Sunday, July 27, 2014

THIERRY HENRY APUUZA TAARIFA ZA KUSTAHAFU

Thierry Henry
Na Juma Mohamed

Staa wa zamani wa Arsenal na Ufaransa, Thierry Henry, amepuuzilia taarifa kuwa atastaafu kutoka kandanda baada ya mkurugenzi wa klabu chake cha sasa New York Red Bulls Gerard Houllier, kutangaza kuwa anatarajia nyota huyo kufungia mchezo wake pazia.
“Alisema hivyo? Tutazumgumza mwishoni wa musimu,” Henry alisema baada ya timu yake ya ligi kuu Marekani kuwalaza waajiri wake wa kitambo Arsenal 1-0 kwenye mechi ya kirafiki Jumamosi.
Alipozidi kuulizwa, mchezaji huyo maarufu duniani alikataa kutoa maoni ikiwa atongezea mwaka mmoja kwa kandarasi yake ya sasa.
Henry alicheza dakika 54 kwenye mechi hiyo na aliunganishia Bradley Wright-Phillips bao la ushindi mbele ya mashabiki zaidi ya 25,000.
Mechi hiyo ilichukua mwelekeo wa kuwa kama thifa ya kumuaga rasmi kwani mashabiki walizindua kibango kikubwa chenye picha yake akiwa na jezi ya Arsenal and Red Bulls.
Mkataba wake na timu hiyo unafikia kikomo mwisho wa musimu huu wa ligi ya Marekani na Henry, 36, anatarajiwa kustaafu na Houllier baada ya tetesi mingi kuwa angefanya uamuzi huo hivi karibuni.
Henry amefungia Red Bulls mabao 46 na kuunganisha mengine 40 katika mechi 116 alizochezea timu hiyo baada ya kuhamia huko kufuatia kutetemesha dunia kama straika anayeshikilia rekodi ya mabao Arsenal na kutwaa Ligi ya Mabingwa na Barcelona.
Alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia 1998.

SOURCE:SUPERSPORT

No comments: