Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya

JUVE WAANZA MZUNGUMZO NA VAN PERSIE, MSHENGA NEDVED

KLABU ya Juventus imempeleka Mkurugenzi wake na mchezaji wake wa zamani, Pavel Nedved akakutane mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28, kujadili suala la kuhamia kwake Turin.
KLABU za Manchester City na Chelsea zinakabaliwa na upinzani wa mabingwa wa Serie A, Juventus katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani, mwenye umri wa miaka 25.
Salomon Kalou
Salomon Kalou atatua Liverpool
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea, Salomon Kalou, mwenye umri wa miaka 26, atakuwa wazi kwenda Liverpool kuungana na kocha wa zamani wa The Blues, Brendan Rodgers, kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo.
KLABU ya Liverpool imeambiwa kwamba mshambuliaji mwingine wanayemtaka wa Barcelona, Cristian Tello, mwenye umri wa miaka 20, atawagharimu pauni Milioni 7.
KLABU ya Chelsea inamtaka mshambuliaji wa Malaga, Salomon Rondon, mwenye umri wa miaka 22, ili arithi mikoba ya Didier Drogba.
KLABU ya West Ham inajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Blackburn, Yakubu, mwenye umri wa miaka 29, ambao anaweza kuwagharimu The Hammers pauni Milioni 1.

MOYES KUMRITHI HARRY SPURS

David Moyes
David Moyes kurithi mikoba ya Harry Redknapp
KLABU Ya Tottenham ina mpango wa kumchukua kolcha wa Everton, David Moyes ili mbadala wa Harry Redknapp, aliyetupiwa virago.
KOCHA wa zamani wa Charlton, Alan Curbishley na kocha wa zamani wa Hull na Preston, Phil Brown wote wamo kwenye orodha ya walimu wanaotarajiwa kurithi mikoba ya Chris Hughton katika klabu ya Birmingham City.
MKURUGENZI wa akademi ya Crewe, Dario Gradi anaamini mchezaji mpya wa Manchester United, Nick Powell, mwenye umri wa miaka 18, ana dalili za kutosha za kuwa kama Eric Cantona au Wayne Rooney kwa mafanikio kwa Mashetani hao Wekundu.