Tetesi za Jumanne magazeti Ulaya

ARSHAVIN ANARUDI ZENIT

KLABU ya Zenit St Petersburg imeanza mazungumzo na Arsenal juu ya kumsajili tena Andrey Arshavin, mwenye umri wa miaka 31, baada ya kiungo huyo kufanya 'mavituuz' kwenye Euro 2012.
KLABU ya Paris Saint-Germain nayo imejitosa kwenye mbio za kuwania saini ya nyota wa Tottenham, kiungo Luka Modric, ikitoa ofa ya dau la pauni Milioni 30 kwa Spurs kumnasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, raia wa Croatia. Man United nayo imeonyesha dhamira ya kumsajili nyota huyo.
Marouane Fellaini
Marouane Fellaini.
KIUNGO 'baab kiubwa' wa Everton, Marouane Fellaini, mwenye umri wa miaka 24, anaweza kutimkia Goodison Park baada ya kusema: "Nataka kucheza Ligi ya Mabinhwa au Europa League. Msimu uliopita tulimaliza nafasi ya saba nikiwa na Everton, na hatukufuzu kwenye michuano ya Ulaya, ambayo ilikuwa ni aibu."
KLABU ya Liverpool inajiandaa kupambana na klabu ya Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, Schalke katika kumuwania mchesaji huru, Salomon Kalou, mwenye umri wa miaka 26, ambaye ametemwa Chelsea mwishoni mwa msimu.
KLABU za Tottenham na QPR inapigania saini ya kipa wa Birmingham, Ben Foster, lakini mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 31 tayari anatarajiwa kuhamia moja kwa moja West Brom kwa pauni Milioni 3, ambako alicheza kwa mkopo msimu uliopita.
KOCHA wa Sunderland, Martin O'Neill amepania kumbakisha katika klabu hiyo, Stephane Sessegnon licha ya tetesi zilizozagaa kwamba mustakabali wa kijana huyo wa Benin mwenye umri wa miaka 26 si mzuri katika klabu hiyo.

WILSHERE HAENDI OLIMPIKI

KOCHA wa timu ya Olimpiki ya England, Stuart Pearce ameamua kutomjumuisha kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere mwenye umri wa miaka 20 katika kikosi chake cha mwisho, baada ya kocha wa Washika Bunduki hao wa London, Arsene Wenger kushindwa kuidhinisha uteuzi huo.
WADI ya majeruhi yas timu ya soka ya taifa England inayoshiriki Euro 2012 imezidi kuongezeka idadi ya wagonjwa, baada ya kocha wa makipa Ray Clemence, mwenye umri wa miaka 63 aliyeichezea Three Lions mechi 61, kutolewa uwanjani jana baada ya kuumia katika mazoezi ya kujiandaa na mechi Ufaransa, iliyoisha kwa sare ya 1-1.