Mmoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wa wadau wa tasnia ya korosho uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Sanaa-Bgamoyo, akitoa mchango wake. |
Mbunge wa Mtwara mjini-Hawa Ghasia, akizungumza jambo katika mkutano mkuu wa wadau wa tasnia ya korosho uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Sanaa-Bgamoyo. |
Na Juma Mohamed, Bagamoyo.
BAADA ya
mkutano mkuu wa wadau wa tasnia ya korosho nchini kutangaza bei dira ya zao
hilo kwa msimu mpya wa 2016/2017 kuwa ni shilingi 1,300 kwa korosho daraja la
kwanza na 1,040 kwa daraja la pili, baadhi ya wakulima wa zao hilo wameonesha kuiunga mkono bei
hiyo.
Wakizungumza
baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika mjini Bagamoyo, wakulima hao Juma
Mgeno na Rukia Omary, wanasema bei hiyo imezingatia hali ya masoko ilivyo huku
wakitaraji kuwa itapanda wakati wa minada.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa wadau wa tasnia ya korosho uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Sanaa-Bgamoyo, wakifuatilia kwa karibu mkutano. |
“Bei dira
kwa hali ilivyo ninavyofahamu mimi naizungumzia kama ni muwafaka tu naikubali
kwasababu kwa jinsi ambavyo bei zetu zilivyo tukiweka bei ya juu matajiri
watakimbia matokeo yake kuna mwaka 2010 ilituyumbisha sana bei..” alisema Juma
Mgeno,mkulima kutoka mkoani Tanga.
Kwa upande
wake, mkurugenzi wa bodi ya korosho nchini, Mfaume Juma, aliwashukuru wajumbe
wa mkutano huo kwa kukubaliana kwa pamoja kuipitisha bei hiyo, huku makamu
mwenyekiti wa bodi, Mudhihiri Mudhihiri akifafanua kuhusu hatua
zitakazochukuliwa kwa waliohusika na upotevu wa fedha za wakulima kiasi cha sh.
Bilioni 17.
Mrajisi mkuu wa vyama vya ushirika, Audax Rutabanzibwa, akifafanua baadhi ya hoja kaika mkutano mkuu wa wadau wa tasnia ya korosho uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Sanaa-Bgamoyo. |
“Mheshimiwa
mwenyekiti nichukue fursa hii kuwashukuru wajumbe wa mkutano wa wadau kwa kuona
uhalisia wa jambo tuliopendekeza kuwa sh. 1,300 kwa kilo katika msimu huu
unaokuja kwa daraja la kwanza..” alisema Mfaume.
“Wajumbe
hawa wanataka taarifa yetu ifanyiwe kazi na wahusika wote wachukuliwe hatua,
kila takaechangia anachotaka ni hicho..lakini nikuhakikishieni zaidi hatua
zitachukuliwa, msimu huu tumebana kila nafasi ya watu kuendelea kupata mapato
nje ya utaratibu..” alisema Mudhihiri.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Omary Kipanga (wakwanza kushoto) akifuatilia kwa karibu mkutano wa wadau wa tasnia ya korosho uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Sanaa-Bgamoyo |
Kiasi hicho
cha fedha kilichotajwa na bodi kinatofautiana na kilichotajwa na Taasisi ya
kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini TAKUKURU kiachoonesha kuwa ni sh. Bilioni
30, kutokana na kutofautiana katika kufanya uchunguzi.
No comments:
Post a Comment