Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya

FERGUSON AAMUA KUBOMOA BEKI

KOCHA Sir Alex Ferguson amemtia kwenye orodha ya wachezaji anaowataka beki wa kushoto wa Everton na England, Leighton Baines na kiungo wa ­Tottenham, Luka Modric baada ya kumsajili kiungo Mjapan, Shinji Kagawa kwa dau la pauni Milioni 12.
KLABU ya Napoli ya Italia, pia inamtolea macho Leighton Baines, mwenye umri wa miaka 27, ambaye anauzwa kwa kiasi cha pauni Milioni Milioni 20.
KOCHA wa West Ham, Sam Allardyce anataka kumsajili winga machachari wa klabu ya Wolves, Michael Kightly, ambaye ana umri wa miaka 26.
Leighton Baines
Manchester United na Napoli zinamtaka Baines, lakini Everton pia haitaki kumuachia.
KLABU za QPR na Sunderland zinamtolea macho kiungo mwenye umri wa miaka 26, aliyewahi kuzichezea Everton na Portsmouth, Manuel Fernandes, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru.
KLABU ya Sunderland inatumai kocha wa Aston Villa, Paul Lambert anamtolea macho mshambuliaji wa Norwich, Grant Holt na hiyo itasaidia mpango wa kumng'ao mshambuliaji Gabriel Agbonlahor Villa Park kutua Stadium Of Light.
KIUNGO wa Swansea, Gylfi Sigurdsson hatarajii kubaki katika klabu hiyo msimu ujao na amesemaq anataka kumfuata kocha Brendan Rodgers Liverpool.
MCHEZAJI anayetakiwa na Newcastle, Douglas amesema kwamba The Magpies wanamtaka kwa dhati - lakini mzaliwa huyo wa Brazil, anayechezea FC Twente pia amesema klabu kubwa Ulaya nazo zinataka huduma yake.
KIUNGO Joe Cole atarejea Liverpool baada ya kumaliza muda wake wa kucheza kwa mkopo Ufaransa, kwa mujibu wa kocha wa Lille, Rudi Garcia.

RONALDO MILELE BERNABEU

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema hana mpango wa kurejea Ligi Kuu England na anataka kucheza hadi mwisho wa maisha yake ya soka katika klabu ya Bernabeu.
KIUNGO wa Manchester City, David Silva amewaambia Real Madrid hana mpango na kuhamia klanu hiyo ya nchini mwake, kwani anafurahia maisha Uwanja wa Ethiad.
Cristiano Ronaldo
Ronaldo.
KOCHA wa Tottenham, Harry Redknapp amemtaka Mwenyekiti wa klabu hiyo, Daniel Levy kufanya haraka kumpa mkataba mpya kama wanathamini yeye kama kocha.
KOCHA wa Stoke, Tony Pulis anafikiri mshambuliaji, Peter Crouch atarejea 'mtamu' zaidi na zaidi msimu ujao, kufuatia kutemwa katika kikosi cha England cha Euro 2012.
KLABU ya Norwich inatumai kumtambulisha Chris Hughton kama kocha wao mpya - na itatuma maombi rasmi kwa kocha huyo wa Birmingham katika saa 48 zijazo.
MWENYEKITI wa Swansea, Huw Jenkins amesema kwamba ipo karibu kumtaja kocha wao mpya, na amekwishazungumza na Ian Holloway juu ya nafasi hiyo