Friday, June 22, 2012

YONDANI AANZA MAZOEZI YANGA LEO ASUBUHI LEO

 







Kelvin Patrick Yondan, beki wa kimataifa wa Tanzania, ameanza mazoezi rasmi leo katika klabu yake mpya, Yanga SC. Yondan alitinga maeozini asubuhi na kushangiliwa ile mbaya na mashabiki wa klabu hiyo Uwanja wa Kaunda, Jangwani, Dar es Salaam. Picha tofauti zikimuonyesha Yondan mazoezini nYanga

Picha kwa hisani ya BIN ZUBEIRY.

Thursday, June 21, 2012

CRISTIANO RONALDO AMJIBU RAISI WA BARCA KWA GOLI - AIPELEKA URENO NUSU FAINALI


Czech Republic 0-1 Portugal (Quarter Final) by fasthighlights-2012

KENNETH ASAMOAH ATEMWA YANGA - KULIPWA FIDIA

Hatimaye mshambuliaji wa Yanga kutoka Ghana Kenneth Asamoah ametemwa na klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa takribani msimu mmoja tu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Yanga, Asamoah amefikia makubaliano na Yanga kwa kulipwa fidia ya kuvunjiwa mkataba wake aliousaini msimu uliopita.

Kenneth Asamoah anaondoka Yanga huku akiwaachia wapenzi wa klabu hiyo kumbukumbu ya goli zuri la kichwa alilowafunga Simba kwenye fainali ya kombe la Kagame mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa.

SIKU KAMA YA LEO: WAYNE ROONEY AFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA KWENYE EURO - SPAIN WABEBA UBINGWA WAKWANZA ULAYA 1964

Baada ya kupoteza ushindi dakika za mwisho kwenye mchezo wao ufunguzi wa Euro 2004 kwa Ufaransa, England wakaanza kampeni yao vizuri kwenye mechi ya pili kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Switzerland.


Kijana wa miaka 18Wayne Rooney alifunga mara mbili akijitangaza kwenye ulimwengu wa soka, huku Steven Gerrard akifunga goli la tatu.


England na Rooney waliendeleza mazuri waliyoyafanya siku kama hii, walipokutana na Croatia kwenye mechi ya mwisho ya group. Lakini hayakuanza vizuri kwa vijana wa Sven Goran Eriksson baada ya Niko Kovac kufungagoli la kuongoza kwa Croatia.


Three lions walihangaika mpaka pale kwenye dakika ya 40, Paul Scholes aliposawazisha - goli la mwisho alilofunga kwa ajili ya nchi yake.


Wayne Rooney baadae kafunga bao la pili kabla ya timu mbili kwenda mapumziko. Baadae Frank Lampard akafunga bao la nne.


Ushindi huo ulimaanisha England wameshinda mechi mbili mfululizo za Euro, ikiwa ni mara ya pili kufanya hivyo, baada ya kuwafunga Scotland na Holland mwaka 1996.


Ushindi huo pia uliweka rekodi nyingie baada ya England kuingia robo fainali kwa mara ya kwanza kwenye historia ya michuano hiyo wakati Euro inapofanyika nje ya ardhi ya England.


Pia siku kama ya leo Spain waliifunga Soviet Union na kufanikiwa kushinda kombe la Euro 1964

TETESI HAI - NYUMBANI NI NYUMBANI: MRISHO NGASSA NJIANI KURUDI YANGA

Yanga wameendelea kuonyesha mabavu katika usajili baada ya kumsajili Kelvin Yondani, Nizar Khalfan, Barthez, Domayo na wengine wengi, leo taarifa za usajili kutoka klabu hiyo zinasema kwamba klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Azam ili kuweza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Khalfan Ngassa.

Habari za ndani zinadai kwamba zinadai kwamba Ngassa, Yanga na Azam wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na huenda kesho kutakuwa na habari nzuri kwa wapenzi wa Yanga juu ya kurudi kwa kipenzi chao Ngassa mitaa ya Jangwani.
"Leo saa nne asubuhi Ngassa alifika pale makao makuu ya Yanga na akawa kwenye kikao kizito katibu wa Yanga na mmoja wa wadau wakubwa wa Yanga bwana Seif." - kilisema chanzo cha habari.

Katika usajili huo Yanga wapo tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha na kumtoa kiungo Nurdin Bakary ili kuweza kumtwaa winga huyo ambaye alishwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio kalba ya kuhama kwa uhamisho uliovunja rekodi ya ndani ya usajili baada ya Azam kulipa milioni 60 kwa Yanga na kumtwaa Ngassa

No comments: