kikosi, lakini kuna maswali mengi juu ya nani anapaswa kuanza kwenye kikosi.
  • Chistian Poulsen hakuanza katika mechi dhidi ya Australia wiki iliyopita na Niki Zimling anaweza akaanza tena.
  • Pia kumekuwepo na na wasiwasi kuhusu kiwango cha Christian Eriksen, lakini pia kumekuwepo na waiwasi kidogo juu ya nafasi yake ndani ya kikosi lakini uwezo wake na ubunifu ni kitu ambacho Denmark wanahitaji.
  • Wass na Lars Jacobsen wapo kwenye upinzani wa nafasi ya beki wa kulia.

TAKWIMU
Denmark wameshinda mechi zao 4 za mwisho za Euro Cup.

Uholanzi wamekuwa wakifunga mabao atleast mawili katika mechi 6 kati ya saba za mwisho za kombe la Euro.

Denmark wamekuwa wakifunga mabao atleast mawili katika mechi 4 za mwisho za kombe la Euro.

EURO PREVIEW: UJERUMANI VS URENO: RONALDO KUWAOKOA URENO DHIDI WAJERUMANI?


VIKOSI VINAVOTARAJIWA KUANZA.
Ujerumani: 1: Neur 2: Boateng 3:Lahm 4: Bedstuber 5: Mertesacker 6: Khedira 7: 8: Schwensteiger 9: Klose 10: Ozil 11: Podolski

Ureno: 1: Patricio 2: Pereira 3: Coentrao 4: Alves 5: Pepe 6: Veloso 7: Moutinho 8: Meireles 9: Postiga 10: Ronaldo 11: Nani




Germany
  • Per Mertesacker amerudi na yupo fiti baada ya kuumia na kukosa nusu ya msimu akiwa na Arsenal. Anatarajiwa kuanza kwenye mechi ya leo akiunda safu ya ulinzi na Badstuber huku Hummels akisubiri kwenye benchi.
  • Bastian Schweinsteiger hajaichezea Ujerumani katika mechi za kirafiki za hivi karibuni lakini amerudi kwenye kikosi na ataanza kwenye mechi ya leo, ingawa yeye, Kroos na Khedira watakuwa wakipigania nafasi mbili za safu ya kiungo cha kati.
  • Magoli aliyoyafunga kwenye mechi dhidi Switzerland na Israel yanamuweka Andre Schurrle katika nafasi ya kugombania namba ya kuanza kwenye winga ya kushoto, ingawa Podolski ana nafasi kubwa ya kuanza, huku Klose akitegemea kuanza badala ya Gomez.Goals in the games against Switzerland and Israel have put Andre Schurrle right in contention to start on the left flank, though Podolski is likely to be favoured, with Klose also set to get the nod over Gomez up front
  • Nani ana wasiwasi mkubwa wa kucheza kutokana na majeruhi, amekuwa akifanya mazoezi ya pekee yake tofauti na wenzake
  • Manager Bento atahitaji sana winga huyo wa Manchester United awe fiti kwa kuwa washambuliaji wake wa pembeni ndio silaha yake kubwa baada ya washambuliaji wake wa kati wakiongozwa na Postiga kukosa makali.
  • Rui itabidi aanze kwenye milingoti mitatu mbele ya Eduardo na kinda Beto, huku akiwa chini ya ulinzi wa mabeki wazoefu Bruno Alves na Pepe.

TAKWIMU
Ujerumani wameshinda mechi 10 za mwisho za Euro Cup

Ujerumani wamefunga atleast magoli matatu katika kila mechi nane za mwisho za Euro Cup.

YANGA WAMEFANYA UHUNI KUMSAJILI KELVIN YONDANI ?

Kanuni za ligi kuu ya Vodacom kama zilivyorekebishwa na kupitishwa tarehe 20 julai 2009 na kusainiwa na Rais wa TFF bwana L.C. Tenga na bwana F. Mwakalebela aliyekuwa Katibu Mkuu zinaeleza kinagaubaga jinsi shuguli za usajili na uhamisho wa wachezaji zinavyobidi kufanywa.

Msimu unapokwisha kanuni ya 49 inaeleza kwamba” klabu itawasilisha TFF kwa maandishi, majina ya wachezaji watakaositisha mikataba yao/ kuwa huru katika usajili wa msimu wa ligi katika muda wa uhamisho utakaotangazwa na TFF na kitalazimika kumpa taarifa ya maandishi/ mchezaji au wachezaji husika”. Kanuni hii inaipa mamlaka klabu kwamba ndiyo yenye kuitaarifu TFF juu ya mchezaji yupi yuko huru na ambaye hayupo huru, Simba Sports Club haijawahi kuiandikia TFF juu ya mchezaji Kelvin Yondani kuwa huru na isingeiambia kwamba yupo huru kwa sababu ana mkataba aliousaini tarehe 23/12/2011 ambao kwa mujibu wa kanuni ya 46 mkataba huo unapashwa kuwasilishwa kwa pamoja na mikataba mingine kwa ajili ya usajili wa msimu wa 2012/2013 kama kifungu hicho kinavyosema “Kilabu zinatakiwa kukamilisha na kuwasilisha kwa pamoja usajili wa timu zote mbili pamoja na majina na mikataba ya makocha wa timu za wakubwa na vijana katika kipindi cha usajili” Kifungu namba 40 kinaeleza kwamba maombi ya usajili wa mchezaji wa kulipwa lazima yawasilishwe pamoja na nakala ya mkataba wa mchezaji, hivyo wakati wa usajili mkataba wa kuendeleza mkataba uliopita kati ya Simba na Kelvin Yondani ndipo unapopashwa kuwasilishwa ingawa Simba imeuwasilisha mapema ili kulionyesha shirikisho hali halisi inayoendelea.

Pamoja na Simba kutoiandikia TFF kwamba Yondani ni mchezaji huru kwani muda haujafika pia kanuni za TFF na zile za FIFA za Regulation on the Status and Transfer of Players katika article 18 na kanuni za TFF katika kanuni ya 44 ambazo zipo “mutatis mutandis” kwa maana kwamba zimenakiliwa herufi kwa herufi lakini zimetofautiana lugha kwani moja ni kiingereza na nyingine ni Kiswahili inaeleza kwamba “kilabu inayotarajia kuingia mkataba na mchezaji wa kulipwa haina budi kuiarifu klabu yake ya sasa kwa maandishi kabla ya kufanya makubaliano na mchezaji wa kulipwa. Mchezaji wa kulipwa atakuwa huru tu kujingia mkataba na klabu nyingine iwapo mkataba wake na kilabu yake ya sasa umekwisha au utakwisha baada ya miezi sita. Uvunjaji wowote wa sharti hili utastahili vikwazo vinavyofaa.
Hili pia limeelezewa katika kanuni ya 57 (1) kwamba “Kilabu kinachotaka kumsajili mchezaji aliyesajiliwa na kilabu kingine au mwenye mkataba na kilabu kingine, kitalazimika kuafikiana na kilabu chake kabla ya kumsajili mchezaji huyo”. Sababu kubwa ya kuhimiza mawasiliano baina ya klabu mbili ni kwanza kujua kama mchezaji huyo ana mkataba wa nyongeza na timu husika lakini zaidi ya hayo ni kuhakikisha kwamba mchezaji huyo haathiriwi na mazungumzo ya timu nyingine wakati anatekeleza mkataba uliobaki. Yanga walichofanya ni kumrubuni mchezaji kwa kuongea nae bila kibali cha Simba Sc lakini pia wangeomba kibali Simba Sc ingewaeleza kwamba mchezaji huyu ana mkataba mwingine alioisha usaini. Kwa mujibu wa kanuni za TFF na FIFA kitendo cha Yanga kuongea na mchezaji wa Simba SC bila kuiandikia simba chochote ni kosa kubwa sana ambalo Simba inaishitaki Yanga iadhibiwe kwa kufungiwa usajili wake wote wa mwaka huu na mwaka ujao.
Pamoja na hayo timu haiwezi kumsajili mchezaji ata kama amekuwa huru bila kuwasiliana na klabu yake ya zamani kwani idhinisho la usajili lazima litolewe na klabu yake ya zamani kama kanuni namba 57 (2) inavyoelekeza hivyo hakuna namna yoyote ambayo Yanga inaweza kumsajili Kelvin Yondani bila Simba kupewa taarifa kwanza. Hili limesisitizwa zaidi katika kanuni ya 45 (6) kwamba “mchezaji ambaye ameingia mkataba wa zaidi ya msimu mmoja hatoruhusiwa kujisajili na klabu kingine kabla ya klabu yake mpya kuafikiana na klabu yake ya zamani” mkataba ulioisha wa Kelvin Yondani ulikuwa ni wa miaka miwili na ulioongezwa ni wa miaka miwili pia.

Mabezo haya yanaitia yanga hatiani kwa pande zote kwani maamuzi ya kama Kelvin ni mchezaji huru yanatolewa na Simba SC kama ikiwasilisha barua TFF juu ya wachezaji ambao wanamaliza mikataba au wanasitisha mikataba. Simba SC haijafanya hivyo kwa sababu muda wake bado, kwa mantiki hiyo yoyote anayetaka kujua mustakabari wa Kelvin inabidi awasiliane na Simba SC na jibu atakalopata ni kwamba Kelvin sio mchezaji huru, ana mkataba na Simba ambao kausaini na kuutia dole gumba (dole gumba lina alama za kipekee za mhusika ambazo hawezi kuzikana kama ilivyo kwa DNA).

Yanga wamefanya uhuni wa kumsajili Kelvin Yondani usiku wa tarehe 6/6/2012 kwa ushahidi uliopo, lakini wanasema mkataba umesainiwa ama October 2011 au February 2012, Simba SC itamshitaki wakili yoyote katika Tanganyika Law Society ambaye atashuhudia mkataba huo kwa kuurudisha tarehe za nyuma na kuomba chama hicho cha mawakili kimsimamishe mhusika uwakili.

Friday, June 8, 2012

ARSHAVIN AWAONGOZA URUSI KUWAGONGA 4-1 CZECH


Russia 4-1 Czech Republic (Euro 2012 - Group A) by fasthighlights-2012

WENYEJI POLAND WAANZA KWA SULUHU - KIPA WA ARSENAL APIGWA KADI NYEKUNDU


Poland 1-0 Greece (Euro 2012 - Group A) - All... by fasthighlights-2012

goli la siku

Q&A with John Bocco

John Bocco @ SS com



Taifa Stars Striker John Bocco is the hottest property in Tanzanian football.
The 23 year old has been Azam's top scorer since, joining the club in 2007. He managed to score nine goals in his first season (2009/10) in the Tanzania Vodacom Premier League and scored 13 goals in the following term.
Last season he emerged top scorer in the Vodacom Premier League netting 18 times. He is a prolific striker and a top asset for both club and country.

SuperSport.com caught up with the Taifa Stars striker ahead of their world cup qualifier against The Gambia.

SuperSport.com: What was the feeling after finishing the top scorer in the Tanzania Vodacom Premier League?

Bocco: It was the best moment of my career, to become the top scorer in the league. Its a great achievement for a young player like me, who still has a lot of years to play. And I'm aiming to maintain my performances and try to achievement in the future.”

SuperSport.com: How was your trip to Abidjan and the game against Ivory Coast?

Bocco: Our trip was good. The climate in Abidjan is like here in Dar es Salaam. We trained well, we played the game and we lost the game at the end. It was painful to us players, but that's how football is and you have to accept the results as a player.”

SuperSport.com: How was it like to play against World class players like Didier Drogba, Yaya Toure and many others?

Bocco: Its very fortunate for us players who play in local leagues to meet such high rated names face to face. And it gives us courage and comfort, for players like us who want to be like them in the future. It was tough playing against them.

SuperSport.com: How are the training sessions getting through?

Bocco: We have had several training sessions previously, and some in the future - and the players are doing well and responding positively to the coach. And we players have a close relations and united, and really working hard in training focusing on the next game.

SuperSport.com: How do you find your partnership with TP Mazembe striker Mbwana Samatta in the frontline?

Bocco: He is a great player, good lad too. And his contribution in the team is great, its good to have a top performer like him in the team. We are good friends.

SuperSport.com: How do you find Kim Poulsen as the National Team coach?

Bocco: He is a good man, wise too. He has been doing pretty well with us, he teaches well and we players understand him well. I have seen changes in the team since the game against Malawi in terms of what he has been teaching us. There is an improvement in the team. And we keep on working harder and harder.

SuperSport.com: What are your expectations towards the game against Gambia?

Bocco: We expect the game to be tough, but we as players and after losing our first game, we will go out there with full spirit to win the game and turn this round for us.

SuperSport.com: What will be the feeling, when the National team qualifies to the World Cup?

Bocco: It will be a historical moment, it will be unbelievable moment for the players and the country. Because I believe it has never happened for Tanzania. We will work hard, to play in world cup one day.

SuperSport.com: What do you say to the home supporters towards the game against Gambia this weekend?

Bocco: I call on for full support from all Tanzanians, and come cheer us as Supporters not as fans, because when we are out there we represent the whole country, and we do it for the country. Their support will be vital to us, and they will make us fight till the end to get the best results, because football is a game of 90 minutes.

No comments: