ANGALIA NAMNA MAN UNITED WALIVYOJITAHARISHA KUBEBA UBINGWA: HELKOPTA ILIYOBEBA KOMBE YABADILI NJIA MARA 2 NDANI YA DAKIKA 5
Waliamini kwamba timu yao imefanya kitu kilichoonekana hakiwezekani kwa kuchukua ubingwa wa Barclays Premier League mbele ya majirani zao wenye kelele.
Na haikuwa tu mashabiki bali pia hata helikopta iliyobeba kombe halisi ilikuwa imeanza safari kuelekea Stadium of Light. Hata mabango yaliyokuwa yametengenezwa na United kusherehekea ubingwa yalianza kusogezwa uwanjani.
Lakini maili 140 katika jiji la Manchester, saa ikisoma saa 4.52pm, Edin Dzeko akasawazisha na kufanya ubao wa matokeo kusoma 2-2.
Kule Sunderland, mashabiki walikuwa wamebana pumzi zao mpaka kipenga kilipopulizwa, lakini dakika 3 tu baadae, Sergio Aguero akaingia na mpira ndani ya box na kufunga goli na kukamilisha the best comeback.
Wachezaji wa United, ambayo walibaki uwanjani wakisubiri hukumu yao, waliambiwa juu ya kilichotokea Etihad, na kwa haraka sura zao zikawa na majonzi.
Mixed emotions: Manchester United fans celebrate (above)
but then comes the news from the Etihad (below)
Mixed emotions: Manchester United fans celebrate (above)
but then comes the news from the Etihad (below)
Na baadae washabiki wa United wakaibuka na bango linaloonyesha 19-3, kwa maana ya kuwadhiaki majirani zao ambao ndio kwanza wamebeba ubingwa wa 3 wakati wao wakiwa tayari na ubingwa wa 19.
Stunned: Manchester United players react to the news
that they have lost the Premier League title
JOHN BOCCO NA MBWANA SAMATTA WAITWA STARS!
Kocha Mkuu wa
Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 14 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji
25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya
Afrika dhidi ya Ivory Coast.
Akitangaza
kikosi hicho ambacho kitaingia kambini kesho kutwa (Mei 16 mwaka huu, Kim
amesema uteuzi wake umezingatia uwezo wa mchezaji uwanjani, nafasi anayocheza na
ubora wake.
Wachezaji
walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius
Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki ni Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris
(Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri
Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso
(Simba).
Viungo ni
Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas
Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20),
Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).
Washambuliaji
ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano
(Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).
Stars
inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro
itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi kabla
kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.
No comments:
Post a Comment