MSHIKA BUNDUKI WA ZAMANI; Thierry Henry atawavaa Chelsea |
KIKOSI cha nyota wa
Ligi Kuu Marekani (MLS All-Star) kitakacohmenyana na Chelsea kimetajwa, na Thierry
Henry, David
Beckham na Landon
Donovan wamejumuishwa.
Wachezaji wamechaguliwa kwa kura na mashabiki, tayari kwa mechi hiyo dhidi ya The Blues Julai 25, mwaka huu.
Wachezaji watatu wa Sporting Kansas City wamo ndani ya kikosi hicho ambao ni wengi kuliko klabu yoyote, kipa Jimmy Nielsen, kiugno Graham Zusi na beki Aurelien Collin.
KIKOSI CHA All-STAR:
Wachezaji wamechaguliwa kwa kura na mashabiki, tayari kwa mechi hiyo dhidi ya The Blues Julai 25, mwaka huu.
Wachezaji watatu wa Sporting Kansas City wamo ndani ya kikosi hicho ambao ni wengi kuliko klabu yoyote, kipa Jimmy Nielsen, kiugno Graham Zusi na beki Aurelien Collin.
KIKOSI CHA All-STAR:
Jina | KLABU |
Makipa: | |
Jimmy Nielsen | Sporting Kansas City |
Mabeki: | |
Steven Beitashour | San Jose Earthquakes |
Aurelien Collin | Sporting Kansas City |
Jay DeMerit | Vancouver Whitecaps FC |
Heath Pearce | New York Red Bulls |
Viungo: | |
David Beckham | LA Galaxy |
Dwayne De Rosario | D.C. United |
Landon Donovan | LA Galaxy |
Graham Zusi | Sporting Kansas City |
Washambuliaji: | |
Thierry Henry | New York Red Bulls |
Chris Wondolowski | San Jose Earthquakes |
NANE BORA COPA COCA COLA KESHO
Na Prince Akbar
ROBO Fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012
inayokutanisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 inaanza kesho (Julai 10 mwaka
huu) kwa timu nne kuumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es
Salam.
Temeke na Mjini Magharibi ndizo zitakazocheza robo fainali
ya kwanza kuanzia saa 2.30 asubuhi. Mara iliyoivua ubingwa Kigoma itacheza robo
fainali ya pili dhidi ya Morogoro kwenye uwanja huo huo.
Robo Fainali ya tatu itachezwa keshokutwa (Julai 11 mwaka
huu) kwa kuzikutanisha timu za Kinondoni na Mwanza. Mechi hiyo itaanza saa 2.30
asubuhi na kufuatiwa na nyingine kati ya Dodoma na Tanga itakayoanza 10 kamili
jioni.
Nusu fainali ya michuano hiyo iliyoanza Juni 24 mwaka huu
katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ikishirikisha timu 28 itafanyika Julai 13
mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Mshindi wa mechi kati ya Temeke na Mjini Magharibi, na
Kinondoni dhidi ya Mwanza ndiyo watakaocheza nusu fainali ya kwanza. Nusu
fainali ya pili itakuwa mshindi wa mechi ya Mara na Morogoro dhidi ya mshindi wa
mechi ya Dodoma na Tanga.
Fainali itafanyika Jumapili (Julai 15 mwaka huu). Mechi
zote kuanzia hatua ya robo fainali hadi fainali zitafanyika kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume.
TWANGA PEPETA KUPAMBA MISS SINZA
Na Princess
Asia
WAKATI bendi ya African Stars
(Twanga Pepeta) itapamba shindano la kumsaka mrembo wa Redds Miss Sinza 2012
lillopangwa kufanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Mawela Social (Ten Star Lounge)
uliopo karibu na hotel ya Vatican City, Kamati ya Miss Tanzania leo itatembelea
warembo hao kwa lengo la ‘kuwafunda’ tayari kupanda
jukwaani.
Mratibu wa kampuni ya Calapy
Entertainment, Majuto Omary ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba Twanga Pepeta
imeandaa zawadi kwa mashabiki wake na wale wa urembo kwa kuwapa uhondo wa nyimbo
mbili mpya ambazo zitakuwa zinasikika kwa mara ya kwanza
jukwaani.
Nyimbo hizo ni Mapambano ya
Maslahi uliotungwa na Muumin Mwinjuma, Shamba la Twanga ambao umetungwa na
Greyson Semsekwa na mmoja ambao haujapewa jina uliotungwa na Jumanne Saidi
ambaye amfunga ndoa na mnenguaji wa bendi hiyo, Asha
Sharapova.
Alisema kuwa nyimbo hizo ni
zawadi kwa mashabiki wa Twanga wa Sinza na vitongoji vyake kwani bendi hiyo
haijafanya shoo huko muda mrefu.
“Tunatarajia kuwa na shoo
nzuri kutoka kwa warembo na bendi ya Twanga Pepeta ambayo mwaka huu imeshinda
tuzo mbili katika tuzo za muziki Tanzania,” alisema.
Kuhusiana na ziara ya Kampuni
ya Lino International Agency, Majuto alisema kuwa Lundenga na wenzake watafanya
mazungumzo na warembo hao baada ya mazoezi yao ya
pamoja.
Alisema kuwa ziara hiyo ni
moja ya faraja kwa warembo na kamati ya Miss Sinza kutokana na ukweli kuwa ujio
wao ni wa Baraka na hitimisho la mashindano ya vitongoji
nchini.
“Miss Sinza ndiyo inafunga
pazia la mashindano ya Vitongoji (vituo) nchini, Lundenga na wenzake wanakuja
kutoa baraka zao kabla ya kuanza pilikapilika za Redds Miss Tanzania,”
alisema.
Shindano hilo lililodhaminiwa
na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Kidoti Fashion, Clouds Entertainment,
sufianimafoto.blogspot.com, Lady Pepeta na flexi P, Fredito Entertainment,
Screen Masters, Brake Point na Jackz Cosmetics Kinondoni.
YANGA NA JKT RUVU TAIFA KESHO, MTIHANI WA KWANZA WA MTAKATIFU THOM
Sunday, July 8, 2012
AZAM, SIMBA KAZINI ZANZIBAR LEO
MASHINE; Sunzu, ataibeba simba na leo? |
Na Prince
Akbar,
MICHUANO ya Kombe la Urafiki
visiwani Zanzibar, leo inafikia hatua ya Nusu Fainali kwa mechi mbili kupigwa
kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC
watacheza na Zanzibar All Stars kuanzia saa 2:00 usiku, wakati Azam FC
watamenyana na Super Falcon kuanzia saa 10:30
jioni.
Azam na Simba, zote zimefuzu
kutoka Kundi A wakati All Stars na Falcon zimetokea Kundi B, lililokuwa na Yanga
pia, ambayo iliondolewa kwa kupeleka watoto.
Simba SC ni mabingwa wa Bara,
Falcon ni mabingwa wa Zanzibar, Azam FC ni mabingwa wa Kombe la Mapinduzi na
washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Bara wakati Falcon inaundwa na mseto wa
wachezaji nyota wa Zanzibar.
Katika mechi yake ya mwisho ya
Kundi A, Simba iliifunga kwa taabu Karume Boys 1-0, bao pekee la mshambuliaji
wake Mzambia, Felix Mumba Sunzu Jr, wakati Azam iliifunga Mafunzo
3-2.
ADEBAYOR WA CHAMAZI; Ataibeba Azam leo? |
Kuna uwezekano mkubwa Simba na
Azam zikakutana katika Fainali Jumatano, kwani zinapewa nafasi kubwa ya kushinda
mechi zao leo, ingawa pia haitarajiwi kuwa kazi nyepesi kwani timu za Zanzibar
nazo zimeimarika siku za karibuni.
Katika mchezo wa leo, huanda
kocha wa Simba Profesa Milovan Cirkovick akapanga kikosi hiki; Juma Kaseja,
Haruna Shamte, Paul Ngalema, Lino Masombo, Shomary Kapombe, Amri Kiemba/Edward
Chirtopher, Mwinyi Kazimoto/Salim Kinje, Mussa Mudde/Jonas Mkude, Felix
Sunzu/Abdallah Juma, Kanu Mbivayanga/ Uhuru Suleiman na Danny Mrwanda/Abdallah
Seseme.
Kwa upande wa Azam,
inawezekana Stewart Hall, akawapanga: Deo Munishi ‘Dida’, Samir Hajji Nuhu,
Ibrahim Shikanda, Said Mourad, Joseph Owino, Abdulhalim Humud, Kipre Herman
Tcheche, Kipre Michael Balou, Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Gaudence Mwaikimba na
George Odhiambo ‘Blackberry’/Hamisi Mcha.
CHELSEA WAGONGA MWAMBA UJERUMANI, WENGER AENDELEA KUSAJILI MAKINDA
Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya
CHELSEA WAGONGA MWAMBA UJERUMANI
KLABU ya Bayer Leverkusen
imeitupilia mbali ofa ya Chelsea kwa mshambulaji wao mwenye umri wa miaka 21,
Andre Schurrle.
KOCHA
Alan Pardew amesema kwamba anafanya kila atakachoweza kuhakikisha anambakiza
mshambuliaji Demba Ba, mwenye umri wa miaka 27, katika klabu ya Newcastle.
TOTTENHAM
Hotspur inataka kutoa dai la pauni Milioni 5 kumsajili mshambuliaji mwenye umri
wa miaka 22, Daniel Sturridge wa Chelsea.
KIUNGO
wa Arsenal, Aaron Ramsey, mwenye umri wa miaka 21, amesema kwamba yeye na
wachezaji wenzake hawajui mambo yatakuwaje mshambuliaji wao Robin van Persie
akiondoka.
KOCHA
wa Swansea City, Michael Laudrup anajaribu kumsajili winga wa Bristol City,
Albert Adomah kutoka Ghana mwenye umri wa miaka 24, usajili ambao unaweza
kumgharimu pauni Milioni 3.
KOCHA
Roberto Mancini yupo karibu kusaini mkataba mpya na Manchester City, licha ya
Chama cha Soka Urusi kutenga kitita kizito kujaribu kumnasa.
KLABU
ya Liverpool imekula za uso tena, baada ya kukataliwa kuuziwa kiungo mwenye umri
wa miaka 25, Esteban Granero na Real Mdrid.
KLABU
ya AC Milan imesema ni bora kumchukua kwa mkopo kuliko kumnunua jumla
mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23.
KLABU
ya Fiorentina inamtaka mshambuliaji wa kimataifa wa Morocco, Marouane Chamakh,
mwenye umri wa miaka 28, ambaye anajiandaa kuondoka Arsenal baada ya mambo
kumuendea ovyo.
KOCHA
wa Wigan, Roberto Martinez anamtaka winga wa Chicago Fire, raia wa Guatemala,
Marco Pappa, mwenye umri wa miaka 24 azibe nafasi ya mchezaji anayetakiwa na
Chelsea, Victor Moses.
KLABU
ya Arsenal nayo ipo kwenye mkakati wa kumnunua mchezaji wa Wigan, Victor Moses,
mwenye umri wa miaka 21.
KLABU
ya Norwich imetoa ofa kwa ajili ya mshambuliaji wa Canaries, James Vaughan,
mwenye umri wa 23, kwa Birmingham kuwasaidia kumbakiza beki wa kati, Curtis
Davies, mwenye umri wa miaka 27.
SPURS MIKONONI MWA AVB
KIKOSI
cha Tottenham Hotspur sasa kipo kamili chini ya kocha mpya, Andre-Villas Boas,
kwa mujibu wa Danny Rose, mwenye umri wa miaka 22.
KOCHA
Roberto Mancini aliepuka mapokezi wakati kikosi cha Manchester City kilipowasili
katika kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Austria, kulingana na tetesi
zinazozagaa kuhusu mustakabali wake.
DZEKO NA ANGELINA JLIE...
MSHAMBULIAJI
wa Manchester City, Edin Dzeko ameungana na mwigizaji nyota wa Hollywood,
Angelina Jolie katika zuli jekundu kwenye tamasha la filamu mjini
Sarajevo.
TAZAMA MAVITUUZ YA SAMATTA CAIRO JANA
Samatta kama Messi |
Samatta shujaa |
rafu |
Kipute |
Kipute |
11 walioanza |
Kipute |
Kidiaba anadaka |
11 walioanza Ahly |
Mtu anatoroka |
Mishemishe |
Kidiaba anaosha |
Ufundi mtupu |
AZAM ACADEMY YAFANYA MAUAJI BURUNDI
Kikosi cha Azam Academy |
Na Princess
Asia
TIMU ya soka ya vijana ya Azam
FC, maarufu kama Azam Academy imeanza vema michuano ya vijana Afrika Mashariki
na Kati, Rollingston baada ya kuifunga mabao 3-0 Nyirakongo Academy ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) miji Bujumbura
jana.
Mabao ya Azam yalifungwa na
Kimwaga mawili na lingine Mudathir.
Katika mchezo huo, kikosi cha
Azam kilikuwa; Aishi, Mgaya, Shabalala, Dizana, Mkomola, Reyna, Mudathiri,
Kaijage, Machuppa, Kelvin na Kimwaga.
Simba na Yanga zilialikwa pia
kwenye michuano hiyo, ila zote zimejitoa dakika za mwishoni.
SAMATTA AIFUNGIA BAO TP MAZEMBE USIKU HUU MISRI
Samatta akiwa n a jezi ya Taifa Stars |
MBWANA Ally Samatta,
mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, usiku huu ameifungia bao moja Tout
Puissant Mazembe ya DRC, ikilala 2-1 mbele ya wenyeji Al Ahly katika mchezo wa
Kundi B wa Ligi ya mabingwa Afrika, uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Jeshi,
mjini al-Qahirah, Cairo, Misri.
Mshambuliaji huyo wa zamani
wa Simba SC, alifunga bao hilo dakika ya 85, akiunganisha pasi ya Kasusula,
ikiwa ni dakika 20 tu tangu aingie uwanjani akitokea benchi kwenda kuchukua
nafasi ya Lungu.
Mabao ya wenyeji yalifungwa
na Emad Moteab dakika ya 12, pasi ya Waleed Soliman na Gedo dakika ya pili ya
muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida za mechi hiyo,
akiunganisha pasi ya Sayed Moawad.
No comments:
Post a Comment