Friday, June 22, 2012

MANJI ATUA KWENYE USAILI JANGWANI, 'APIGA GOTI' KUMSALIMU BI RUKIA

Mgombea Uenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji (kulia) akimsalimia Bi Rukia makao makuu ya klabu, Jangwani jioni hii alipofika kwa ajili ya usaili

Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga mwenye suti akisalimiana na wanachama wa Yanga makao makuu ya klabu mida hii, alipofika kwa ajili ya usaili.

Mgombea Ujumbe, Peter Haule kulia akisalimiana na Clement Sanga

Wanachama wakishuhudia zoezi nje ya klabu

Manji akizungumza na wanachama

Manji na Peter Haule

Manji akiingia kwenye chumba cha usaili, Clement Sanga anatoka


ANAOMBA KUWA MAKAMU MWENYEKITI YANGA



SIMBA WAPOKEWA KIFALME MWANZA


Kikosi cha Simba msimu uliopita

MABINGWA wa soka Tanzania, Simba SC wamepokea kwa furaha mjini Mwanza walikowasili leo, walkitokea Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kutembeza Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu na pia kucheza mechi za kirafiki.
Msemaji wa Simbs SC, Ezekiel Kamwaga ameiambia BIN ZUBEIRY kutoka Mwanza mida hii kwamba timu imefika salama tayri kwa mchezo wao wa kwanza kesho dhidi ya Toto African na Jumapili itacheza na mabingwa wa Uganda, Express kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Simba imekwenda Mwanza bila nyota wake wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ambao wamekuwa mapumziko hadi Jumatatu.
Hao ni Nahodha Juma Kaseja, Haruna Moshi ‘Boban’, Mwinyi Kazimoto na Amir Maftah ambao walirejea nchini juzi kutoka Msumbuji walipokwenda kucheza na wenyeji wao ‘Mambaz’ katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika (AFCON) zitakazopigwa mwakani nchini Afrika Kusini, ambapo ilitolewa kwa mikwaju ya penalti.


USAILI WAENDELEA JANGWANI

Zoezi la usaili linaendelea katika klabu ya Yanga hivi sasa…tazama picha mbalimbali za zoezi hilo. Hapa ni wazee wa klabu hiyo...

Kamati ya Uchaguzi kazini

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Ridhiwani Kikwete kulia na Mwenyekiti wake Jaji John Mkwawa kushoto wakiendelea na kazi

Ramadhani Mzimba 'Kampira' akiondoka baada ya usaili

Hamisi Kiiza (kulia) akizungumza na rafiki yake Abdulsamad

No comments: