Saturday, December 10, 2016

Malori zaidi ya 600 ya Dangote yawasili Bandari ya Mtwara tayari kwa kuanza kazi..


Meli ya MV Morning Composer iliyobeba Malori ya mwekezaji wa kiwanda cha Saruji cha Dangote Industries Ltd Mtwara, Al Hadj Aliko Dangote, ambayo yanatarajiwa kuanza kubeba Saruji kutoka kiwandani hapo na kuisambaza maeneo mbalimbali nchini. Jumla ya Malori 651 yanashushwa usiku huu katika Bandari ya Mtwara. Bandari hiyo kwa mara ya kwanza toka kujengwa kwake mwaka 1950 inaanza kushusha Magari. Meli hiyo ina urefu wa Mita 200, huku Meli nyingine yenye Malori kama hayo zaidi ya 400 inatarajiwa kutia nanga kesho mapema baada ya Meli ya sasa kumaliza kushusha mzigo.

Meli ya MV Morning Composer iliyobeba Malori ya mwekezaji wa kiwanda cha Saruji cha Dangote Industries Ltd Mtwara, Al Hadj Aliko Dangote, ambayo yanatarajiwa kuanza kubeba Saruji kutoka kiwandani hapo na kuisambaza maeneo mbalimbali nchini.

No comments: