GAMBIA WAJA NA NGE 11 WA ULAYA KUIVAA STARS JUMAMOSI
TIMU ya soka ya taifa ya
Gambia, The
Scorpions inatarajiwa kuwasili leo usiku saa 3:20, kikosini ikiwa na wachezaji
11 wanaocheza soka ya kulipwa nchi mbalimbali Ulaya.
Wachezaji wa kulipwa wa Gambia
watakaotua na ndege ya Kenya Airways tayari kwa mechi ya Kundi C dhidi ya
wenyeji Tanzania, Taifa Stars Jumamosi kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia
ni; Momodou Futty Danso wa Portland Timbers ya Marekani, Lamin Basmen Samateh wa
Hibernian F.C. ya Scotland, Pa Saikou Kujabi wa NK Lokomotiva ya Croatia,
Mustapha Kebba Jarju wa Mons ya Ubelgiji, Yankuba Mal Ceesay wa Djurgardens IF
ya Sweden,
Demba Savage wa HJK ya
Finland, Alieu Darboe wa Le Mans ya Ufaransa, Momodou Ceesay wa MSK Zilina ya
Slovakia, Pa Modou Jagne wa FC St. Gallen ya Uswisi, Tijan Jaiteh wa Randers FC
ya Denmark na Omar Colley wa NK Triglav ya Slevenia.
Wengine ambao wanacheaa
nyumbani ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Ousman Koli, Saihou Gassama, Bubacarr
Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry,
Ali Sowe na Saloum Faal.
The
Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku lakini kukawa na
ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya ambapo
ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es Salaam.
Timu hiyo itafikia kwenye
hoteli Sapphire iliyopo Mtaa wa Lindi na Sikukuu eneo la Kariakoo, wakati
waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi
hiyo.
Refa atakuwa Ruzive Ruzive na
wasaidizi wake watakuwa ni Salani Ncube na Edgar Rumeck, mwamuzi wa akiba ni
Norman Matemera na Kamisaa ni Fanie Wallace Mabuza kutoka Swaziland wakati
mtathmini wa waamuzi ni Ali Baligeya Waiswa.
Waamuzi hao watawasili nchini
kesho (Juni 8 mwaka huu) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways wakati
Kamishna wa mechi hiyo atawasili siku hiyo hiyo saa 12.50 jioni kwa ndege ya
South African Airways na Mtathmini wa waamuzi atatua pia Juni 8 mwaka huu saa
7.55 mchana kwa ndege ya Kenya Airways.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.
PROGRAMU YA MAZOEZI YA
GAMBIA
IJUMAA JUNI 8
01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja
wa Karume
10.00 jioni Mazoezi- Uwanja
wa Taifa
JUMAMOSI JUNI
9
04.00 asubuhi Mkutano na
Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
10.00 jioni Mazoezi- Uwanja
wa Taifa
COPA COCA COLA TAIFA JUNI 24 DAR MPAKA PWANI
MICHUANO ya Copa Coca-Cola
ngazi ya Taifa inaanza kutimua vumbi Juni 24 mwaka huu kwenye mikoa ya Dar es
Salaam na Pwani huku pambano la ufunguzi likiwa kati ya Kigoma na Lindi
litakalofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es
Salaam.
Ofisa Habari wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia leo BIN
ZUBEIRY kwamba, upangaji ratiba (draw) umefanyika leo (Juni 7 mwaka huu)
kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kushuhudiwa na
waandishi wa habari, makocha wa timu za mikoa za Copa Coca-Cola na wadhamini
kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola.
Amesema makocha 35 wa timu za
Copa Coca-Cola kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani wako kwenye kozi
ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayoendeshwa na wakufunzi
Ulric Mathiot wa FIFA kutoka Seychelles na wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF), Sunday Kayuni wa Tanzania.
Amesema mikoa 28 ya kimpira ya
Tanzania itashiriki katika mashindano hayo na imegawanywa katika makundi manne
ya timu saba saba. Baadaye timu zitapambana katika hatua ya robo fainali, nusu
fainali na fainali itakayofanyika Julai 15 mwaka huu.
Amesema Kundi A lina timu za
Arusha, Ilala, Kigoma, Kusini Pemba, Lindi, Rukwa na Ruvuma. Kundi B ni Iringa,
Kaskazini Pemba, Manyara, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza na Tanga. Dodoma,
Kaskazini Unguja, Kinondoni, Mara, Mbeya, Mtwara na Temeke ziko kundi C wakati
kundi D ni Kagera, Kilimanjaro, Kusini Unguja, Pwani, Shinyanga, Singida na
Tabora.
“Viwanja vitakavyotumika
katika mashindano hayo ambapo mechi zitakuwa zikichezwa asubuhi (saa 2.30) na
jioni (saa 10.00) ni Uwanja wa Karume na Tanganyika Packers (Kawe) kwa Dar es
Salaam. Viwanja vya Mkoa wa Pwani ni Tamco na Nyumbu. Timu zote katika
mashindano hayo zitacheza katika viwanja hivyo,”amesema.
Wambura pia amesema mbali ya
Kigoma na Lindi, mechi nyingine za ufunguzi Juni 24 mwaka huu ni kundi B
Morogoro na Manyara (saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Kawe), kundi C ni Temeke na
Kinondoni (saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Nyumbu) na kundi D ni Kilimanjaro na
Kusini Unguja (saa 2.30 asubuhi Uwanja wa Tamco).
Amesema wachezaji wanaotakiwa
kushiriki kwenye michuano hiyo ya umri chini ya miaka 17 ni wale waliozaliwa
kuanzia Januari 1, 1996
RAGE AWASHITAKI YANGA FIFA, AWAITA WAHUNI, WANAHARIBU SOKA
Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage akizungumza na Waandishi wa Habari, mchana huu makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi kuhusu sakata la Yondan |
Rage amesema leo mchana katika
Mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya Simba, Mtaa wa Msimbazi kwamba
ushahidi wa Yanga kumsajili Yondan wakati amekwishasaini Simba, ni picha
anayoonekana akisaini wakati amevaa jezi mpya ya timu ya soka ya taifa ya
Tanzania, Taifa Stars yenye nembo ya wadhamini wapya, Kilimanjaro
Beer.
Rage amesema kwamba kitendo
walichofanya Yanga ni uhuni ni kinautia aibu mchezo wa soka, hivyo amewaagiza
mawakili wa klabu hiyo kukaa leo kuandaa mashitaka ya kupeleka
FIFA.
Aidha, Rage alionyesha nakala
ya mkataba ambao Simba imesaini na Yondan, ikionyesha amepeaa fedha taslimu Sh.
Milioni 25 kwa miaka miwili.
“Simba Sports Club
imesikitishwa na kitendo cha Young Africans kuvunja taratibu za usajili kwa
kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patrick Yondan, kwanza kwa kuzungumza naye na
baadaye kwa ushahidi wa picha kuonekana wakimuandikisha makaratasi ambayo
baadaye imeripotiwa na vyombo vya Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa
kuichezea timu hiyo ya Young Africans,” alisema Rage.
Nakala za mkataba wa Yondan na Simba SC |
Alisema Yondan ni mchezaji halali wa Simba SC aliye na mkataba hadi Mei 31, mwaka 2014, baada ya kuongeza mkataba na klabu yake, Desemba 23, mwaka jana. Mkataba wa awali wa Yondan Simba uliisha Mei 31, mwaka huu. “Sheria za FIFA za hadhi na uhamisho wa wachezaji ziko wazi, katika kipengele cha 5 kifungu kidogo cha 2 kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja tu kwa wakati mmoja,”alisema Rage.
Mapema jana BIN ZUBEIRY 'ilifichua' Yondan kusaini Yanga kwa Sh. Milioni 30, mkataba wa miaka miwili- maana yake mchezaji huyo amekunja zaidi ya Sh. Milioni 55 kwa mikataba yote.
Lakini Yondan mwenyewe jana aliukana mkataba wa Simba, akisema hajasaini.
Wednesday, June 6, 2012
MAN CITY HATARINI KUMPOTEZA MANCINI
Last Updated: 07th June 2012
MANCHESTER CITY inaweza kujikuta katika inampoteza kocha wake, Roberto Mancini kutokana na nchi yake, Italia kutaka kumpa jukumu la kitaifa.
Kocha
wa sasa wa The Azzurri, Cesare Prandelli yuko kwenye shinikizo kali na matokeo
yoyote mbaya katika Euro 2012 yatamfanya afukuzwe
kazi.
Na
Mancini, mwenye umri wa miaka 47, ndio mtu anayekubalika zaidi na FA ya Italia
kumbadili Prandelli, baada ya kutwaa ndoo ya Ligi Kuu ya England.
Bosi
huyo wa City, amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Etihad. Mjadala kuhusu
mkataba mpya umekwishafanyika, lakini bado hajasaini.
Mancini
kwa sasa yupo mapumzikoni Sardinia ambako atakuwapo hadi wakati wa maandalizi ya
msimu mpya mwezi ujao.
Mtaliano
huyo amesema angependa kuikochi nchi yake siku moja, ingawa hakutarajia nafasi
hiyo ingekuja mapema kiasi hiki.
City
itasaini mkataba mpya na kocha huyo wa miaka minne , ambao utapandisha mshahara
wake kutoka pauni Milioni 3.5 hadi Milioni 5.5 kwa mwaka.
Hiyo
itamfanya awe kocha anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika Ligi Kuu ya England,
sambamba na kocha wa Manchester United, Alex Ferguson.
Kocha
huyo wa zamani wa Inter Milan amefanya kazi nzuri katika kipindi cha miaka
miwili na nusu akiwa na City.
KatikaIn
his first full season he won the club their first trophy in 35 years with the FA
Cup. Then last term he delivered City’s first title in 44
years
THREE LIONS WATUA KWA MBWEMBWE ZOTE POLAND
TIMU ya taifa ya England
imewasili Poland jana, huku mshambuliaji wa timu hiyo Wayne Rooney akiwataka
wachezaji wenzake kujituma katika Euro 2012 na kusahau matokeo mabaya ya
nyuma.
Tayari kwa kazi: Wayne Rooney
anataka kuithibitishia dunia
Wanatua: Kikosi cha England
kikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Krakow Airport jana tayari kwa Euro
2012.
Mashabiki: Watoto wa Poland
wakiilaki England katika Uwanja wa Ndege wa Balice , Krakow
Autographs: Rooney, Andy
Carroll, Scott Parker, Ashley Young na Jordan Henderson
wakisaini
Mapokezi baab kubwa: Wachezaji
wa England wakipewa shangwe wakati wanawasili katika hoteli ya Stary,
Krakow
Wanaingia ndani: Nahodha wa
England, kiungo Steven Gerrard anaonekana akifurahia kutua
Poland
Tayari kupaa: Kocha wa
England, Roy Hodgson na kikosi chake
Saini
za mafanikio: John Terry juu na Wayne Rooney wakisaini bango la wadhamini kabla
ya kuelekekea Poland kwa ajili ya Euro 2012
Anakwea ngazi: Wayne Rooney,
Steven Gerrard, Roy Hodgson na Andy Carroll na Phil Jagielka wakipanda ngazi za
ndege huko Luton kuelekea Krakow
Shangwe: Mashabiki wa England
wakiitazama ndege ikiondoka Luton kuelekea Poland na Ukraine
Nani ni nani: (kutoka kushoto kuelekea kulia) Andy
Carroll, Phil Jones, John Terry, Rob Green, Joe Hart, Jack Butland, Joleon
Lescott, Martin Kelly, Danny Welbeck (mstari wa pili) Gary Neville (Kocha), Ray
Lweington (Meneja Msaidizi), Jordan Henderson, James Milner, Glen Johnson, Scott
Parker, Phil Jagielka, Stewart Downing, Ray Clemence (Kocha wa makipa), Dave
Watson (Kocha wa makipa), (mstari wa tatu) Alex Oxlade-Chamberlain, Jermain
Defoe, Theo Walcott, Steven Gerrard, Roy Hodgson (Meneja), Wayne Rooney, Ashley
Cole, Ashley Young na Leighton Baines.
LIVERPOOL NAO WAWEKA MKWANJA MEZANI KUMNASA ADAM JOHNSON
Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya
CHELSEA KUNG'OA KIUNGO EVERTON
KLABU ya Chelsea inamtolea
macho ikitaka kumsajili kwa dau la pauni Milioni 20, kiungo wa Everton mwenye
umri wa miaka 24, Marouane Fellaini,.
KLABU
ya Queens Park Rangersinataka kumsajili mshambuliaji wa Montpellier na Ufaransa,
Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 25, ambaye thamani yake ni pauni Milioni
50.
KLABU
mpya Ligi Kuu, Southampton inajipanga kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa
Burnley, Jay Rodriguez, mwenye umri wa miaka 22, kwa dau la pauni milioni
7.
KOCHA
Chris Hughton anapanga kurejea Birmingham City kumchukua beki Curtis Davies,
mwenye umri wa miaka 27, mara atakapothibitishwa kocha mpya wa Norwich.
KLABU
ya Arsenal ipo karibu kumsajili mshambuliaji wa Malaga, mwenye umri wa miaka 22,
Salomon Randon nyota wa kimataifa wa Venezuela, ambaye imeripotiwa dau lake
katika klabu hiyo ya Hispania ni pauni Milioni 20.
KLABU
ya Liverpool inamtaka winga wa Manchester City, Adam Johnson, mwenye umri wa
miaka 24, ikiwa tayari kutoa dau la pauni Milioni 16, na itampa uhakika wa
kucheza katika kikosi cha kwanza.
NAHODHA WA BAADAYE ENGLAND
KIUNGO
wa Sunderland, David Meyler amempendekeza Jordan Henderson kuwa Nahodha wa
baadaye wa England.
KLABU
ya Chelsea imemuambia Roberto Di Matteo ingependa kumuacha aendelee kuwa kocha
na vyanzo vimesema kocha huyo atakuwa kazini Stamford Bridge mwanzoni mwa msimu
mpya.
No comments:
Post a Comment