Sunday, July 27, 2014

ROONEY APIGA 2, UNITED IKIIUA ROMA 3-2

Wayne Rooney,
Na Juma Mohamed

Magoli mawili kutoka kwa mshambuliaji wa Uingereza, Wayne Rooney, yalisaidia Manchester United kuwachakaza AS Roma 3-2 katika mechi ya kombe la kimataifa iliyosakatwa jijini Denver.
Rooney aliibuka shujaa wa mechi baada ya kuunganisha mpira uliochongwa na Juan Mata na kuifungia United goli la tatu na kufanya mambo 3-0 lakini United, ambao waliezeka Los Angeles Galaxy kichapo cha 7-0 Jumatano waliruhusu wapinzani wao kupenya ngome dakika za mwisho mwisho.
Bao la hali ya juu kutoka kwa Miralem Pjanic lililofungwa kutoka hatua kumi kutoka duara wa katikati kutoka upande wa Roma dakika ya 75 na penalty ya gwiji Francesco Totti yalitingisha dau la United lakini waliweza kukamilisha ushindi wa 3-2.
Rooney aliwapatia uongozi dakika ya 36 baada ya kupinda mpira kimyani baada ya kulishwa na Mata kabla ya kurudisha shukrani na kuunganishia kiungo huyo wa Uhispania la pili dakika tatu baadaye aliimaliza kwa kumvisha kipa Lukasz Skorupski kanzu maridadi.
Rooney alitinga lake la pili kupitia penalty sekunde za mwisho za kipindi cha kwanza.
Kwingineko, Arsenal waliibuka timu ya kwanza ya ligi ya Premier kupoteza mechi Marekani musimu huu wa kiangazi baada ya Bradley Wright-Phillips kufunga bao la kipkee na kuinua timu yake New York Red Bulls kuandikisha ushindi wa 1-0.
Mabingwa wa Uropa, Real Madirid walishindwa kupitia penalty na Inter Milan baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 baada ya muda wa kawaida.
Gareth Bale alifunga la kwanza  kipindi cha kwanza kabla ya Mauro Icardi kusawazisha cha pili.

SOURCE:SUPERSPORT

No comments: