Sunday, July 27, 2014

DI MARIA KUANZA MAZOEZI AGOSTI 5

Angel Di Maria

Na Juma Mohamed

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, anatarajia Angel Di Maria kuanza mazoezi ya kujiandaa musimu mpya Agosti 5 na hana habari kiungo huyo matata wa Argentina anaondoka kwenda Paris St Germain.
“Hakuna jambo jipya kwenye soko,” Ancelotti alijibu kuhusu ripoti Di Maria yuko karibu kukamilisha uhamisho hadi mabingwa hao wa Ufaransa kwa ada ya Euro milioni 70.
“Di Maria alimaliza Kombe la Dunia na sasa anapumzika. Atarudi Agosti 5 kuanza mazoezi na wenzake,” kocha huyo aliongeza.
Alikuwa akiongea na wanahabari baada ya timu yake kulazwa na Inter Milan kupitia penalty katika mechi ya kirafiki jijini California Jumamosi.
Aliendelea kuwa Real hawatafuti mshambuliaji mwingine baada ya nyota wa Ujerumani, Toni Kroos na kiungo machachari wa Colombia, James Rodriguez.
Straika wa Ufaransa, Karim Benzema, ni tegemeo na Isco anaweza kutumika kama mshambuliaji wa ziada, Ancelotti alisema.
Real wataanza kampeni ya La Liga wikendi ya Agosti 23/24 nyumbani dhidi ya Cordoba waliopanda daraja musimu jana.

SOURCE:SUPERSPORT

No comments: