MAN CITY KUMSAJILI STURRIDGE
Sturridge |
KLABU ya Manchester City
inajiandaa kumsajili Daniel Sturridge wa Chelsea kwa dau la pauni Milioni 10,
ikitumia mwanya wa mchezaji huyo kuboreka na klabu yake ya sasa.
Inafahamika kwamba Roberto
Mancini anataka kumsajili tena mchezaji huyo aliyekuzwa Man City na kuna imani
ataendelea vizuri kisoka akiwa Etihad.
Sturridge amebakiza mwaka
mmoja tu katika mkataba wake Chelsea na anaangalia upya mustakabali wake baada
ya kuwa anasugua makalio benchi miezi ya mwishoni mwa msimu, kiasi cha kukosa
nafasi kwenye kikosi cha England cha Euro 2012.
City inapewa nafasi kubwa ya
kuinasa saini ya kinda huyo wa miaka 22, anahusishwa mno na mpango wa kurejea
Manchester na alipigwa picha hivi karibuni katika mapumziko, akiwa na Micah
Richards, visiwa vya Caribbean.
Anaangalia mustakabali wake
katika wakati ambao Chelsea inakisuka upya kikosi chake katika safu ya
ushambuliaji, kwa kubeba nyota wapya kama Hulk, Eden Hazard na Marko Marin,
wakati Kevin De Bruyne pia atatua moja kwa moja Stamford Bridge kwa ajili ya
msimu ujao.
Chelsea itataka pauni Milioni
12 kumuachia Sturridge, ambaye aliwekwa kama mchezaji wa ‘spea’ kwenye kikosi
cha England, kufutaia msimu ambao aliifungia klabu yake mabao 13 na kuichezea
mechi mbili timu yake ya taifa.
Pamoja na hayo, City
ilikubaliana na Chelsea kupata asilimia 15 iwapo nyota huyo atauzwa wakati
inamuuza mchezaji wake huyo wa zamani wa akademi yao, kwenda Stamford Bridge
mwaka 2009 na kwa sababu hiyo ina matumaini ya kumsajili kwa pauni Milioni 10
tu.
Vyanzo vimesema kwamba kinda
huyo wa miaka 22, mshahara wa pauni 65,000 kwa wiki anazopewa na Chelsea
mchezaji huyo haliwezi kuwa tatizo kwa City.
Mancini anamzimikia kinoma
Sturridge na aliwahi kusema siku chache baada ya kuanza kazi Etihad kwamba
anasikitika kijana huyo kuuzwa Chelsea.
Sturridge amechanganyikiwa na
hafurahii kupangwa pembeni badala ya nafasi ya mshambuliaji wa kati, jambo
ambalo limemponza hadi kupoteza namba yake katika kikosi cha England.
Baada ya kiwango chake
kushuka, akawa anakaa benchi bila kutumika kabisa katika fainali zote, Ligi ya
Mabingwa Ulaya na Kombe la FA
No comments:
Post a Comment