Tuesday, October 20, 2015

FIFA yatangaza 23 wanaowania Ballon d'Or..England watoka 'kapa'

The FIFA Ballon d'Or trophy

Na Juma Mohamed.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa kushirikiana na Chama cha Soka Nchini Ufaransa, wametangaza orodha ya wachezaji 23 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia (FIFA Ballon d’Or).
Kutokana na maamuzi ya kamati ya utendaji ya shirikisho hilo na FA ya Ufaransa, wameteua pia orodha ya makocha 10 watakaowania tuzo ya kocha bora katika mchakato wa upigaji kura utakaoanza Oktoba 26 na kumalizika Novemba 20 mwaka huu.
Orodha ya wachezaji waliotajwa kuwania tuzo hiyo kutoka katika vilabu na mataifa mbalimbali ni kama ifuatavyo:-
 Sergio Agüero (Argentina/Manchester City), Gareth Bale (Wales/Real Madrid), Karim Benzema (France/Real Madrid), Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid), Kevin De Bruyne (Belgium/VfL Wolfsburg/Manchester City), Eden Hazard (Belgium/Chelsea), Zlatan Ibrahimović (Sweden/Paris Saint-Germain), Andrés Iniesta (Spain/FC Barcelona), Toni Kroos (Germany/Real Madrid), Robert Lewandowski (Poland/FC Bayern Munich), Javier Mascherano (Argentina/FC Barcelona), Lionel Messi (Argentina/FC Barcelona), Thomas Müller (Germany/FC Bayern Munich), Manuel Neuer (Germany/FC Bayern Munich), Neymar (Brazil/FC Barcelona), Paul Pogba (France/Juventus), Ivan Rakitić (Croatia/FC Barcelona), Arjen Robben (Netherlands/FC Bayern Munich), James Rodríguez (Colombia/Real Madrid), Alexis Sánchez (Chile/Arsenal), Luis Suárez (Uruguay/FC Barcelona), Yaya Touré (Côte d'Ivoire/Manchester City), Arturo Vidal (Chile/Juventus/FC Bayern Munich).
Kwa upande wa makocha waliotajwa kuwania tuzo ya kocha bora wa mwaka ni kama ifuatavyo:-
Massimiliano Allegri (Italy/Juventus), Carlo Ancelotti (Italy/Real Madrid), Laurent Blanc (France/Paris Saint-Germain), Unai Emery (Spain/Sevilla FC), Pep Guardiola (Spain/FC Bayern Munich), Luis Enrique Martínez (Spain/FC Barcelona), José Mourinho (Portugal/Chelsea), Jorge Sampaoli (Argentina/Chilean national team), Diego Simeone (Argentina/Atlético Madrid), Arsène Wenger (France/Arsenal).


No comments: