Oscar Pistorius |
Mwanariadha mlemavu nchini Afrika
Kusini Oscar Pistorius ameruhusiwa kuondoka gerezani mwaka mmoja tu
baada ya kufungwa jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuuwa mpenzi wake
Reeva Steenkamp.
Aliachiliwa huru Jumatatu usiku badala ya
Jumanne kama wengi walivyotarajia. Baada ya kuachiliwa huru, alielekea
kwa mjomba wake Arnold Pistorius.Pistorius ameruhusiwa kukamilisha kifungo chake cha miaka 5, akiwa nyumbani kwake.
Oscar Pistorius |
Kama sehemu ya msamaha huu bingwa huyo wa zamani wa mbio za walemavu atahitajika kukaguliwa kisaikolojia kila baada ya kipindi fulani na hatawahi kuruhusiwa kumiliki bunduki.
Familia yake imekanusha madai kuwa ameachiliwa mapema ikisema kuwa japo hayumo gerezani angali anatumikia kifungo chake nyumbani.
Msemaji wa familia hiyo amesema kuwa hajapunguziwa kifungo na atatumikia kipindi hicho kwa uadilifu kulingana na sheria za taifa.
Hata hivyo bingwa huyo wa zamani anakabiliwa na hatari ya kurejeshwa gerezani iwapo kiongozi wa mashtaka atafaulu kubatilisha uamuzi wa mahakama ya chini iliyompata na hatia ya kuua bila kukusudia Steenkamp.
SOURCE: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment