Tuesday, September 27, 2016

DC Newala amaliza kwa siku Tatu tatizo la maji lililodumu kwa miaka 12.


Mkuu wa wilaya ya Newala Aziza Mangosongo akifurahi pamoja na wananchi wa vijiji vya Mnali na Mapinduzi wilayani humo waliosota kwa miaka 12 bila kupata maji safi na salama.



JUMA MOHAMED, MTWARA.

Baada ya kusota kwa muda wa miaka 12 bila kupata huduma ya maji safi na salama, wananchi wa vijiji vya Mnali na Mapinduzi tarafa ya Kitangali halmashauri ya wilaya ya Newala, sasa wameondokana na kero hiyo kwa jitihada za mkuu wa wilaya ya Newala Aziza Mangosongo.
Wananchi hao ambao awali walilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji, wameamua kuandaa hafla ya mapokezi na kumpongeza mkuu wa wilaya huyo pamoja na kumkabidhi zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mbuzi na Korosho, kwa kufanikisha kupatikana kwa huduma hiyo katika vijiji hivyo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mnali, Salehe Masoud, amesema wananchi wa vijiji hivyo waliamua kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya kuwasilisha kero hiyo ndipo mkuu wa wilaya alipoamua kwenda kuweka kambi ya siku Tatu akiwa na timu yake mpaka walipofanikisha kutatua changamoto hiyo.
Wananchi wa vijiji hivyo wamemuahidi kumpatia chumba mkuu huyo wa wilaya ili apumzike na kupata Baraka za wazee, pindi akiwatembelea katika shughuli zake za kiutendaji.

No comments: