Wednesday, June 13, 2012

ALI HASSAN MWINYI MGENI RASMI TUZO ZA TASWA


RAIS mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya ya utoaji tuzo za wanamichezo bora wa mwaka 2011 zinazotolewa na Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) zitakazofanyika kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubillee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taswa Juma Pinto alisema jana kwamba, chama chake kimeualika Mwinyi kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya michezo hapa nchini.
Alisema maandalizi kwa ajili ya hafla hizo zilizodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries, yanaendelea vema ambapo kituo cha televisheni cha ITV kitarusha Live tukio hilo.
Mshindi wa jumla atazawadiwa kitita cha shilingi milioni 12.5 ambapo wanaowania katika mpira wa kikapu kwa upande wa wanawake ni pamoja na Doritha Mbunda, Evodia Kazinja (JKT Queens), Faraja Malaki (Jeshi Stars), huku kwa upande wa wanaume ni Alpha Kisusi, (Vijana), Filbert Mwaipungu, Gilbert Batungi (ABC), wakati Liliam Sylidion na Doritha Mbunda watachuana katika Netiboli.
Kwa upande wa gofu wanaowania ni Madina Iddi ,Hawa Wanyeche ,Ayne Magombe kwa upande wa wanawake,wakati kwa wanaume ni Frank Roman,Nuru Mollel na Issac Anania kwa upande wa Wabaume, huku gofu ya kulipwa ni Fadhili Saidi Nkya, Yasini Salehe na Hassani Kadio.
Ahmada Bakar,Amina Daud Simba (kisahani na tufe),Othman Ally Othman (mkuki, kisahani na tufe) wanawania kwa upande wa Olimpki maalum, huku katika Paralimki ni Zaharani Mwenemti, Joseph Nziku, Yohana Mwila kwa upande wa Wanawake, wakati Faudhia Chafumbwe, Siwema Kilyenyi na Janeth Madise watachuana kwa upande wa wanawake.
Katika ngumi za ridhaa mchuano utakuwa kati ya Suleiman Kidunda,Victor Njaiti na Abdalah Kassim,huku kwa upande wa waogeleaji (Wanawake) ni Magdalena Moshi, Gouri Kotecha, na Mariam Foum na kwa wanaume ni Amaar Ghadiyali na Omary Abdallah.Judo itawaniowa na Mbarouk Seleman Mbarouk, Mohammed Khamis Jumana Azzan Hussein Khamis.
Wavu (Wanawake) itawaniwa na Zuhura Hassan, Theresia Ojode (JESHI STARS DAR)na Everlyne Albert wa magereza, huku kwa upande wa Wanaume ni Mbwana Ally, ( MZINGA CORPORATION – MOROGORO),Kevin Peter (MAGEREZA – DAR),Farhan Abubakar ( MAFUNZO ZNZ) na katika ngumi za kulipwa ni Benson Mwakyembe,Nasibu Ramadhan,Francis Cheka,Nassib Ramadhan na Fadhil Majia.
Watakaowani Tenisi kwa upande wa Wanaume ni Waziri Salum, Omary Abdallah,Hassan Kassim, wakati Wanawake ni Rehema Athuman, Mkunde Iddy na Violet Peter.Baiskeli ni Sophia Hussein,Sophia Anderson kwa upande wa Wanawake, huku Richard Laizer naHamisi Hussein watachuna kwa upande wa wanaume.
Tuzo ya wachezaji wanaocheza nje itawaniwa na Henry Joseph,Mbwana Samatta-Soka, Sophia Mwasikili (Soka), huku ile ya mchezaji bora chipukizi itwaniwa na Theresia Ojode- wavu (Jeshi Stars),Shomari Kapombe (soka) SIMBA na Salum Abubakari-Azam (soka), wakati mchezaji wan je anayecheza Tanzania ni Haruna Niyonzima-Yanga,Kipre Tchetche-Azam,Emmanuel Okwi-Simba (soka).
Aidha, tuzo ya mwanasoka kwa wanawake itawaniwa na Asha Rashid,Mwanahamisi Omary (Mburahati Queens),Fatuma Mustapha (Sayari),Eto Mlenzi (JKT), wakati kwa upande wa wanaume ni John Bocco,Aggrey Morris-Azam na Juma Kaseja-Simba, huku katika Riadha Wanawake ni pamoja na Zakia Mrisho,Mary Naali na Jaqueline Sakila wakati kwa upande wa Wanaume ni Dickson Marwa na Alphonce Felix.
Mikono Wanawake ni Abinery Kusencha (JKT Ruvu),Kazad Mtong (Magereza Kiwira) na Faraji Shaibu Khamis (Nyuki Zbar), huku kwa upande wa Wanaume ni Doris Mangara-(Magereza Kiwira),Zakia Seif (Ngome Dar),Mary Kimiti (Magereza Kiwira) na .Kriketi Wanawake itawaniwa na MoniCa Pascal,Asha Daudi na Esther Wallace, huku Wanaume ni Kassimu Nassoro,Benson Mwita na Riziki Kiseto.

TAIFA STARS YAJIPANGA KUIKABILI MSUMBIJI


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema ili kuitoa Msumbiji ‘Mambas’ kwenye michuano ya Afrika ni lazima timu yake ishinde mechi ya marudiano itakayochezwa Juni 17 mwaka huu jijini Maputo.
Mechi ya marudiano kusaka tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa ulioko Zampeto nje kidogo ya Jiji la Maputo kuanzia saa 9 mchana kwa saa za huko.
Kim amewaambia Waandishi wa Habari leo (Juni 13 mwaka huu) kuwa maandalizi ya kikosi chake yanakwenda vizuri ingawa ana wachezaji watatu ambao ni majeruhi; kipa Mwadini Ali, na mabeki Nassoro Masoud Cholo na Waziri Salum.
Amesema wachezaji hao hawatakuwemo kwenye msafara wa timu hiyo utakaoondoka Juni 15 mwaka huu saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi.
Kocha huyo amesema baada ya mechi tatu maendeleo kiuchezaji kwa timu yake inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ni mazuri ingawa bado anafanyia kazi kwa nguvu safu ya ushambuliaji. Mechi iliyopita Taifa Stars iliifunga Gambia 2-1 huku mabao yote yakifungwa na mabeki.
Iwapo Taifa Stars itaitoa Msumbiji katika raundi ya mwisho itapangiwa moja kati ya timu 16 zilizocheza Fainali za AFCON zilizofanyika Januari mwaka huu katika nchi za Gabon na Equatorial Guinea. Katika mechi ya kwanza dhidi ya Msumbiji iliyochezwa Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Taifa Stars ambayo msafara wake utakuwa na wachezaji 20 itaagwa kesho (Juni 14 mwaka huu) saa 6 mchana kambini kwao- hoteli ya Accommondia (Tansoma) jijini Dar es Salaam. Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa ajili ya kujenga afya kupitia mpira wa miguu.

WAAMUZI KOZI YA FIFA KUPIMWA UFAHAMU WA ALAMA


Waamuzi 54 wanaoshiriki kozi ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyoanza Juni 11 mwaka huu, kesho (Juni 14 mwaka huu) watahamia Uwanja wa Karume kwa ajili ya mazoezi ya alama (signals). Mazoezi hayo yatafanyika kuanzia saa 1-4 asubuhi.
Kozi hiyo itakayomalizika kesho (Juni 14 mwaka huu) inaendeshwa na wakufunzi Carlos Henriques na Mark Mizengo kutoka FIFA wakisaidiwa na wakufunzi wengine wanne wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Wakufunzi wa TFF ni Kapteni mstaafu Stanley Lugenge, Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala.
Waamuzi wanaoshiriki ni 14 wa Tanzania wenye beji za FIFA ambao ni Erasmo Jesse, Ferdinand Chacha, Hamis Changwalu, Hamis Maswa, Israel Mujuni, John Kanyenye, Josephat Bulali, Judith Gamba, Mwanahija Makame, Oden Mbaga, Ramadhan Ibada, Saada Tibabimale, Samuel Mpenzu na Sheha Waziri.
Washiriki wengine ni 20 wa daraja la kwanza (class one), kati ya hao watano wanatoka Zanzibar. Lakini vilevile wapo waamuzi chipukizi (watoto) 20 ambao mwaka jana walitumika katika michuano ya Kombe la Uhai na Copa Coca-Cola.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MISS DAR INTER COLLEGE KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA J'MOSI


Na Mwandishi Wetu
WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012 jumamosi hii wanatarajiwa kutembelea makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kujifunza.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi huo wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkatabala na chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) Juni, 22 mwaka huu.
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail, alisema ziara hiyo itawasaidia sana warembo hao katika harakati zao za kielimu.
Alisema Makumbusho ya Taifa ni sehemu muhimu kwa kila Mtanzania kufahamu kutokana na kuwepo vitu vingi vya kihistoria vilivyopata kutokea katika karne zilizopita.
Kama mjuavyo kule kuna kuna fuvu la mtu wa kwanza duniani (zinjathropas), vyombo, magari na vitu vingine vya kwanza kuanza kutumika,”alisema.
Dina aliongeza kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo washiriki 13 kutoka vyuo vya IFM, Ustawi wa Jamii, Chuo Cha Biashara (CBE), uandishi wa Habari (DSJ) na Huria (OUT) wanaendelea na mazoezi kwenye hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Warembo hao ambao wapo chini ya ukufunzi Marlydia Boniface na Bob Rich ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd’s Original, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Shear Illusions, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.


KUONA TWIGA STARS, ETHIOPIA 2,000/-


Kiingilio cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Ethiopia itakayochezwa Jumamosi (Juni 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 2,000.
Kiwango hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu, kijani na rangi ya chungwa. Viti hivyo kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 48,590 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua washabiki 60,000.
Viingilio vingine kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni sh. 5,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 10,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi kuanzia saa 3 asubuhi.
Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi Grace Msiska atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Bernadettar Kwimbira, Happiness Mbandambanda na Linda Chikuni, wote kutoka Malawi. Kamishna ambaye anatoka Kenya ni Maqulate Atieno. Waamuzi hao wanawasili leo.

JAPHERT KASEBA KUZIPIGA NA FRANCIS CHEKA SIKU YA SABA SABA

Mabondia, Francis Cheka (kushoto) na Japhert Kaseba, wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao unaotarajia kufanyika Siku ya tarehe saba mwezi wa saba katika uwanja mpya wa taifa .Picha na Maktaba ya www.superdboxingcosach.blogspot.com)
Ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii nchini wakiongozwa na Diamond pia kutakua na mechi ya Bongo Move na wasanii wa Bongo Fleva watakapochuana kwa mara nyingine katika mpambano uho ulioandaliwa na Global na kuratibiwa na Kaike Siraju utakuwa ni mpambano wa kwanza wa Masumbwi kufanyika katika uwanja mpya wa Taifa

Baadhi ya mabondia watakaosindikiza mpamnbano huo ni Adiphoce Mchumia tumo atakaedundana na Ramadhani Kido wakati Amos Mwamakula ataoneshana kazi na Rashini Ali uku Mkongo Kanda Kabongo akizipiga na Said Mbelwa wakati bondia chipkizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala inayonolewa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli Masta na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'Super D' watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

No comments: